monjozee
Senior Member
- Sep 19, 2016
- 115
- 297
KWA HILI LA TBC SERIKALI SHARTI IJIWAJIBISHE ILI KUTOA MFANO KATIKA JAMII.
Na; Joseph Monia Politician
Ni takribani zaidi ya siku tatu sasa tangu Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambacho ni kituo cha serikali,kilipotangaza habari za uongo, za kutengeneza na za kupotosha jamii juu kupongezwa kwa rais Magufuli na rais wa Marekani ndg.Donald Trump.
TBC walitangaza kuwa rais Trump amempongeza rais Magufuli kwa utendaji wake, jambo ambalo ni la UONGO na UPOTOSHAJI.
Kituo cha utangazaji cha nchini Uingereza kupitia idhaa yake ya kiswahili yaani "BBC SWAHILI" hii leo wamelijadili suala na kuthibitisha kuwa TBC waliingia mkenge kwa kuokota taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii.
Hii ni aibu kubwa kwa TBC yenye falsafa ya "UKWELI NA UHAKIKA" pamoja na Taifa lote kwa kuonekana kutafuta sifa za kutengenezwa zisizo na uhalisia ndani yake
Naiomba Serikali ichukue hatua juu ya suala hili, hasa kwa kutangaza habari ya uongo na pili kwa kuvunja Sheria ya vyombo vya habari nchini.
Tumeshuhudia baadhi ya vyombo vya habari kupigwa faini, kupewa maonyo makali na vingine kufungiwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutangaza habari za uongo kama walivyofanya TBC.
"UUNGWANA NI VITENDO".
[HASHTAG]#Mytake[/HASHTAG]; Sifa hazitafutwi kwa kutengeneza matukio na kuaminisha umma mambo yasiyokuwepo.
Fanya kazi watu wataona, kisha matunda ya kazi yatakutangaza.