A
Anonymous
Guest
MALENGO ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs), hususan lengo la tatu ni kuhakikisha uwapo wa Afya Bora na Ustawi. Umoja wa Mataifa (UN), unahimiza uwekezaji kwenye huduma za afya.
Ajenda ya Shirika la Afya Duniani (WHO), mwaka 2018 katika maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani, yalilenga kuhamasisha huduma ya Afya kwa Wote (UHC), bila vikwazo vyovyote vya kiuchumi.
Ripoti ya mwaka 2022 ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNDP), asilimia 83 ya watu wenye umaskini uliojikita katika maeneo mbalimbali wako nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Theluthi mbili ya watu maskini wako katika nchi za kipato cha kati na asilimia 83 wako vijijini.
MTIHANI WA HUDUMA KWA MTOTO
Ajenda ya dunia ni kuwa na Mfuko wa pamoja wa UHC, kwamba ifikapo 2030 nchi husika iwe imefikia mpango huo kwa kiwango kikubwa. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ndiye mratibu wa azma hiyo nchini.
Ili kufikia malengo hayo, kulitokea mabadiliko ya vifurushi kwa aina ya huduma za matibabu kwa wanachama tangu Machi mwaka huu, jambo ambalo limeleta taswira na vikwazo.
Sera ya Afya ya Mwaka 2007 inabainisha kwamba, huduma za afya kwa wazee, wajawazito pamoja na watoto wenye umri chini ya miaka mitano, huduma za matibabu ni bure.
Wanachama walioondolewa kwenye huduma hiyo kutokana na masharti mapya ni watoto, yaani walio chini ya miaka 18 kundi maalumu ambalo linatambuliwa na Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.
Kwa sasa usajili wa watoto wanaohitaji huduma hiyo tangu Machi mwaka huu, ni kwamba, wanatakiwa wafikie orodha ya watoto 100 shuleni, ndipo wajiunge na Toto Afya, jambo ambalo walezi, walimu na wazazi wameshindwa kulitekeleza.
Takwimu zinaonesha kuna watoto wengi wanaozaliwa nje ya mfumo rasmi, kama wanafunzi 9,011 wa shule za msingi na sekondari walipata ujauzito katika kipindi cha kati mwaka 2021 hadi 2022 nchini. Wengi wa wanafunzi ambao wengi wao wako chini ya miaka 18, wakishajifungua huishia kwenye kundi la mama walea pekee (single mothers) na tegemezi kwa familia.
KUANZA MFUMO MPYA
Ikiwa imepita miezi mitano, tangu kusitishwa kwa huduma ya Toto Afya kwa mtoto mmoja mmoja. Sharti lililopo kutoka NHIF mzazi au mlezi ambaye awali alimlipia mtoto wake kila mwaka Sh. 50,400 ‘Toto Afya Kadi’ kwa ajili ya matibabu ya mwanaye kwa mwaka, sasa hawezi kufanya hivyo aidha amsajili mwanaye kupitia vifurushi tofauti kwenye kundi la Najali Afya’, ‘Wekeza Afya’ au ‘Timiza Afya’,
Mfano kifurushi cha mtu mmoja ambacho hakimhusishi mtoto au tegemezi ni kuanzia Sh. 192,000 hadi Sh. 984,000 kwa mwaka kulingana na umri wa mhusika.
Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), anasema mfuko huo unakusanya fedha ila matumizi yao hayana msingi huku wakikopeshana Sh. bilioni 41.
Waziri Ummy Mwalimu, anasema, mfuko huo, unaelemewa kutokana na kulipia gharama kubwa kwa ajill ya Magomjwa Yasiyoambukiza (NCDs), kama kisukari, kiharusi na shinikizo la juu la damu.
Anasema magonjwa hayo yameugharimu mfuko takribani Sh. billioni 99.09 kwa kipindi cha mwaka 2021/2022. NHIF, unahudumia wanachama milioni 4.33 sawa na asilimia nane ya Watanzania wote wapatao milioni 60, asiimia sita wakihudumiwa na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Waziri amesema kukwama muswada bima afya kwa wote, ni kukosekana kwa chanzo cha uhakika cha fedha.
KUMINYWA HAKI YA MTOTO
Machi 13, mwaka huu, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ulitangaza kwamba utaratibu wa malipo ya Sh. 50,400 ya huduma ya ‘Toto Afya Kadi’, umeondolewa kuanzia Machi 13, mwaka huu, kwa ambao bima zao zimekwisha na wanaohitaji kujiunga wajiunge na mfumo mpya.
Watoto walio chini ya umri huo, hususan wanaougua NCDs na magonjwa sugu; ikiwamo moyo, himofilia, kifafa na mengineyo hulazimika kulipia Sh. 30,000 hadi 130,000 kwa kila kliniki kwa mwezi, kutegemeana na hospitali.
“Mbali na gharama za dawa alipoumwa mwaka huu, alilazwa kwa siku tatu katika hospitali maarufu (jina tunalo) iliyopo Gongo la Mboto, nililipa Sh. 286,000 kwa siku hizo, bado dawa,” anasema Belina Brown mzazi wa Frank Martin mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
Leila Marius mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam: "Mwanangu aligundulika kuwa ana matatizo kwenye ubongo baada ya kuugua ugonjwa wa kifafa na kuhitajika kuhudhuria kliniki Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kila mwezi. Sasa bima yake imekwisha Machi mwaka huu, hivyo ninalipia huduma hiyo kwa fedha taslimu.
“Kila mwezi natakiwa niwe na Sh. 150,000 au 200,000 kwa sababu kuna wakati mwingine dawa alizoandikiwa hazipo Muhimbili, nanunua kwenye maduka ya nje bei ni juu zaidi. Ninafanya kazi yenye mshahara wa Sh. 250,00 kwa mwezi,” anasema Leila.
Janela Muagi, mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam, anasema mtoto wake anaugua ugonjwa wa moyo na kila mwezi anahudhuria kliniki ya watoto wenye ugonjwa huo, hospitali ya Dar Group ambayo ni tawi la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na kila mwezi ni Sh. 130,000.
Regina Valence, Mwenyekiti wa Wanawake wa Chama cha Himofilia Tanzania, na mzazi wa watoto wawili wanaougua ugonjwa wa himofilia, alisema umoja huo wenye wanachama wanaokadiriwa kufikia 200, watoto walio wengi hawana huduma ya bima afya. "Watoto wetu wao wana kliniki muda wowote akivuja tu damu."
Mkurugezni Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC), Anna Henga, anasema ni kinyume na Sheria ya Mtoto pamoja na marekebisho yake mwaka 2019, Ibara ya 24 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto ya Mwaka 1989 na Ibara ya 14 ya Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto.
NINI KIFANYIKE
Kamati za Usimamizi wa Vituo vya Afya na Bodi ya Afya kwenye Wilaya ambazo husimamia vituo vya afya, zahanati, hospitali za Wilaya na zilizopo ngazi ya mkoa au taifa, ziruhusiwe kisimamia huduma hiyo, iwapo kwenye eneo husika mzazi tayari ana kiasi hicho cha fedha, alipie huduma pale walipo.
Vilevile walimu wa shule wana maoni kwamba, utaratibu huo kwao kwanza ni jambo geni na mzigo kwao kwa kuwa hawajawahi kupewa elimu namna ya kuhamasiaha jamii ijiunge.
Pia serikali ichangie gharama.ya huduma za watoto iwapo mzazi analipia Sh. 50,400 kwa mwaka pia serikali ichangie kiasi kama hicho na jumla iwe Sh. 100,800.