Hivi unaweza ukaoa mwanamke hajui kupika?

Je unaweza kuwa na mpishi asie mke wako ?

Kwa tafsiri yako Mke ni nini ? Na ni kwamba kutokujua kwake hafundishiki au hataki ?

To each their own...
 
Salam,

Mwanamke amekamilika kila idara, Kitandani yupo safi tu ila hajui kupika. Je, wanaume unaweza ukaoa mwanamke wa aina hiyo?
Suala kubwa la kujiuliza kwa Nini mwanaume anaoa, je mwanamke kujua kupika ni kwa ajili ya mume peke yake au familia yote? Je Nini faida za mama mwenye nyumba kujua kupika?

Kuna majukumu ya mama ndani ya nyumba, na majukumu ya baba ndani ya nyumba, Moja ya jukumu kubwa la mama ndani ya nyumba ni kuhakikisha mume na watoto wake wanakula chakula kizuri.

Mama anayejua kupika anaweza kusimamia mapishi ya nyumbani kwake hata kwa hatua za mwisho tu, mfano kuonja chakula kilichoiva vizuri na kujua tatizo liko wapi kabla hakijafika mezani. Huu ni mfano tu. Kuna wamama wengi hawapiki lakini wanajua taste ya chakula kinacholiwa na waume zao na watoto wao.

Lakini Kuna jambo la asili, sometimes kupika kwa mwanamke ni feminine and romantic act, inaongeza sukari au ladha katika mahusiano. Mwanaume sehemu kubwa ya maisha yake na utulivu ipo katika tumbo lake, na asilimia kubwa ya wanaume wanakamatwa hapo, mwanaume part ya upendo wake ipo kwa yule anayempikia chakula kizuri, mwanamke anayejua taste za chakula za mwanaume wake ana chance kubwa sana ya kuwa na mahusiano mazuri. Mwanamke hawezi kuhangaika kujua chakula unachopenda au usichokipenda bila kuwa na chembe za upendo na heshima juu ya mwanaume huyo.

Watoto wanaokula chakula kitamu wana asilimia kubwa ya kuwa stable katika maisha ya nyumbani na shuleni. Kwa nyumbani chakula kitamu hakitoki katika mikono isiyo na upendo, hata wasichana wa kazi wenye upendo ndio wanaohangaika kupika chakula kizuri kwa wanafamilia.

Upendo wa familia uko kwa kiasi kikubwa kwenye chakula kinacholiwa katika familia hiyo, kuanzia kinavyopikwa, kinapikwa na nani, kinasimamiwa vp kupikwa, na mwisho kinaliwa vp, familia wanazokula pamoja ziko IMARA sana, kwani state ya stability na familia unaweza kuiona jinsi wanavyobehave wakati wa kula. Haya yote yameshikiliwa na mama.

Mwanamke akijua kupika vizuri ukijumlisha na attributes zingine anakuwa ni mke Bora na mama Bora kwa watoto wake. Mwanamke kujua kupika it comes with a lot of responsibility kwa familia in terms ya ustawi wa familia yake.

Suala la msingi kujua, mwanamke kujua kupika ni kwa ajili ya familia yake. Lakini ni Moja ya very important feminine and romantic character ambayo mwanamke anaihitaji katika kuweka ladha katika mahusiano yake.

Wanaume wanapenda wanawake wanaodisplay feminine characters, kupika ni Moja ya very feminine character yenye maksi nyingi kwenye mahusiano.

Jaribu kujiuliza zile hotel zenye romantic kitchen zinatumika vipi na kwa Nini hata cost yake Iko juu.

Sent from my Infinix X6820 using JamiiForums mobile app
 
Salam,

Mwanamke amekamilika kila idara, Kitandani yupo safi tu ila hajui kupika. Je, wanaume unaweza ukaoa mwanamke wa aina hiyo?
Kazi ya mke sio kupika.
-- kumstarehesha mwanaume,
-- kuzaa.


Hayo mengine Ni mambo ya kidunia tu.
 
Kusema ukweli nimejua kupika baada ya kumaliza skuli yaani chuo

Tena Alienisaidia ni bebi wangu maaana nilimwambia sijui kupika so akawa ana nielekeze kila siku napika kitu kipya kupitia msaada wa YouTube nashukuru Mungu mpk navoongea hapa naweza kupika chapati laini kiasi kwamba ikaliwa kesho bila kuwa kaukau

So kama anafundishika jaribu kumpa hizo tips za upishii kama unampenda utamsaidiaa
 
Mwanamke wako muite get mnunulie unga wa chapatiiiAkipikaa chapati zimenyookaa huyo Amekidhi vigezooo ilaa akikupikia chapati hazieleweki kama maisha yako mke hunaa
 
Back
Top Bottom