Hivi ninayechukizwa sana na tabia hizi zifuatazo niko peke yangu au?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,029
109,989
1. Nachukia tabia ya mtu kutopenda kwenda na muda na anajifanyia tu Mambo yake Kienyeji Kienyeji.

2. Nachukia tabia ya mtu ambaye hajui Kujipanga Kiratiba na yupo yupo kama Zombie fulani hivi duniani

3. Nachukia tabia ya Mtu kuamka asubuhi akiwa hajui hata atafanya nini Siku nzima

4. Nachukia tabia ya Mtu kutokuwa Up to date kwa Taarifa za Ndani na Nje ya nchi

5. Nachukia tabia ya Mtu ambaye najua kuwa Yeye ni Mpumbavu halafu Yeye anaona yuko sahihi kwa alifanyalo

6. Nachukia tabia ya Mtu ya kutojichanganya na Watu wa kila rika

7. Nachukia tabia ya Mtu kutopenda kuwa Mdadisi Mdadisi na Mpenda Kujisomea Magazeti na Vitabu

Ongezea zako ila ukitaka kuwa Rafiki wa GENTAMYCINE uwe na Sifa zangu tajwa hapa juu huwezi Kafie zako mbele tu Oky?
 
Kuna ya kuchukiza uliyo andika ILA 5, 6 & 7 inatakiwa busara kuya judge

Mfano:
#5; Huwezi kusema unajua mtu ni mpumbavu labda pia utuambie umetumia kigezo gani kumuona ni mpumbavu. Tambua tu kuna aina tofauti tofauti za Intelligence japo kwa upumbavu wetu tunadwanavyo thamini yule mwenye uwezo wa kukariri mavitabu na kujibu mtihani. Mf: Kama unafikiri kutunga nyimbo na kuimba ni rahisi mchukue Proffesor umshindanishe kuimba na Diamond Platnus

#6: Naona wewe unaongelea kundi moja la watu ulioko wewe ambalo ni extroversion. Lakini yapo makundi mengine likiwemo la wasio jichanganya ambao wengi huishia kuwa wasomi wabobevu (Doctors, Lawyers etc)

#7> Ukiongelea mtu mdadisi dadis, na kupenda kujua kila kinachotokea hapo unaongelea waandishi wa habari; sasa sijui unataka kila mtu awe wa fani hiyo?; Watu kama Doctors, Engineers, Lawyers nk wapo focused kwenye fani zao wala hawana time sijui ya Mange na jamii ya hizo mambo......
 
Hizo tabia ulizozitaja,zote ninazo na hunifanyi kitu,

Kila mtu aishi maisha aliyoyachagua,hatufanani

Live the life you love,love the life you live.

:cool:
 
1. Nachukia tabia ya mtu kutopenda kwenda na muda na anajifanyia tu Mambo yake Kienyeji Kienyeji.

2. Nachukia tabia ya mtu ambaye hajui Kujipanga Kiratiba na yupo yupo kama Zombie fulani hivi duniani

3. Nachukia tabia ya Mtu kuamka asubuhi akiwa hajui hata atafanya nini Siku nzima

4. Nachukia tabia ya Mtu kutokuwa Up to date kwa Taarifa za Ndani na Nje ya nchi

5. Nachukia tabia ya Mtu ambaye najua kuwa Yeye ni Mpumbavu halafu Yeye anaona yuko sahihi kwa alifanyalo

6. Nachukia tabia ya Mtu ya kutojichanganya na Watu wa kila rika

7. Nachukia tabia ya Mtu kutopenda kuwa Mdadisi Mdadisi na Mpenda Kujisomea Magazeti na Vitabu

Ongezea zako ila ukitaka kuwa Rafiki wa GENTAMYCINE uwe na Sifa zangu tajwa hapa juu huwezi Kafie zako mbele tu Oky?
nachukia mtu anae chukia chukia kilakitu kama wewe
 
1.nachukia vijana ambao muda wote ni ubishi wa simba na yanga
2.Nachukia vijana ambao hupenda kuisifia punyeto kama ndio unafuu wao wa mapenzi
3.Nachukia media za kibongo kukuza vitu vya kijinga wakati mambo ya maana yakiachwa nyuma
4.nachukia ukabila na udini maana hurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na taifa
 
Upendo ni pamoja na kumuacha mtu kuwa huru kufanya au kuwa vyovyote anavyotaka.
 
Back
Top Bottom