Hostel za udsm vs Ghorofa za Magomeni

Mkuu hii umetoa wapi?....
acheni kusikiliza porojo za watawala gharama waliyopeleka Tba kwenye mradi wa Hostel ilikuwa ni Siasa mradi ule umewakula Pesa nyingi kuliko inayozungumzwa amini ninachokwambia
Mkuu nimesema nimechangia uzi huu "in lay man perspective", kama ni chuoni ingekuwa ni assignment kwa kuweka mawazo yangu ya kile ninachodhani
 
Ni rahisi sana kujua kwa nini Gorofa za magomeni zimegharimu kiasi kikubwa kuliko za UDSM...

Ghorofa za UDSM ni kwa ajili ya matumizi ya hostel... Kwa hiyo zimejengwa kwa mfumo wa vyumba na siyo nyumba za kusema kuna master, sebuleni na vyumba vitatu vya kulala...


Ghorofa za Magomeni zimejengwa katika mfumo wa nyumba na siyo vyumba... Kwa lugha nyingine siyo rooms bali ni apartments...

Gharama lazima zitofautiane hata kama ni chache...


Cc: mahondaw
 
Magomeni CO Hostel ni makazi ya watu mkubwa uwe unawaza kabla ujenzi wake unagharama tofauti kwa nyumba moja (floor) ukilinganisha na ujenzi WA hosteli
 
Design ya nyumba za kuishi familia si sawa na design ya vyumba vya kuishi watoto wa chuo, nadhani nimeeleweka.
 
Kwanza kabisa nitangulie kusema uzi huu si wa kupingana wala kui-challenge serikali yangu bali kuibua mjadala ambao utatusaidia kusimamia vema rasilimali za taifa. Sasa naomba kuanzia hapa;

Hostel za UDSM
Naambiwa yapo majengo 20 kila jengo lina ghorofa 4 na gharama yake ni 10bn

Ukichukua majengo 20 X kwa ghorofa 4 utapata ghorofa 80 (floors) ambazo zimetumia 10bn.

Maghorofa ya Magomeni;
Naambiwa yapo majengo 5 kila jengo lina ghorofa 8 hadi 9 na gharama yake ni 20bn. Tufanye wastani wa ghorofa 9 kwa zote.

Ukichukua majengo 5 X kwa ghorofa 9 utapata ghorofa 45 (floors) ambazo zimetumia 20bn

Sasa pale Magomeni kuna shida. Yafaa kuunda tume kuokoa pesa ya taifa maana Jografia ya Dar ni ile ile iweje wametumia pesa nyingi vile?

Naomba changia kwa weledi, usimtukane mtu, usimtukane Kiongozi yeyote maana ni kosa kisheria. Weka point tujifunze usiweke tusi!
Hata ya udsm hayahojiki uliwahi ona wapi mchawi anajiroga? Yaani mjenzi wa Yale majengo ndie anayepaswa kuwa mkaguzi sasa nani kamkagua
 
Janga hapa ni kuamini super structure tu ya ghorofa 45 inagharimu bilioni 20!

Alieturoga kafa.

Tunapigwa siasa, hayo majengo yatatumia si chini ya 50B
 
Back
Top Bottom