Huenda shirika la kazi duniani na shirika la haki za binadamu wakajitosa sakata watumishi 9932

Kwani wakati wanaajiliwa, hao waajili kwanini hawakuhakiki vyeti, usikute wakati wanaajili mkataba wao na mwajili wa wakati huo alihitaji vyeti feki.. Magufuli analeta taratibu ambazo mwajili wa awali hazitambui.
Hakuna muajiri anayetaka vyeti feki waliajiriwa enzi za mazowea hizi sio enzi hizo.
 
Je wakati wanaomba kazi waliwakilisha vyeti? Je kwanini hawakuhakiki wakati huo
Uhakiki huu ni maalum ambao haukufanywa na waajiri. Uhakiki huu vyeti vinapelekwa necta vinalinganishwa na results slip na kama kuna jina lingine kama Hilo. Waajiri wa kawaida kwa mfano halmashauri anaangalia cheti kwa juu tu akiona kinafanana na cha baraza basi wakati hata feki vinafanana na vya baraza tena ni vile vile vya baraza vinaibiwa blank vinajazwa kulingana na matakwa ya mteja.
 
Hakuna muajiri anayetaka vyeti feki waliajiriwa enzi za mazowea hizi sio enzi hizo.
Kwani Bashite kaajiriwa enzi ipi...? Hujui mwajiri aliyemuajiri Bashite kahitaji vyeti feki vya Bashite!? Usishangae basi kuona hao wengine waliajiriwa na mwajiri sawa sawa na yule aliyemwajiri Bashite
 
Tuende mbele turudi nyuma! Katika taratibu zote za Ajira Kama umemuajiri mtu na unataka kumfuta kazi ni muhimu kuwa na amicable dismissal huo ndio ubinadamu WA kawaida hivyo naiomba serekali iwafikirie Hawa ndugu zetu
Hawafutwi kazi wanatakiwa wajiondoe wenyewe in two weeks wakibisha wanapelekwa mahakamani. Serikali inakwepa kuwalipa ikiwaachisha. Kuhusu kuwaombea msamaha inategemea kukubaliwa au la.
 
Na kama walifoji vyeti, ww uliwaajiri kwa vyeti gani?
Waliajiriwa bila kujulikana sasa wamejulikana na ukaguzi maalum. Uhakiki huu ni tofauti na ule wa kawaida unaofanywa na HR anapoajiri. Pamoja ya kwamba walikuwa wanapewa rushwa lkn pia walikuwa wanakiangalia cheti kwa macho tu wakiona kinafanana na cha necta wanaajiri lkn uhakiki huu kila cheti kilipelekwa necta na kufananisha na details za mtahiniwa kule kwenye mafile yao ndio maana waligundua na zoezi kuchukua muda mrefu. Hata zoezi la umri litafanywa hivyo hivyo wengi wamepeleka vyeti vya uongo kwenye umri lkn katika uhakiki vitalinganishwa na mwaka ulionza darasa la kwanza mpk la saba sec n.k pia vyeti vya darasa la saba vinaandikwa tar ya kuzaliwa wataumbuka wengi.
 
Sidhani kama hawa ndugu zetu wana haki yeyote ya kuidai serikali. Labda tu serikali iamue kuwahurumia. Walijipatia hizo nafasi kinyume na sheria, they have to go, hawana wanachodai. Walipaswa warudishe mpaka hiyo mishahara yote waliyolipwa sikuzote wanafanya kazi. Hizo kazi hazikuwa za kwao. Walichukua nafasi za watu wengine wenye vyeti halali ambao hawakuzipata hizo kazi kwasababu zilikuwa zimeshaibiwa.
 
Utaratibu haukufuatwa wa kusitisha ajira zao....
Wakikomaa serikali utapata hasara kubwa sanaa
Utaratibu umefuatwa vizuri serikali iko makini wamefikiria vyote hivyo ndio maana wameambiwa waache wenyewe in two weeks atakayekataa atapelekwa mahakamani hii maana yake serikali haikuachishi kazi Bali unaacha mwenyewe ukibisha na kupelekwa mahakamani ikithibitika kweli umefoji unafungwa serikali inakutoa kwa kipengele kingine cha kazi kinachokataza mfanyakazi kuendelea na kazi unapokutwa na hatua ya kesi ya jinai.
 
