Hivi ndugu ama mdogo wako huwa unampa shilingi ngapi ya matumizi chuoni?

Wa kiume namchapa na laki moja.wa kike nampiga na 80.wa kike wana njia nyingi za kuingiza pesa hata ukampa milioni kwa mwezi atapewa tu tena.wa kiume namnunulia tv wa kike simnunulii maana atapewa tu.wa kiume nampiga na Tecno na wa kike nampiga na ka toch maana atapewa Samsung galax A3 hata usipompa. ni hivyo tu ndugu mtoa mada
hahaa mkuu we kiboko
 
Inategemea kama anaishi chuo au amepanga nje matumizi ni tofauti.

Wanaoishi chuo kama ni msichana kwa mwezi mpe 200000 au na zaidi kulingana na mfuko wako hapa ni pamoja na chakula na matumizi. Sasa kwa chuo inategemea kama ana mkopo au hana kabisa. ila awe anajua kutumia vizuri

mvulana mpe 150000 kama hana mkopo kabisa. Zinatosha.

Kama ana mkopo hapa inabidi ujue ana %ngapi?? Inatosha au haitoshi? Maamuzi ni wewe..

Nb inategemea maeneo chuo kilipo chakula ni sh ngap? Hilo ni muhimu sana.
upo sahihi
 
Ukiwa umechoka sana 5,000 kwa siku = 150,000 per moon, otherwise kama mambo safi angalau umpe 7,000 na kuendelea per day = 210,000 au maximum 250,000 (isizidi hapo utamharibu maana huku uraiani kuna watu wanalamba kilo 5 na kamaliza chuo wakikata kodi mtu anabaki 400,000 na maisha yanakwenda sembuse mwanafunzi
kbs mkuu
 
NAONA UUMPE TUU KAMA WANAVYOPEWA WENGINE MEALS AND ACCOMODATION NA SERIKALI. 8500 PER DAY INATOSHA HAIJALISHI SEHEMU ANAPOKAA AU JINSIA FANYA HIVYO HAYO MENGINE ATAKUWA ANAKUPIGA HELA. KUHUSU FIELD UMPE NYINGINE LAKI SITA KILA FIELD, KUHUSU STATIONARY MNUNULIE COMPUTER KUTOKANA NA MATUMIZI YAKE MAMBO YA COPY UTAKUWA UMEACHANA NAYO MAANA KAMA WAALIMU WANATOA HARD COPY KUNA SIMU NZURI SANA SIKU HIZI ATAPIGA PICHA HATA KWA KUTUMIA SIMU YA MWENZIE ILI ATASOMA KWA KUTUMIA COMPUTER . NA PIA NAULI YA MKOANI UMPE MZAZI YA NDANI YA CHUO ACHANA NAYO 8500 INATOSHA UTAKUWA UMEMAIDIA NAMNA YA KUPANGA BAJETI PIA
 
Mie Dogo langu nampa 3,000 tu kwa siku. Nilisha mwambia kuwa starehe kwa sasa hazimuhusu, Maisha magumu.
Anaenda na kurudi hivyo anapata mlo mmoja wa 1,500 chuoni the rest nyumbani. Notes kama ni nyingi anatoa taarifa anapewa pesa yake.

NB: Dogo ni wa kiume lakini.
 
Nyumbani walikua wananitumia 150K kwa wiki. Nilipo pata kazi kipindi nasoma, wakaacha kunitumia, matumizi yangu yakawa 100k kwa wiki, mpenzi nilikua nampa 70k kwa wiki na hii nilikua natoa kwenye sehemu ya salary yangu.
 
Back
Top Bottom