Patience123
JF-Expert Member
- Mar 10, 2013
- 5,092
- 8,779
Ni kila mmoja kujitambua na kutambua wajibu wake na nafasi yake kwa mwenzie,Changamoto no lazima ziwepo kwa sababu kila mmoja ana makuzi yake,hobby zake na vipaumbele vyake,kinachotakiwa ni kuviunganisha ili muende pamoja,unapoamua kuishi na mwenzako kuna baadhi ya vitu unatakiwa ubadilike kutokana na kuwa mwenzako kuna vitu ambavyo anavipenda na vingine havipendi. Ikitokea kutokuelewana jambo,focus kusuluhisha kuliko kuachana,Kuwa makini kuchagua marafiki wenu maana si kila mtu anapenda kuona watu wanapendana,"Ninakupenda" na "samahani" huleta haiba kwenye mahusiano na kufuta vifundo kwenye nyoyo za wapendanao. Usichukulie mapungufu ya mwenzi wako kama silaha ya kumuadhibu,bali mpende kutokana na hayo na utafute namna nzuri ya kuyakabili,kama ana kengeza...assume kwamba anarembua...uvumilivu na kuaminiana iwe ni ngao na kila mmoja ajifunze kumfikiria mwenzie vizuri.