Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,811
- 15,404
Siku hizi ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utakutana na manung'uniko mengi kutoka kwa watu hususan sisi wazawa wenye rangi nyeusi yakituhumu ubaguzi katika kutoa huduma kwa wateja wenye ngozi nyeusi kwenye hii mighahawa ya kitalii.
Ukisoma maoni kutoka kwenye malalamiko ya mtoa hoja unakuja kugundua kwamba tatizo ni kubwa sana na baadhi ya mighahawa inayotajwa ni iliyopo maeneo ya Masaki Jijini Dar es salaam.
Sasa swali langu ni hili. Hivi hapa nchini hatuna taasisi ambayo inachunguza ubora unaotolewa kwa wateja si kwa hii mighahawa pekee bali pia na maeneo mengine?
Hizi tuhuma za ubaguzi kwenye mighahawa siyo ngeni na siamini kama serikali haizisikii lakini zimekuwa sikiishia kwenye mitandao ya kijamii bila kupatiwa suluhu.
Kama taasisi hiyo haipo kisheria kwa nini Bunge kwa busara zake isiunde chombo kitakachosimamia ubora wa huduma kwa wateja siyo kwenye sekta binafsi pekee bali pia kwenye taasisi za serikali ili kuboresha huduma kwa wateja bila ubaguzi.
Taasisi hiyo inatakiwa iwe inatuma wateja bandia na warekodi kila kitu ili kuwe na ushahidi iwapo kutakuwa na huduma mbaya na kuwachukulia wahusika hatua.
Naamini chombo hicho kitasaidia kuondoa malalamiko yanayotolewa kila siku kuhusu ubaguzi kwenye hii mighahawa inayotajwa kila siku.