Hivi yupi bora kati ya wawili hawa? Magufuli PhD holder lkn kingereza F, Mbowe kingereza A form six.

Ni aibu sana kwa mtu wa phd.
Idd Amin hakuwa na phd ila watu walikuwa hawajari kutokana na elimu yake pia hata wakati huo kiingereza kilikuwa sio kiviiileee!

Kwenye mkutano mmoja alisema.

"you people's of kabare you are very vegitable." watu wakashangaa so huwezi kulinganisha na phd mbichi kabisa ya am a politicians.

Walimu wa chemistry wafundishe kwa kiswahili hili wanafunzi wao wakipata phd ieleweke kuwa ni ya kiswahili!

Hapa ni kazi tu!
 
Nadhani sasa ifike muda tujifunze kuwaheshimu Viongozi wetu hasa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Hizi siasa za maji taka zisiondoe utu wetu wa kuheshimiana tulio nao Watanzania. Hivi fanikio la Kiongozi linatokana na kujua kwake kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha au kuwa tu Mtendaji mzuri anayesaidiwa na jopo la wataalam wa masuala mbalimbali? Hivi unajua kuwa Urais ni TAASISI hivyo dhihaka au kebehi yako kwa Rais wetu haimlengi tu Magufuli bali Watumishi wake wote wanaomzunguka na kumsaidia kazi zake. Marais Francois Hollande wa Ufaransa na Vladmir Putin wa Urusi wanajua hicho Kiingereza chako kukiongea kiufasaha? Je nchi zao zipoje katika maendeleo? Watanzania tuliwaona wengi tu wenye kujua hicho Kiingereza unachokipigania ( na ambacho nina uhakika usio na shaka kuwa hata wewe pia hukijui ) lakini tulimchagua Rais Dr. John Pombe Joseph MAGUFULI aje atufanyie kazi na siyo atuzungumzie Kiingereza pale IKULU kwakuwa walikuwepo waliokuwa wakizungumza Kiingereza lakini wameifikisha nchi hapa ilipo sasa kwa upuuzi wao. Jifunze kuheshimu MAMLAKA!
I second your comments all i can say is that it takes sometimes to emancipate some of us from Colonial mentality.
 
Mpime Magufuli kupitia kiswahili. Mpe mahesabu ya chemia uone kama yatamshinda. Kiingereza ni lugha lugha tu. Ndio maana mtoto wa miaka 3 anaweza kuongea kiingereza, lakini hawezi kusolve maswali ya chemistry.
 
Nimeona kuna mvutano mkubwa sana juu ya umuhimu wa kingereza na kiswahili kwa viongozi wetu wa kitaifa, lkn kuna mada tena ilikuwepo sana kipindi cha nyuma kwamba mtu mwenye elimu ya kidato cha sita hastahili kuongoza chama kilicho na wasomi ndani wa viwango tofauti kuanzia darasa la wengi (sekondari za kata) hadi maprofesa (Baregu - Said Arfi).
Lakini hii mada ilikuwa na ukinzani toka upande wa pili nao wakihoji ni vipi chama kiongozwe na Dr. wa kutunukiwa kama zawadi (kupewa bila kuivujia jasho elimu, ktk mpira ungeweza sema points za mezani pasipo onyesha juhudi ama uwezo wako dhidi ya wengine) na tena kikiwa na Katibu mkuu mwenye elimu darasa la wengi Yusuph Makamba ilihali chama kina wasomi wenye elimu kubwa tena lukiki kuanzia maprofesa hadi hapa na pale(Mark Mwandosya - Lusinde, maji marefu).....?
Maana kwa vijana ni muhimu tukaelewa kipi ni bora, kwani kuna baadhi ya vijana wamekosa kazi kisa kingereza ktk usahili (interview) na wamechukuliwa watu wenye uwezo wa kuzungumza kingereza!
Na sasa wameanza kutokea watu wakiilinganisha Tanzania na nchi hadi zenye uchumi wa juu na kura ya turufu ktk maamuzi ya dunia (Russia na China) kwamba mbn zinatumia lugha zao na zimefanikiwa, pasipo kujua nchi zile na Tanzania kuna utofauti mkubwa sana...! Nawasilisha.
Mjadala wa kingereza cha jpm ni kupoteza muda. Muhimu ni uwezo wa kufikiri wa rais wetu na uwezo wake wa kutenda. Kingereza ni lugha tu kama kimasai kihindi kiswahili au kisonjo. Wapo watu wana shida kuongoea lugha fasaha lakini sio kuelewa. Wapo wahindi, wamasai wasudani huwezi kuelewa wewe mswahili wakiongea kingereza japo maprofesa. Msituchanganye nyie ukawa rais wetu ni jembe. Urembo wa paka sio hoja kama hakamati panya.
 
Nakumbuka Kiingereza alichoongea Mbowe ni "ZITTO IS WHO" akimaanisha "WHO IS ZITTO" wakati akizungumzia kuondoka kwa ZITTO Chadema. Sijawahi kusikia tena akipasua mayai
nikupe link mkuu akiwa ughaibuni
 
S
Nakumbuka Kiingereza alichoongea Mbowe ni "ZITTO IS WHO" akimaanisha "WHO IS ZITTO" wakati akizungumzia kuondoka kwa ZITTO Chadema. Sijawahi kusikia tena akipasua mayai
Sina hakika Kama masikio yako yana matege au ndio uwezo wako kwenye kiingereza Ni wa kiwango cha Ras Simba, ukadandia lori la propaganda bila kujua linaenda wapi!, Mbowe alisema "this is war!", poleee!.
 
