mwanateknolojia
JF-Expert Member
- Nov 17, 2014
- 1,026
- 1,749
Niende moja kwa moja katika maada yangu.
Nina amini kuwa humu ndani ya JF kuna watendaji wa serikali wakiwemo wa wizara ya Maliasili na utalii na pia wa wizara ya fedha na wa TRA. Ningependa sana na wale wote mlio kirani Mhe. Rais na Makamu wake muwafikishie kilio hiki.
Kiukweli biashara ya mazao ya misitu na hasa mkaa kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ni biashara moja ngumu sana na ugumu wake unatokana na utitiri wa tozo ambazo kiukweli nyigine ndizo nafikiri ndizo mheshimiwa Rais Samia aliziita ni KODI ZA DHULUMA .
Ili uweze kufanya biashara ya mkaa nchini Tanzania unatakiwa kulipia vifuatavyo:-
Pamoja na kulipa gharama hizo zote lakini pia kila unapokwenda kununua mkaa porini ni lazima ulipe tena ghara zifuatazo:-
Ukija sasa kwenye bei ya kila gunia tunauza kati ya 35,000/= mpaka 38,000/= na hivyo unakuta wastani wa faida kwa kila junia ni kati ya 1500 hadi 4500/=, Hali hii inafanya mazingira ya biashara hii kuwa magumu sana kwani hata ukuwaji wa mtaji ni mdogo sana sababu faida inayopatikana ni ndogo mno inayoishia kwenye mlo tu wa kusukuma wiki.
Hivyo natoa wito kwa wizara ya maliasili kuyaangalia upya haya malipo ya kodi ya TFS (TSHS 12,500 ) anayolipa mfanyabiashara kila wakati kwakweli ndiyo yanayonyonya faida kariba yote ya mfanya biashara. Kama mfanya biashara tayari alishalipia vibali vyote akalipia na kodi ya biashara hiyo TRA, Je haya malipo mengine tena ya kulipa kila wakati hivi ni ya kazi gani? Kuna maana gani kulipa kodi kule TRA wakati tena kila wakati unatakiwa ulipie tena kodi na ushuru wa kila gunia? Hayo malipo ya kodi kule TRA na hayo malipo ya kodi ya TFS yote yapo kwenye kundi la malipo ya serikali, je kwanini serikali itoze kodi ya kitu kimoja mara mbili mbili?
Alafu jambo la kushangaza na kusikitisha ni kwamba, TFS wanatoza hizo kodi ilihali mkaa unavunwa kutoka mashamba ya watu binafsi na sio mashamba ya serikali. Mashamba na misitu ya serikali TFS walishayawekea vibao vinavyoyatambulisha na walishapiga marufuku kuvuna mkaa humo je hizi tozo wanazotoza kila wakati ni za kazi gani kama sio DHULUMA?
Tunaiomba serikali izikutanishe wizara zote zinazohusika na suala hili kuangalia namna ya kupunguza huu mzigo mkubwa wa kodi kwa wafanya biashara wa mkaa, na kuondoa mkanganyiko ijulikane kama kulipa TRA au ni kulipa TFS lakini kuendelea kutoza kotekote kunaonyesha wazi kuwa hapa kuna malipo ya KODI ZA DHULUMA.

- Gharama ya kibali cha uvunaji katika wilaya unakonunua au kuchoma mkaa=TSHS 261,000/=
- Gharama ya kibali cha stoo katika wilaya unakokwenda kuuzia mkaa = TSHS 305,000/=
- Gharama ya leseni ya biashara katika halmashauri unapofanyia biashara ya mkaa = TSHS 81,000/=
- Kodi ya mapato TRA, kwa mtaji wa chini kabisa unakadiriwa TSHS 250,000/=
- Jumla ya gharama hizi zote ni TSHS 897,000/=
Pamoja na kulipa gharama hizo zote lakini pia kila unapokwenda kununua mkaa porini ni lazima ulipe tena ghara zifuatazo:-
- TSHS 12,500/= malipo ya kodi ya TFS kwa kila gunia moja.
- TSHS 1,500/= Malipo ya ushuru wa Halmashauri kwa kila gunia moja
- TSHS 15,000/= Malipo ya kibali cha kusafirisha mkaa
- TSHS 18,000/= Malipo ya service levi
- TSHS 500/= ushuru wa kila gunia kwenye kata unapouzia mkaa