Hivi Ndivyo Pesa Inavyo Dhalilisha Watu Wazima.

Unaweza kuwa na mada nzuri lakini inaharibiwa na style yako ya kila neno kuanza na herufi kubwa... Kiukweli nimeingiwa uvivu hata kuisoma...
Kuna mkuu mmoja nae alikuwa na staili hiyo ya uandishi, nadhani alizingatia ushauri wa wadau na sasa amejirekebisha. Mimi binafsi mtu akiandika kwa herufi kubwa aya nzima, napata kichefuchefu na kuacha kushindwa kusoma. Hata hawa wanaotumia 'Title Case' ni tatizo.
 
Shida yako umechanganya kazi na mambo ya kuwa na pesa, huyo Mzee yupo kazini na ana majukumu yake aliyopewa, kama hajayatimiza ana haki ya kuambiwa ukweli, sasa jinsi ya kumwambia inategemea na "ntu na ntu" wengine wana lugha laini wengine ngumu
Umenena mkuu maana kama angekuwa ni mzee wa age yake napo tungesema vipi Ila Cha msingi uwe kijana au mzee ukishakuwa na pesa sio vizur kumdharau mtu yoyote tuwe nakauli angalau
 
Hapana na kamwe pesa isikufanye ukamtoa mwenzio utu pia na malezi mkuu hivi unaanzaje kumtukana mtu mzima aliyekuzidi umri kisa pesa. Binadamu tunajisahau sana jamani tuwakabidhi watoto wetu kwa Mungu katika malezi.
 
Back
Top Bottom