Hivi ni Taasisi yetu tu au Taasisi zote za Umma pesa imekua ngumu kwa Wafanyakazi?

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
26,149
75,253
Wakuu, especially waajiriwa wa serikali.

Hivi Na nyie ofisini kwenu pakavu kama kwetu au ofisi yetu ndio imekua mfano? Maana kusema kweli 2023 na 2024 hii miaka imekua migumu sana.

Posho hazitoki yapo madeni tu tokea ya September 2023, safari imekua kitu hadimu, vikao vya hela hamna wala kazi za masaa za ziada hazilipwi.

Okay, sasa sijui pesa ipo wengine tunabaniwa tuliopo chini au Taasisi zote sahivi zimebaniwa hela?

Nimechoka kushinda kwenye uzi wa Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Mliojiajiri karibuni kunitukana!
 
Back
Top Bottom