Huu Mwenge usiwe unakimbizwa Dar es Salaam, unatuchosha na kutupotezea muda

Mwenge wa uhuru ni kielelezo cha uhuru wa Tanzania, ni taa yenye kumulika nchi na miradi yake.

Ni nyota inayotukumbusha kwamba uhuru ni jambo muhimu na la kipekee kwa binadamu aliye kamili.

Hivyo basi hata hapo kwenye foleni yakupasa uwe na fikra chanya ya kutafakuri uzuri na ubora wa Mwenge na siyo kwamba unapoteza muda.

Ni muhimu kila Mtanzania akaguswa na Mbio za Mwenge, ukiwemo wewe uliyeguswa ukiwa kwenye foleni.

Usijinunishe bali furahi na tafakari huu utamaduni wetu adhimu wa kuukimbiza Mwenge wa Uhuru.

Sema Mwenge oyeeeeee
Aliye kuroga wewe alikufa kama angekuwa tupo hai angekuonea huruma
 
Imagine kwa muda wa karibia 2 hours sasa tuko kwenye foleni kupisha Mwenge.

In this Millennium tunapotezeana muda kiasi hichi kisa Mwenge!

Disappointment ya hali ya juu.

Wakazi wa Kigamboni tunaotumia daraja kwenda mjini, Muda huu usijaribu.

Bora ukapange foleni kwenye kivuko.

Its worse
Leo unakuja bunju yani hii nchi haki Afrika **** shida. Barabra ya mabwepande mbovu kwa miaka mingi. Ila kisa leo mwenge unapita wamepitisha grader wakamwaga na kokoto hapo ili mwenge upite vzuri na baada ya siku kadhaa itarudi kuwa vile vile. Mimi leo nilikuwa nna safari ya kwenda down town ila siendi maana najua nitakuwa stcuk kwenye folen kuanzia bunju hadi mwenge huko.
Mimi sielewi haya masuala ya kutengeneza barabara kiongozi akiwa anapita. Kuna siku rais nadhani ilikuwa feb alienda mtembelea mzee Makamba. Ile barabara ya kuelekea mtaani kwake mbovu sana miaka na miaka. Ila siki 2 kabla likapitishwa gereda ikachongwa na kumwaga kifusi. Mabanda ya wauza mboga mboga yakaondolewa. Boda bida wakaambiwa waondoke pale kituoni wakae mbali. Lakini hawakusema kuwa atapita rais. Ila mimi nikabaki najiuliza baada ya kupita rais wanajaribu kumficha umasikini walionao anaowatawala hadi wanabomoa mabanda yao au maana sielewi. Barabara yenyewe baada ya mwez ikarudi katika hali yake na kwa makamba hata hakukaa zaidi ya dakika 30
 
Mwenge wa uhuru ni kielelezo cha uhuru wa Tanzania, ni taa yenye kumulika nchi na miradi yake.

Ni nyota inayotukumbusha kwamba uhuru ni jambo muhimu na la kipekee kwa binadamu aliye kamili.

Hivyo basi hata hapo kwenye foleni yakupasa uwe na fikra chanya ya kutafakuri uzuri na ubora wa Mwenge na siyo kwamba unapoteza muda.

Ni muhimu kila Mtanzania akaguswa na Mbio za Mwenge, ukiwemo wewe uliyeguswa ukiwa kwenye foleni.

Usijinunishe bali furahi na tafakari huu utamaduni wetu adhimu wa kuukimbiza Mwenge wa Uhuru.

Sema Mwenge oyeeeeee
Ukizeeka utakuwa mchawi wewe.
 
Mwenge ukipita kwa mafisadi unazima
 
Back
Top Bottom