FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,061
Habari!
Awali ya yote, natumai mu wazima wa afya.
Nimemsikia Joe Biden akisema kuwa ana wasiwasi kwamba rais Donald Trump "atajaribu kufanya wizi" katika uchaguzi ujao wa rais wa mwezi Novemba mwaka huu.
Joe Biden hakuishia hapo tu bali amedai kuwa anaamini Jeshi litalazimika kumuondoa kwa nguvu Trump kutoka White House endapo akigoma baada ya kushindwa uchaguzi wa Novemba.
Kauli hizi zimepokelewa kwa mitazamo tofauti tofauti kwa wale waliopata kumsikiliza Joe Biden.
Kuna wanaodhani ni mzaha tu ama mbinu za kisiasa za Joe Biden za kumtawala mpinzani wake kuelekea katika uchaguzi ujao huku wengine wakizipuuza kauli hizi lakini kuna ambao kauli hizi zimejenga hofu ndani ya mioyo yao.
Mimi naweza kuziita hofu hizo 'hofu tupu' na kuna masuala mengine mengi ya kuhofia na si hiki cha Trump kugoma kuachia ngazi.
Pamoja na hayo, Trump hakukaa kimya.
Trump akizungumza jana katika mahojiano yake na FOX News alidokeza kuwa ataachia ngazi kwa amani endapo atashindwa uchaguzi ujao wa Novemba.
Katika mahojiano hayo Trump alinukuliwa akisema, “Certainly, if I don't win, I don't win.”
Sasa, ni kipi kinachompelekea Joe Biden kuhisi hiki anachokihisi?
Je, hizi si dalili kuwa Joe Biden ameanza kushindwa mapema kumkabili Donald Trump kwa hoja za kuweza kujenga ushawishi wa kupigiwa kura?
Kauli hizi za Joe Biden kuelekea uchaguzi wa Novemba zinaashiria kitu gani?