Hivi watu wa hali ya chini wanawezaje kuoa na hizi mali?

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
14,602
31,905
Wakuu jana nilikuwa namdodosa mtarajiwa wangu juu ya vitu/mali inayotakiwa nikitaka kubeba jumla!!
Yaan kwa haraka hara inaenda kwenye million 2 hivi, sasa hapa nimewaza kama mambo ndo haya watu wa hali ya chini wanaoa vipi? Je ni kila mtu anafata hizi taratibu, kama hawafati ni njia gani wanatumia ili waeleweke ukweni?

Ebu nipeni mbinu, maisha ya ubachela yashanichosha na kuwapa watu pesa zote hizo bado ni mtihani kwangu...na biashara zangu zinaweza kuyumba!

Natanguliza shukrani!!
 
Hizo ni mila tu za KiTanzania na ukiziendekeza utavitoa hivo vitu kweli..
Pole yenu mnaooa familia za bibi anakaa kinondoni ila unaombwa blanketi la bibi..


Msomeshe demu wako kwamba huo uwezo wewe huna,,..au mwambie umuoe afu utalipa taratibu ila akiwa tyri kwako..haha
 
Mkuu mpaka suti zinahitajika aisee
 
Dogo mahari huwa hailipwi yote, tafuta laki nane oa. Lakini umezungumzia mahari tu? Je una hela ya sherehe?
 
Naona kuna bill zinakuja mtu anakomaa single 50, doubke laki,, hizi lawama afu kuna kitchen party then ndoa....sielewi...
 
Mkuu ni yeye tu..picha bado silielewi elewi yani!!
Mwambie huyo mchumba wako hali halisi, maisha yenyewe haya anayaona yalivo bana matumizi kwenye hiyo mil mbili ibaki hata laki tano..... Kwanza ni mtu wa wapi? Hiyo kapanga yeye au wazazi?
 
Usiogope mkuu,mahari huwa hailipwi yote! Unalipa kidogo kisha unaoa
 
nikijumlisha vurugu zote kuanzia mahari mpaka ndoa kuisha nilitumia karibu milion 6.... nikiwaza hela zangu najiona mjinga sana.. kuna hidden cost hapo kama shela, pete, nauli ya send off, gharama za church, bado harusi ina sehem zina mapungufu bwana harusi itakulazimu ujazie

ila yote alisababisha mama yangu ndie aliekuwa anataka harusi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…