Huenda ni kweli mwandishi alikosea, lakini hii ndio 'polite language' ya kumjibu mtu mzima?

Yani mnawafata watu mpaka makanisani tena Ijumaa Kuu awa waandishi wa magazeti ya Chadema wanatafuta choko choko ili wapate matukio ya kuuza magazeti yao.
Akili za kindumilakuwili, na hazikutoshi kabisa hata kwa matumizi yako mwenyewe
 
Hili jibu ni wazi boss huyu wa TAKUKURU amejenga mtazamo hasi ama na mwandishi au gazeti husika.

Hivi angekuwa ni mwandishi wa HabariLeo au wa gazeti la Uhuru haya ndio yangekuwa majibu?
Thubuutuuuu, hataki kibarua chake?angenywea kama kidonge cha piliton
 
Mhariri wa hili Gazeti hili ni adui wakubwa wa Serikali kuwapa Ushirikiano ni kuinajisi Serikali ya Rais Magufuli
 
waandishi wengi wa habari wa vyombo binafsi hawajasomea taaluma yao, na baahadhi wamesomea kozi hizo kwenye vyuo vya wahuuni wa Dar, hivyo hawana maadili ya kazi zao, kila Sikh wanalalamika tu
 
Ndiyo maana Mkapa aliwaponda waandishi wa Tanzania na kuwasifu kina Riz Khan.
 
Tatizo la waandishi wengi wa nchini hspa ni kuwa wengi ni ma F4F na hawijishughulishi kufanya utafiti kabla ya kusaka habari.
Sasa kwa mtu aliye kanisani au msikitini , utafiti mdogo tu wajinsi ya kutafuta habari hugeuza zoezi zima kuwa ni la kuudhi.
Ameteuliwa kwenda kuswali au kutoa huduma kwa watanzania?hivi analipwa mshahara kwa kwenda kanisani au msikitini?ebu wacha kutufanya watanzania kama mandunya
 
Hawa viongozi wanadhani mwandishi wa habari anatakiwa pale tu wanapotaka sifa. Huyo boss wa PCCB aangalie sana waadishi wapo wakati wote na mahali popote.
 
Huyo mwandishi hana akili kabisa. Badala ya kumtafuta siku za kazi tena aende ofisini kwake apate habari ana kwa ana yeye anampigia simu siku ya mapumziko tena ya ibada.

Hivi hii nchi ni lini watu wake watapata akili?
Kwani siku za kazi hapa tanzania ni ngapi?mbona unajiondoa akili wewe?
 
MWANDISHI NI MPUMBAVU... SIKU SI YA KAZI. NI SIKU YA IBADA KWA MHUSIKA. kma mhusika ni muislamu huwez mpigia simu saa sita hadi saba kumuuliza any news huu ni ujinga. au weekend unamuuliza hbr za kazi? mwandish tumia akili ndogo tu.
 
Kama mwansishi anajua ni zoezi linaloendelea angetumia common sense tu kwamba siku ya kazi atauliza maswali yake. Alitengeneza emergency isiyokuwepo.
Mkuu ijumaa siyo siku ya kazi?au kuna waraka wa utumishi mpya umetolewa?
 
Mlowola naye ni binadamu kama binadamu wengine, ana udhaifu wake katika tabia. Mimi nadhani kilichomkasirisha ni mwandishi kutopredict ijumaa kuu angekuwa wapi kwa muda huo. Yeye akachukulia kwamba mwandishi lazima angekuwa aware na siku yenyewe.
Ila si jibu jema kwa mtu hata kama umegundua udhaifu wake.

"Education is what remains after one has forgotten everything he/she learnt in school" by Albert Enstein. Wengi hatutumii elimu tuliyopata darasani.
 
Ameteuliwa kwenda kuswali au kutoa huduma kwa watanzania?hivi analipwa mshahara kwa kwenda kanisani au msikitini?ebu wacha kutufanya watanzania kama mandunya
Hapo mkuu umechemka, kuteuliwa au kuajiriwa sehemu hakumnyimi mtu Uhuru wa kuabudu, tena hasa iwe ni siku ya mapumziko, tusitetee kabisa kama kweli alitaka kumuhoji kwa nini asiombe muda wa kuonana naye? Huyu mwandishi alikurupuka na hajui majukumu yake sio Ati kwa vile ni mwandishi basi anyenyekewe hata kama amekosea, tena kamkuta jamaa muungwana sana
 
kwani vitendo vya rushwa vina sikukuu?
Sawa, angeweza kwamwambia wakati huo yuko katika ibada na kumpa miadi ya baadaye ambayo ni muafaka kwake. Majibu kama haya yanathibitisha kuwa semina elekezi kuhusu utawala bora bado inahitajika kwa wateule hawa.
Semina elekezi kwa ajili ya waandishi wapumbavu kama Hawa ni kupoteza fedha ya umma.Waandishi wa habari wajiongeze. Hii ni awamu ya 5
 
Back
Top Bottom