mwanazuoni mgeni
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 1,944
- 1,715
Umeeleza vizur dadaPole sana ndugu,
Kuwa mwanaume peke yake haitoshi kwa maisha ya sasa eti kisa zamani baba zetu waliheshimiwa na mama zetu. Kama wewe ni mwanaume unayejiamini, recognize and appreciate your woman's competency, badala ya kulalamika na kuonyesha kutojiamini, tambua, kubali, heshimu na mshukuru mwanamke kwa uwezo alionao hivi sasa, ni kwa faida yako, familia yenu na jamii kwa jumla. Dunia ya sasa imebadilika nasi pia tunapaswa tunapaswa tubadilike, tena haraka sana, maisha hayawezi kuendelea kuwa kama maisha ya zamani, ugunduzi mpya umefanyika, maarifa mengi yamepatikana ambayo zamani hayakuwepo. Zama za kale zilimpendelea mwanaume zaidi kuliko mwanamke lakini hali ya sasa ni tofauti. Wanawake wengi wa sasa wameshathitisha hilo. Ukiondoa masuala ya kimaumbile yanamtofautisha mwanamke na mwanaume kama kubeba ujauzito, kuzaa, kunyonyesha, kupata hedhi nk, lakini zaidi ya hapo hakuna sababu mwanaume mzima kulalama leo kwamba apewe haki zaidi eti tu kwa kuwa ni mwanaume. Wanawake wengi leo wamesoma na wama maarifa mengi, tena kwa ushindani wa kitaaluma pamoja na hao wanaojiita wanaume. Wanafanya vizuri sana mashuleni, vyuoni na hata makazini. Hivi leo tuna madaktari, wahasibu, wahandisi, wanasheria, marubani wengi wanawake wenye uwezo mara nyingi tu zaidi ya hao waliozoea kuitwa wanaume.
Kama unataka mwanamke akuheshimu leo, JIONGEZE, onesha uanaume wako kwa uwezo wa kiakili, ubunifu, kutatua matatizo, kufanya kazi kwa bidii, fanya mambo practically ambayo yatakupa credits kutoka kwa mwanamke wako, mfano provide food and shelter for your family, protect your family, love and care for your family , be proud to hassle for your family. Heshima ya kuwa mwanaume inakuja kwa kufanyiwa kazi na haiji tu eti kisa wewe ni mwanaume unayevaa suruali. Respect is earned not granted.
By the way, just imagine what if huyo mwanamke unayemlalamikia hapa angekuwa ni dada yako?! Naamini ungeona fahari kuwa na dada wa aina hiyo, si ndio!!?? Lakini kwa kuwa ni 'mwanamke wako' unamuona tofauti, acha hizo hizo, furahia uwepo wake, uwezo wake na yote wewe na yeye furahieni maisha, maana ni mafupi mno