Hii nchi bwana kweli bata mzinga wengi, yaani mtu abashangaa rais kuhojiwa kweliii....
 
Hivi rais hahojiwi ati..? Watu (manabii ) walihojiana na Mungu sembuse binadamu, ndio maana msoga boy kawapiga sana kisa nidhamu za kimaskini na unyenyekemu kindovo. Ikiwa mwanaye tena mwenye umri mdogo kuliko wewe unaeshangaa eti rais kuhojiwa anamuhoji iwe mimi niliyepanga foleni kupiga kura nisihoji? Kweli hii nchi nyumbu awataisha!
 
Nimekua nikimfuatilia mh mkulu hasa akiwa anakutana na mabalozi wa nchi mbali mbali simuoni akiongea kiingereza au waandishi wa habari wa Ikulu uwa wanakata sehemu anayokua anaongea? Nakumbuka enzi wa wa awamu ya nne alikua anaachiwa tunamsikia.
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili,hao wanaokuja yawapasa wajifunze kiswahili,ushawah kwenda ujerumani,China au Urusi?? LAZIMA uongee Lugha zao kama huwezi tumia mkalimani,JIVUNIE LUGHA YAKO MKUU
 
Niliwahi msikiliza Mbowe akihojiwa in English. The guy is great upstairs. Not only in English but also his reasoning capacity exceeds Magufuli by far.
 
raisi lazma ajue lugha ya kimataifa english, wetu pengne ipo siku ....
 
Nimeona kuna mvutano mkubwa sana juu ya umuhimu wa kingereza na kiswahili kwa viongozi wetu wa kitaifa, lkn kuna mada tena ilikuwepo sana kipindi cha nyuma kwamba mtu mwenye elimu ya kidato cha sita hastahili kuongoza chama kilicho na wasomi ndani wa viwango tofauti kuanzia darasa la wengi (sekondari za kata) hadi maprofesa (Baregu - Said Arfi).
Lakini hii mada ilikuwa na ukinzani toka upande wa pili nao wakihoji ni vipi chama kiongozwe na Dr. wa kutunukiwa kama zawadi (kupewa bila kuivujia jasho elimu, ktk mpira ungeweza sema points za mezani pasipo onyesha juhudi ama uwezo wako dhidi ya wengine) na tena kikiwa na Katibu mkuu mwenye elimu darasa la wengi Yusuph Makamba ilihali chama kina wasomi wenye elimu kubwa tena lukiki kuanzia maprofesa hadi hapa na pale(Mark Mwandosya - Lusinde, maji marefu).....?
Maana kwa vijana ni muhimu tukaelewa kipi ni bora, kwani kuna baadhi ya vijana wamekosa kazi kisa kingereza ktk usahili (interview) na wamechukuliwa watu wenye uwezo wa kuzungumza kingereza!
Na sasa wameanza kutokea watu wakiilinganisha Tanzania na nchi hadi zenye uchumi wa juu na kura ya turufu ktk maamuzi ya dunia (Russia na China) kwamba mbn zinatumia lugha zao na zimefanikiwa, pasipo kujua nchi zile na Tanzania kuna utofauti mkubwa sana...! Nawasilisha.
Uchochezi
 
Nadhani sasa ifike muda tujifunze kuwaheshimu Viongozi wetu hasa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Hizi siasa za maji taka zisiondoe utu wetu wa kuheshimiana tulio nao Watanzania. Hivi fanikio la Kiongozi linatokana na kujua kwake kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha au kuwa tu Mtendaji mzuri anayesaidiwa na jopo la wataalam wa masuala mbalimbali? Hivi unajua kuwa Urais ni TAASISI hivyo dhihaka au kebehi yako kwa Rais wetu haimlengi tu Magufuli bali Watumishi wake wote wanaomzunguka na kumsaidia kazi zake. Marais Francois Hollande wa Ufaransa na Vladmir Putin wa Urusi wanajua hicho Kiingereza chako kukiongea kiufasaha? Je nchi zao zipoje katika maendeleo? Watanzania tuliwaona wengi tu wenye kujua hicho Kiingereza unachokipigania ( na ambacho nina uhakika usio na shaka kuwa hata wewe pia hukijui ) lakini tulimchagua Rais Dr. John Pombe Joseph MAGUFULI aje atufanyie kazi na siyo atuzungumzie Kiingereza pale IKULU kwakuwa walikuwepo waliokuwa wakizungumza Kiingereza lakini wameifikisha nchi hapa ilipo sasa kwa upuuzi wao. Jifunze kuheshimu MAMLAKA!

For first time na support hoja yako. Premier wa China, Chancellor wa Germany Angela Markel etc. Hawajui Kiingereza ila Nchi zao ziko very Successful na ndio wafadhili wakubwa wa miradi ya Maendeleo Tanzania.

Imagine watu wasiojua Kiingereza wanatupa pesa za kufanya miradi ya Maendeleo nchini.
 
Back
Top Bottom