Hospitali binafsi ya Ks iliyoko mkoani Mbeya inawadhulumu watumishi wake. Tunaomba imulikwe

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
Wizara ya afya na ustawi wa jamii na/au kamati ya afya mkoa/wilaya ya Mbeya imulikeni hospitali ya Ks iliyoko maeneo ya Mafiati.

Hospitali hii licha ya kutulipa watumishi wake mishahara duni ya hadi Laki moja(100,000/=) kwa mwezi huwa haiwasilishi michango yetu ya kila mwezi kwenye mifuko ya Kijamii(NSSF, PSPF, LAPF). Tume jaribu kuuliza lakini tunapigwa danadana kila mara. Ikitokea ukaonekana unafuatilia sana unafukuzwa kazi kwa mdomo na wala sio kwa barua kama ambavyo inatakiwa.

Watumishi wa hapa tunahudumia wagonjwa wengi sana wa bima na cash kwenye kila shift tunayoingia lakini pamoja na hayo yote hatuthaminiwi. Unafanya kazi hadi unakuja kuondoka au kufukuzwa let's say baada ya miaka mitano au hata mwili lakini kwa muda wote huo hakuna hela ambayo imekuwa ikipelekwa kwenye mifuko tajwa hapo juu licha ya kukatwa. Tuna wasiwasi kuwa huenda hata kodi ya serikali itakuwa inawasilishwa TRA licha ya kukatwa kila mwezi.

Hivyo basi tunaiomba Wizara ya afya
na/au kamati ya Afya mkoa/wilaya ya Mbeya kuimulika hospitali hii na ikiwezekana kufika kujionea hali halisi.

Naomba kuwasilisha.
 
Hili ni tatizo kubwa sana nchi sio hapo tu,

Wafanyakazi wengi wana nyanyasika sana tena sana,

Hao wanaojiita TUCTA sijui kazi yao ni nini?

Nilikuja gundua sio serikalini sio binafsi kuajiriwa ni ujinga tu,

Mshahara wenyewe hata ukiamua kuuza karanga una-udouble
 
Mkuu umesoma had chuo kikuu na unalipwa laki moja kwa mwez? Mimi nimeishia form two lakin kwa week napata zaid ya laki mbili

Polen sana wasom
Sio kila anayefanya kazi hospitali kamaliza chuo kikuu,

Kuna watu wanaosaidia katika usafi hawa hasa ndo wanaonyanyasika sana
 
Mimi kaniaogopesha sana mkuu laki moja kwa mwez unaitumiaje kwa mfano? Kila siku uweke vocha ya elf inabak elf sabin bado hujahonga kwa mchuchu, bora tu akalime mbona mimi huwa nalima na biashara nafanya
Huo mshara anao sema huwezi kufanya chochote maana kwa haraka haraka matumizi yanazidi mshahara
Hapo tukichukua kodi ya nyumba ,nauli, vocha, chakula haitoshi kabisa
 
Huo mshara anao sema huwezi kufanya chochote maana kwa haraka haraka matumizi yanazidi mshahara
Hapo tukichukua kodi ya nyumba ,nauli, vocha, chakula haitoshi kabisa
Wafanyakazi wengine mfano Madaktari wanalipwa mshahara wao vizuri tu kama ilivyo serikalini. Shida iliyopo ni kwamba makato yote eg NSSF na TRA yanafanyika lakini katu hayajawahi kuwasilisha kwenye mifuko husika.

Wafanyakazi wanaolipwa Laki moja ni wale wa reception, Medical attendants na wengine wa kada za chini.
 
Wafanyakazi wengine mfano Madaktari wanalipwa mshahara wao vizuri tu kama ilivyo serikalini. Shida iliyopo ni kwamba makato yote eg NSSF na TRA yanafanyika lakini katu hayajawahi kuwasilisha kwenye mifuko husika.

Wafanyakazi wanaolipwa Laki moja ni wale wa reception, Medical attendants na wengine wa mada ya chini.
Mkuu mi naona hapo unatakiwa kufika kwa wahusika ambao ni wizara husika na chama cha kutetea wafanya kazi ili kuwasilisha malamiko yenu na unatakiwa uwasilishe kwa barua na ukiwa na baadhi ya vielelezo ambavyo vitakusaidia kama ushaidi wa unacho lalamikia
 
Hao kama Salamaan health center Mwanza matatizo kila kukicha wakati wanahuduma wagonjwa wengi kwa cash na bima
 
Back
Top Bottom