Hivi wenzetu wanawachapa mikwaju watoto wao kama sisi?

BABA SANIAH

JF-Expert Member
Oct 20, 2013
4,576
5,861
Habari za muda huu Wana jukwaaa. Tuhame kidogo kwenye migegedo tuje huku kwenye malezi.

Sisi watoto wa kiswahili na uswahilini tulivyolelewa tunajua wenyewe (ukitoa wale wa mboga Saba) ukizingua kipondo tu toka kwa wazi.

Mara nyingine kama Sasa hivi msimu wa maenbe tunaangua tu embe mbichi bila ya sababu, mara tuko na mbwa tunawasaka paka, mara tuna manati shingoni tunawinda ndege na mambo mengine mengi mengi ambayo tuliokulia uswahilini tumeyapitia.

Hata mitabia mibaya pia tumeipitia, kucheza kombolela kujificha na huko huko kulana uroda pia tumeipitia.

Sasa najiuliza watoto wa wenzetu, indians, Arabians, Chinese, Europeans wote, hivi watoto wao wanapigwa kama sisi?

Je na watoto wao Wana mitabia mibaya kama ya kwetu? Kama hawana mitabia mibaya na hawapigwi kama sisi je?

Sisi tunafeli wapi kwenye malezi ya watoto wetu? Na wenzetu wanatuzidi sehemu gani kwenye malezi?

Hebu tuzungumze kidogo hapa.
Karibuni🙏
 
Back
Top Bottom