Hivi nifanyeje ili niweze kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi?

Kutokana na kasi na mwenendo mzuri wa serikali yetu hivi sasa chini ya Rais magufuli.

Na mimi nikiwa kama mtanzania mpenda maendeleo natamani sana kuteuliwa kuwa mkurugenzi au mkuu wa wilaya kwani najijua kabisa siwezi kuwa jipu na ninao uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii na kwa juhudi kubwa.

Na kwa kuthibitisha maneno yangu nipo tiali kufanya kazi hata kwa malipo ya nusu mshahara na nikienda kinyume na masharti ya kazi nipo tiali kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Kikubwa zaidi kilichopo moyoni ni kushirikiana na viongozi wenzangu katika kuwa letea wananchi maendeleo.

Swali langu ni kuwa je nifanyeje ili niweze kuteuliwa katika katika nafasi hizo?
Rekebisha uandishi wako, u dc faster.
1. Tiali = tayari
2. katika imejirudia
3. kuwa letea = kuwaletea.
 
Mi naamini kwa serikali zilizopita walikuwa wanaangalia vigezo vya uchama na usaidizi katika kampeni ila nina imani na serikali ya magufuli.
 
N wazi kuwa viongozi wanazaliwa na kuendelezwa vipaji vyao.Ingawa Ukuu wa wilaya ni cheo cha kuteuliwa,namwomba mteuzi na wanaomsaidia waone haja kunipa nafasi hiyo ili waione kazi yangu.Kila nilipoteuliwa,kazi niliifanya kwa bidii kubwa na kwa mafanikio.

Darasa la kwanza monitor,darasa la tano hadi la saba kiranja mkuu,sekondari makam mwenyekiti debate club,waziri wa uchumi,makam mwenyekiti Assa,chuo katibu na Rais wa muda kwa miezi minne hatimaye waziri wa habari na utangazaji,baada ya kuanza kazi mwl mkuu msaidizi ,nilipohama shule kule nilipokwenda baada ya mwezi nikawa mwl wa Taaluma,mwenyekiti wa walimu wote wa Taaluma,mwl mkuu kwa miaka mitano hadi nikapewa cheti cha The most improved school in Tanzania kupitia Matokeo makubwa sasa BRN na sasa masomoni nilipo nikichukua Diploma ya Ualimu wa sekondari ni mkurugenzi wa mawasiliano na katibu wa mfuko wa maafa na starehe na kidogo niuchukue urais wa chuo ila siye wa Diploma tulizuiliwa kugombea kwa kigenzo cha muda wa kukaa chuoni baada ya kuona nitawadefeat wa naochukua degree.

Wengine wanaweza kuniona wa ajabu lkn nimeona ninawiwa kuisaidia nchi.
0752473710
Tutakufukiria uafisa elimu wa wilaya.
 
Angalia CV ya makonda na tabia zake kwa wafalme na watoto wao, usipopewa basi fanya shuhuli nyingine tu.
 
Kutokana na kasi na mwenendo mzuri wa serikali yetu hivi sasa chini ya Rais magufuli.

Na mimi nikiwa kama mtanzania mpenda maendeleo natamani sana kuteuliwa kuwa mkurugenzi au mkuu wa wilaya kwani najijua kabisa siwezi kuwa jipu na ninao uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii na kwa juhudi kubwa.

Na kwa kuthibitisha maneno yangu nipo tiali kufanya kazi hata kwa malipo ya nusu mshahara na nikienda kinyume na masharti ya kazi nipo tiali kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Kikubwa zaidi kilichopo moyoni ni kushirikiana na viongozi wenzangu katika kuwa letea wananchi maendeleo.

Swali langu ni kuwa je nifanyeje ili niweze kuteuliwa katika katika nafasi hizo?
Ukitaka ukuu wa wilaya fanya mambo yafuatayo
1.uwe mkali mkali yaani ngumi mkononi
2.tafuta kiongozi wa chama pinzani umtukane kwenye media
3.umtafute mzee mashuhuri wa CCM anaekinzana na serikali kuhusu katiba umsemee mbovu au njia ingine kata funua. Ukuu wa wilaya si lelemama.
 
Dhana ya uwongozi inaanzia shule, makundi kama UVCCM, WAWATA, YCCS na BAKWATA ukiweza kujenga hoja kule na kuteuliwa kuwa mwakilishi wa wilaya na mkoa. Vinginevyo ingia jeshini unaweza kuwa kanali mstaafu ukapewa wilaya au mkoa.
me nishawahi kuwa mwenyekiti wa TYCS naweza pata ukuu wa wilaya?
 
Uwe unapambana na yeyote unaemhisi yuko upinzani!

Jitahidi kufuta vumbi kwenye viatu vya viongozi wa CCM kila unapowaona!

Tandika makofi yeyote unaemhisi ni mwanaharakati wa mabadiliko!

Kama wewe ni police hakikisha unatumia risasi za moto haswa!
 
Ukiona baadhi ya watu wanalilia kwenda ikulu jiulize pana kitu gani pale ikulu?

Siamini eti ili uwatumikie watanzania basi ni lazima uwe dc au mkurugenzi. Watu kama nyinyi ndio mnaochangia kuifanya nchi hii isiendelee. Haya tunaita ni mawazo mgando.

Ungesema unataka ugombee ubunge hata mimi ningekuunga mkono! Sasa eti unataka uteuliwe! Tangu lini mteule akamteua mtu asiyemjua? Mkomae tu na maisha hakuna jinsi.
 
Kutokana na kasi na mwenendo mzuri wa serikali yetu hivi sasa chini ya Rais magufuli.

Na mimi nikiwa kama mtanzania mpenda maendeleo natamani sana kuteuliwa kuwa mkurugenzi au mkuu wa wilaya kwani najijua kabisa siwezi kuwa jipu na ninao uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii na kwa juhudi kubwa.

Na kwa kuthibitisha maneno yangu nipo tiali kufanya kazi hata kwa malipo ya nusu mshahara na nikienda kinyume na masharti ya kazi nipo tiali kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Kikubwa zaidi kilichopo moyoni ni kushirikiana na viongozi wenzangu katika kuwa letea wananchi maendeleo.

Swali langu ni kuwa je nifanyeje ili niweze kuteuliwa katika katika nafasi hizo?

Hapo kwenye red sasa ndo mashaka yanapo anzia mkuu.
 
Back
Top Bottom