Hivi taifa letu lina wasomi au wataalamu wa kugushi na kuingia na majibu yaani vibuti

Mi nadhani hiki kizazi cha sasa nacho uwezo umepunguzwa kidogo. Kwa sababu ukiangalia mambo mengi ambayo yanafundishwa kidato xha 3 na 4 leo, miaka ya nyuma yalikuwa kidato cha 2 kama si cha kwanza ila leo wanafunzi wanaferi, pia hata mitihani ya miaka hii ni mirahisi mno kuliko ya zamani il kuferi ndio kunaongezeka, acha hayo mchukue aliesoma miaka ya nyuma aliemaliza la 7 aliefundishwa na mwalimu wa UPE na mwanafunzi aliemaliza kidato cha 4 miaka ya karibuni aliefundishwa na mwalimu wa digirii, uwezo wao ni tofauti kabisa. Ni naona tufanyie uchunguzi na hili la upungufu wa uwezo wa kufikiri. Leo hii toa hesabu 25 mara 3 kati ya wanafunzi 100 basi 96 lazima watafute kikokotozi. Nakumbuka babuyangu anasemaga hii mizani ya kliniki inapunguza akiri, labda linakaukweli kidogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom