Hivi Pengo huwa ni wa St. Joseph ama St. Peter?

Ni sawa kuuliza Rais wa Tanzania ni wa Dar au Dodoma?
Kwa hiyo unadhani Pengo ni mkuu wa kanisa katoliki tanzania? Wakatoliki hatuna utaratibu huo. Pengo ni askofu mkuu wa Dar peke yake. Na pia kama kadinali ni raia wa Vatican. Ukadinali haumfanyi kuwa mkuu wa kanisa katoliki tanzania bali ni cheo tu kinachomweza kupiga kura kumchsgua papa kule roma na kushiriki katika shughuli mbalimbali za vatikani! Kwa hapa nchini Baraza la Maaskofu ndio chombo kikuu cha kanisa katoliki. Wanaweza hata kumfukuza Pengo!
 
Heh, hii mpya. Sio mkatoliki mimi ila sikujua kuwa Cardinal anaweza fukuzwa na Baraza la maaskofu. Ila hujasema atafukuzwa cheo cha uaskofu au kitu gani!!?
 
Nafahamu Kadinali Pengo ni askofu wa Jmbo Kuu la Dar es Salaam ambapo makanisa ya St Peter's na St. Joseph yako ndani ya jimbo hilo lakini napenda kujua je Pengo Kanisa lake la nyumbani ni lipi?

Personally nina ushuhuda wa hili japo kwa watakaojua zaidi yangu watanisaidia. Nakumbuka Kanisa Katoliki tokea huko nyuma Makazi halisi ya Cardinali huwa ni hapo lilipo Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay ambako kwa nyuma kuna nyumba kubwa tu. Wakati nikisoma vidudu / chekechea ( nursery / kindergarten ) hapo St. Peters back in mid 80's kila mchana tulipokuwa tukitoka Shule hapo Mimi na Marehemu Dada yangu Masista wa enzi hizo walikuwa wakitufuata hapo na kutupeleka kushinda na kucheza na Hayati Cardinal Laurean Rugambwa katika makazi yake kisha baadae tunafuatwa na kurudishwa nyumbani na sijawahi kusikia kama hata Makadinali wengine waliofuata waliubadili huo mfumo wa kuishi katika Nyumba yao hiyo hapo Oysterbay.

Ninachojua tu ni kwamba kule Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph ndiko Makadinali hufanya shughuli zao nyingi kwa kiasi kikubwa na nadhani kuna muda huweza hata kukutana na Wageni wao japo eneo lao Kuu la Shughuli za Kikanisa huwa ni kule Kurasini.

R.I.P Cardinal Laurean Rugambwa na Mwenyezi Mungu ampe maisha marefu na yenye afya bora Cardinal Polycarp Pengo.
 
Mkuu ninachojua ni kuwa wakati wa sikukuu kuu za kanisa hususani sikukuu kubwa katika kanisa kama pasaka ni lazima askofu mkuu asali katika kanisa kuu la jimbo na kukalia kiti cha kiaskofu.Na kwa taratibu za kanisa askofu mkuu anasali ile misa kuu na kwa jimbo la dar es salaam misa kuu ni ile ya saa nne katika la st joseph ambapo askofu mkuu wa jimbo analazimika kusali katika himaya yake.
sasa kwa alhamisi kuu na ijumaa kuu mwadhama amesali st joseph kama muumini wa kawaida pasipo kuongoza ibada(nadhani hii ni kwa sababu ya afya yake) na jumapili ya pasaka ile misa kuu anapaswa kusali kanisa kuu kama hataongoza ibada basi askofu msaidizi aongoze ila yeye lazima awepo kama atataka kwenda st peter aende baada ya kusali kanisa kuu.
kumekuwa na upendeleo sana kwa kanisa la st peter kuliko st joseph wakati ndo kanisa kuu.
 
nakumbuka wakati sista wangu yupo aekondari darasa moja na akina simon msuva..kuna kijana ana mwanya mkubwaa kama jino limeng'oka bt halioti tena..tangu form one wanamtania wanamwita kardinali pengo...
Si yule Ex wako mwenye pengo?
 
Kwa hiyo unadhani Pengo ni mkuu wa kanisa katoliki tanzania? Wakatoliki hatuna utaratibu huo. Pengo ni askofu mkuu wa Dar peke yake. Na pia kama kadinali ni raia wa Vatican. Ukadinali haumfanyi kuwa mkuu wa kanisa katoliki tanzania bali ni cheo tu kinachomweza kupiga kura kumchsgua papa kule roma na kushiriki katika shughuli mbalimbali za vatikani! Kwa hapa nchini Baraza la Maaskofu ndio chombo kikuu cha kanisa katoliki. Wanaweza hata kumfukuza Pengo!
Upo sawa ila umekosea kidogo.Baraza la maaskofu hawana uwezo wa kumfukuza Pengo wala Padri yeyote.
Si utakuwa raisi wa machizi wenzako. wabongo watakupongeza kama anavyopongezwa Kitale kwa mateja au kicheko kwa uswazi.
 
St. peters- hapa ni uaskofuni, yani makazi ya askofu mkuu was jumbo yalipo

St. Joseph- hapa ni makao makuu ya jimbo la daslam, pengo anakuja hapa pakiwa na matukio maalum ya kijimbo, ingawa Mara nyingi wanafanyia msimbazi kutokana na changamoto ya nafasi hapo st Joseph

NB. Hii IPO kwa baadi ya majimbo ambapo makazi ya askofu yanakuwa mbali na kanisa la jimbo, mfano, njombe Dodoma.....hapo unaweza ukae hata mwezi mzima kusipokuwa na tukio la kijimbo, au sherehe kubwa humwoni hapo...... Ila kuna majimbo mengine askofu anakaa na kusali hapohapo Manisa la jimbo
 
Pengo ni Askofu Mkuu, jimbo kuu la dar,St.peter's ni parokia ya dar,,,,tunawezaje kuhoji kwanini Pengo yuko St,Peter's,,,je angeingia mskitini tungesemaje
 
Back
Top Bottom