KERO Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila) Madaktari wanafunzi ni Janga. Watu wanakufa kwa uzembe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna uzembe mkubwa sana kwenye usimamizi wa hawa ma intern huko mahospitalini
Mwaka juzi nilikuwa na mgonjwa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa; Yaani 90% ya matibabu yote anayetegemewa ni Intern

KOSA KUBWA KULIKO YOTE NILILO LIONA NI KUWA, hapakuwa na consistence ya hao ma Intern yaani kila siku mbili anabadilishwa; yaani Kila siku mbili una intern tofauti, fikiria wagonjwa waliopo Hospitali ya Rufaa ni wale waliopo Serious hivyo wanataka mtu wa kufuatilia alichofanya jana kinaendeleaje; pale eti kila siku mbili wana rotate? UTARATIBU WA HOVYO KABISA!

Ukweli niliumia sana kwani ningetaraji hata kama ni Intern akae hata wiki (ajenge uhusiano na mgonjwa) ndio ahamishwe ward nyingine ILI pia ajifunze. Yaani wale Intern wana try and error nyingi sana kama wanatibu Ngombe ila siwalaumu kwa kuwa, wana achiwa kila kitu/hawasaidiwi

Huyo basi anayeitwa Msimamizi alikuwa anapita saa nne asubuhi kwa kama dakika 5; na jioni tena kwa kama Dakika 5.
Mimi sio dactari ILA kwa mtu yeyote aliye elimika, anaweza kuona kabisa kuwa kinachofanyika sio sawa!
Na hao ma intern wanatoka hapo hawajajifunza chochote!
 
Upo sahihi kabsa nmewahi kumuuguza faza mdogo pale kwa mwez ....kuna sku wodi moja walikufa karibu wagonjwa wote...dokta kufika asubuh alihamaki balaa....kilichosaidia upande wetu alikuwa ni mtu mzto...
 
Nilipoteza mtoto aliyekua anazaliwa mwaka jana hospital ya ifisi mkoa wa mbeya kwa uzembe wa madaktari wanafunzi. Hili la madaktari kujifunzia kwenye miili ya watu wetu, inakera sana
Si ushitaki, haumfahamu mambulukuku huko mbeya? Mwanasheia anaevizia kesi namna hizo?
 
Nini maana ya neno "mloganzila?". Neno "mloga" ni kinyambulishi cha neno "kuloga" kuwangiwa. Kwahiyo ni hospital ambayo hakuna matumaini!
Mkuu malizia tu na maana ya "Nzila" ni njia kwahyo ni mlogaji anayelogea njian yaani eneo la ulozi kama ulozi mwingine wa njia za panda😭
 
Kwakweli tunaomba wizara ya afya iangalie utaratibu huu tutapoteza wagonjwa wengi kwa magonjwa yanayotibika.
 
Nilikutana nao Muhimbili hao madaktari wanafunzi ni changamoto! Matibabu yaliyohitaji ganzi walinitibu bila ganzi, yale maumivu sitayasahau 😭😭😭
 
baada ya kupitia tena vipimo alibadilika ghafla na kuwa mkali sana na kumfokea yule daktari mwanafunzi kuwa kwanini hajaona tatizo la nyonga kuvunjika?

Haiwezi kamwe kutokea. Kama kosa watajuana wenyewe. We kitu gani hadi afokee mwenzie? Labda kwenye vikao vyao wanaweza,na si mbele ya mgonjwa na muuguzi. Tamathilia ingekuwa nzuri usingepitiliza kituo.
 
Huyo mwanafunzi ndio mzembe kama yeye hajaona tatizo na mgonjwa bado ana maumivu Kwa Nini asiombe ushauri Kwa mwalimu wake
 
Ulikutana nao kwenye hizo sites?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…