secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 610
- 984
๐๐๐๐๐, Unajua nacheka Kwa nini, hii ni maajabu!
Huko UDOM wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu wameanzisha malalamiko ya chini chini kupinga utaratibu unaotumiwa na uongozi wa chou wa kuwahamisha sehemu (blocks/mabweno) walikokuwa wanajihifadhi.
Wanafunzi wanadai kuwa wanapangiwa sehemu (blocks and rooms) zingine bila kushirikishwa ilihali hawakai bure bali wanatoa pesa zao.
Hasira za wanafunzi zinakuja baada ya kuhamishwa kutoka kwenye blocks ambazo zinatoa maji na kupelekwa kule kusiko na maji, kutengwa na marafiki zao (ambao walikuwa wanakaa sehemu/room Moja) huku wakiamini kuwa mali zao hazitakuwa salama tena .
Kwa kudhani kuwa watakaokuja kupangwa nao wanaweza kuwa na tabia zisizofaa mfano wizi, wapendao kufanya ngono kwenye dabo deka na tabia zinginezo zisizofurahisha mtima. Wengime wameenda mbali Kwa kudai kuwa baadhi yao wanachangia (wamenunua pamoja) vifaa kama vile heater, ndoo, majaba na hata nguo za kuvaa๐ hivyo kutenganishwa kwao kutaleta sintofahamu juu ya nani achukue hivyo vifaa na nani aache huku ikizangatiwa kuwa hivyo vifaa havigawanyiki kirahisi.
Cha kushangaza zaidi ni kwamba wasomi wa chuo chenye hadhi kubwa (UDOM) wanashindwa kupaza sauti zao Kwa uongozi wa chuo nakulipinga hili suala Kwa hoja kuntu na badala yake wanaanza kuongea chini chini kama watoto wa mama wa kambo huku wakisubiri miujiza.
Kama wasomi wanashindwa kupambana na suala hili Kwa kulihoji japo kidogo Mimi naona itakuwa ngumu Kwa raia wa kawaida kupaza sauti ili kupinga madudu yanayofanyika katika nchi kuliko Dunia kupita kwenye tundu la sindano.
Share out kwa Generation Z kutoka Kenya.