Hoja za African Supremacy waafrika kujisifia ni watu bora zaidi huwa zinanichekesha, ukweli ni kwamba tunashika mkia mambo mengi yena kwa kujitakia

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Jun 28, 2024
249
701
1720121272155.png


Tuna uwezo mkubwa kimiujiza, wajerumani wachache waliwaua babu zetu wengi sana waliochanjwa na kinjikitilengwale dawa ya kuzuia risasi.

tuna tiba asili zenye nguvu - magonjwa, magonjwa kama malaria, kipindu pindu, ebola inamaliza waafrika wengi mno.


Tunapendana, achilia mbali waafrika kuwa katili kwa wanyama yani hata sisi kw sisi hatupendani kwa kiwango kikubwa sana, kiongozi yupo tayari kukopa nje anunue gari ya milioni 300 huku wananchi wanahangaika kupata hata mlo, kuna kurogana sisi kwa sisi, n.k.

kitu pekee nachoweza kubaliana nacho tuna nguvu za miili tu ndio maana hata matajiri weusi wa Marekani ni wanamichezo, nje ya hapo ngumu sana.
 
Lugha ya kiingereza ilikuwa inadharaulika mno mbele ya kilatini.

Iliitwa lugha ya Wajinga, Wahuni na Walevi.

Ila Leo ndio lugha kuu ya nyanja mbali mbali ulimwenguni.

Wameanza na saikolojia mwisho itakuja kwenye real things, be humble
 
Sisi ni dhaifu katika maeneo mengi sina hakika kama tupo tayari kukubali kwamba sisi ni dhaifu kwa kiwango kikubwa.

Siku tutakayo kubali ndio hatua ya kwanza kujitambua.
 
Back
Top Bottom