Mimi ningekuwa mmojawapo kati ya hawa watakatishaji vyeti tena ningeishukuru serikali kwa kuniachisha kazi bila kunishtaki. Serikali imewasaidia kuwaacha waondoke na wabaki na hizo fedha ambazo tayari walikuwa wameshalipwa. Wasitafute makubwa, waondoke tu.
 
NYIE WACHOONGENI TU WENZENU, HAMJUI KUWA KUGHUSHI VYETI NI KOSA LA JINAI?KUJIPATIA KAZI KWA UDANGANYIFU NI KOSA LINALOSTAHIKI ADHABU YA MIAKA 7 JELA NA KULIPA FEDHA ZOTE WALIZOKWAPUA WAKIWA KAZINI HUKU WAKIJUAFIKA KUWA WAO NI VIMEO!
 
Tukiamua kuacha ujinga tunaweza. Hamna anayefurahia majanga yaliyowakuta hao watu. Hata hivyo kuamini kuwa kuna organization ya kimataifa inaweza kuja hapa kuamua mambo ni ujinga wa kiwango cha lami.
Kuna wajinga wenzetu wengine waliamini ICJ watakuja kuzuia JPM asiapishwe Nov 5, 2015. The Zunguz didn't show up.
Again, kuacha ujinga maamuzi tu.
 
Kwani Bashite kaajiriwa enzi ipi...? Hujui mwajiri aliyemuajiri Bashite kahitaji vyeti feki vya Bashite!? Usishangae basi kuona hao wengine waliajiriwa na mwajiri sawa sawa na yule aliyemwajiri Bashite
Tofautisha kati ya kuajiriwa na kuteuliwa. Hamna mkuu wa Mkoa anayeajiriwa mkuu.
 
Mkuu fikiria nje ya box kwanza. Hivi serikali ndo iliwaambia wagushi vyeti? Na huoni kwamba walikuwa wanawanyima haki yao watu wenye haki ya kushika nafasi hizo?

Pia kumbuka kosa walilo lifanya walitakiwa kuchukuliwa hatua Kali za kisheria lakini rais kafanya hekima tu. Na mbona wenyewe hawaongei kitu ila wasiohusika ndo mnajaa povu?
 
Utaratibu haukufuatwa wa kusitisha ajira zao....
Wakikomaa serikali utapata hasara kubwa sanaa
Utaratibu gani ulitaka wakafunguliwe kesi waongezewe matatizo ya gharama za kesi na kufungwa ?
 
Reactions: SDG
Je wakati wanaomba kazi waliwakilisha vyeti? Je kwanini hawakuhakiki wakati huo
Collusion kuna watu wengine wataondoka nao hasa maofisa uajiri. Hao kudakwa ni part One part two ni ya waliowaajiri
 
Reactions: SDG
Mimi nashauli wasitoe makucha tu.
Wavue na nguo kabisa wabaki uchi mtupu.

Mtu aliyekaa ktk nafasi ambayo hastaili na hana vigezo kielimu ya nafasi hiyo juwa ya kwamba utendaji wake ktk kutoa huduma ktk jamii unaambatana na rushwa,ufisadi,10%ndio kigezo kikuu kwao.
Na ndio maana taasisi nyingi hufa . hakuna michango ya mawazo endelevu sababu hauna elimu husika.
Mfano wewe mpiga debe ,ukapewa uchef unadhani utatulisha chakula gani? Hapo ni ugali maharage tu siku ukipika wali utaona umefanya la maana ,sababu ndio uwezo wako kutokana la kiwango cha upiga debe wako.
 
Reactions: SDG
Katika watumishi hao 9930±, je hakuna watu ambao yamefanyika makosa?Je kama makosa yamefanyika, itaandikwa list mpya kuwasafisha?
 
Reactions: SDG
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…