Hivi watu wa hali ya chini wanawezaje kuoa na hizi mali?

Milioni mbili no kiasi kidogo sana.hebu chukua Huyo bint ana elimu ys chuo kikuu. Anafanya kazi mahali na pato lake kwa mwezi ni km 1.8. Atafanyiwa kitchen party zawadi zote zenu. Atafanyiwa send off zawadi zote zenu. Atapewa plot mbweni hio ni yenu.bado mahari mil.2, unaona ni nyingi ? .hujui kua mahari hailipwi yote ?. Km hayo yote unajua bado unalia mahari kubwa basi nenda msata au kiromo mahari ni lk 2, utoa mke na miaka 4 ndoa kalasi.
 
nikijumlisha vurugu zote kuanzia mahari mpaka ndoa kuisha nilitumia karibu milion 6.... nikiwaza hela zangu najiona mjinga sana.. kuna hidden cost hapo kama shela, pete, nauli ya send off, gharama za church, bado harusi ina sehem zina mapungufu bwana harusi itakulazimu ujazie

ila yote alisababisha mama yangu ndie aliekuwa anataka harusi sana
hongera sana Mkuu ila kwahiyo gharama hiyo kama ungewekeza kwenye biashara,kilimo au ufugaji ungepiga hatua kubwa sana ila waafrika vitu vya kutupotezea pesa tunaviendekeza sana kuliko uzalishaji mali sherehe yenyewe ni ya siku moja tu.
 
yote nilikuwa nayajua ila mama yangu ndio shida.. hela ndogo ndogo ya kulima au kuwekeza ninayo ila harusi nilikuwa siitaki na sijawai kuitaka.. ila mama aliutumia umama kulazimisha nifanye harusi..

ila najiona mjinga sana asingekuwepo mama yangu nisingeifanya kwa kweli...harusi ni ujinga

Kwani milion mbili ni hela nyingi sana?unahonga sh ngapi kwa mwezi?unazungusha raundi za bia na washkaji sh ngapi kwa mwezi?unabeti na kuliwa sh ngapi kwa mwezi?
 
yote nilikuwa nayajua ila mama yangu ndio shida.. hela ndogo ndogo ya kulima au kuwekeza ninayo ila harusi nilikuwa siitaki na sijawai kuitaka.. ila mama aliutumia umama kulazimisha nifanye harusi..

ila najiona mjinga sana asingekuwepo mama yangu nisingeifanya kwa kweli...harusi ni ujinga
Duuh pole ila usiumie sana jamani
 
yote nilikuwa nayajua ila mama yangu ndio shida.. hela ndogo ndogo ya kulima au kuwekeza ninayo ila harusi nilikuwa siitaki na sijawai kuitaka.. ila mama aliutumia umama kulazimisha nifanye harusi..

ila najiona mjinga sana asingekuwepo mama yangu nisingeifanya kwa kweli...harusi ni ujinga
pole sana Mkuu ila siyo mbaya umeweka kumbukumbu muhimu kwenye maisha yako aise.
 
nacholaumu nina ndugu zangu hawana ajira au shughuli ya kuingiza kipato cha uhakika.. why nisiwape hela wao waizungushe zaidi ya kuitumia one day.. wanawake wenyewe tunaoa sababu ya watoto na kukuza familia.. wameanza kugongwa toka sekondari...mama niliongea nae sana akasisitiza anataka aone harusi yangu.. hapo sikuwa na jinsi

teh teh teh sikama hapo Mdau wanataka kumtoza 2m kumbe mtu mwenye kishagongwa muda mrefu tu alafu yeye wanataka alipie pesa yote hiyo itakua anapotesa bure tu
 
Fanya kitu kimoja muite demu wako mwambie hiyo pesa. huna, chakufanya unapanga chumba au km tayari unacho achomoke home kimyakimya afu ndani ya wiki moja make sure unaenda kujitambulisha. Fanya mpango kwa padri nunua ubwabwa wa kutosha na bia km kreti 5,na soda kisha ita ndugu wapande zote mbili funga ndoa, hakuna vikao wapige ubwabwa na kigeregere kwisha mchezo. Mziki woofer wako wa ujanani enzi za chuo.

Ukitumia pesa nyingi ni million 1. Maisha kwisha.
Mahari badae.

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Jambo la kuoa ni suala nyeti na ambalo linaendana na kuondoa uzinifu ila mazingira ya uoaji ndiyo huwafanya wengi kutokuoa hivyo kujikuta wakiingia dimbwi la zinaa.

Jambo zuri tunapaswa tuliangalie katika maamrisho ya dini zetu maana tukumbuke katika maamuzi ambayo hatupaswi kukurupuka ni pamoja na kuoa katika ukristo sitambui hukumu yake ila nitazungumzia kidogo kwa waumini wa dini ya uislamu in sha Allah...

Mahari katika ndoa ya kiislamu..
Habari njema kwa waumini wa dini hii ni kuwa uislamu ni dini iliyokamilika na haujaacha chochote ambacho kipo katika maisha yetu hivyo uislamu umezungumzia suala la mahari katika kuoa...hivyo hatupaswi kuhofia suala hili pale tunapotaka kuoa labda ukute familia ambayo hawaijui dini yao.

Kwanza mahari anayepanga ni mwanamke anayeolewa na hupanga kutokana na uwezo alionao anayemuoa na ili kumfanya kutoa mahari yaliyo ndani ya uwezo wake na alipe mahari yote ila pia kumfanya asiache kuoa kuhofia ukubwa wa mahari maana suala la kuoa ni wajibu..
Uislamu unahimiza kuoa
Mwenyezi Mungu ametupa neema kubwa sana ya kuwaumba wake zetu katika jinsi zetu.
Mwenyezi Mungu anasema:
"Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu,"
Annahl – 72
, hivyo mwanamke hupanga mahari hata ikiwa ataitaji chochote kilicho na thamani ndogo wazazi wake wanapaswa waridhie ndoa yao.

Ila tofauti ni kuwa wanawake baadhi, familia zetu na baadhi ya kabila wanaamini kuwa thamani ni pale unapoolewa kwa mahari makubwa hivyo kufanya suala la kuoa kuwa gumu na kuongeza idadi ya watoto kuzaliwa nje ya ndoa na kuwakosesha haki muhimu katika malezi bora.

Naomba kwa wakristo wanaofahamu dini inavyozungumzia mahari aseme pia.

Ushauri wangu.
Zungumza naye akaongee na wazazi wake kuwa hauna huo uwezo na usiishie hapo uende pia kuzungumza na wazazi wake kuwa nia ya kumuoa bintiye unayo ila uwezo wa kiasi hicho cha mahari hauna ili wakupunguzie na ufanikishe jambo hilo lenye kheri ndani yake
 
Kwa hali ya sasa mahari ya 2m ni kawaida sana. Kuna upuuzi mwingi sana katika koo zetu.......unadaiwa blanketi ya bibi wakati bibi anakaa Mwenge au Ilala, shenzi kabisa.

Halafu rubii hapo juu anasema wazaramo wanaolewa kwa mahari ndogo na kaonesha dharau. Kama alivyoeleza huyo Muislam hapo juu....wazaramo wengi ni waislam na dini yao inawahimiza kuweka mahari ndogo. Haijakatazwa kuweka mahari kubwa lakini kwao ni jambo la kawaida mtu kuambiwa mahari ya laki 5.
 
Kuna jamaa yangu alilipa mahari M3 na gharama zingine sendoff.
Mkewe anadaiwa zaidi ya m20 za Loan board.
Jamaa analalamika kila siku
 
Back
Top Bottom