bhachu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 8,415
- 9,796
Umeandika nini sasa?Mji wa New York uko masaa 3 mbele ya mji wa California lakini haimaanishi kuwa California ni mji ambao uko slow...wala New York sio kwamba uko fast ... miji yote inaishi kwa kutegemea TIME ZONE...
Kuna mtu mpaka sasa yuko single...na mwingine alioa mapema tuu na kusubiri miaka 10 kupata mtoto...na yupo mwingine ambaye alipata mtoto ndani ya mwaka mmoja tuu baada ya kuoa.
Kuna ambaye aligraduate akiwa na miaka 22 na akasubiri miaka 5 kupata kazi nzuri...na kuna ambaye aligraduate akiwa na miaka 27 na akapata kazi mara moja!!
Kuna ambaye alikuwa mkurugenzi wa kampuni akiwa na miaka 25 tuu na akafariki akiwa na miaka 50 wakati huohuo yupo aliyeweza kuwa mkurugenzi akiwa na miaka 50 na akaishi hadi miaka 90...
So mwisho wa siku unagundua kuwa kila mmoja wetu ana TIME ZONE yake... Ndugu zako au rafiki zako wanaweza kuwa mbele yako au wanaweza kuwa nyuma yako lakini kamwe USIWAONEE WIVU WAWAPO MBELE YAKO na pia USIWAKEBEHI UWAPO MBELE YAO maana kila mtu yupo kwe TIME ZONE yake..
Hold on, be strong, and stay true to yourself...maana all things shall work together for your good...Hujachelewa na wala Hujawahi...upo ON TIME... STAY BLESSED.