Hivi Muhubiri T.B.JOSHUA ana cheo gani CHADEMA&UKAWA?

Swali ni Kwanini TB joshua hakuhudhuria kuapishwa kwa JPM na wakati ndio alikuwa mwenyeji wake na JPM alienda kumpokea ?


Nini kilitokea Jamaa kuishia hoterini na kugeuza ?,mtoa Mada hujamalizia alichoongea Edward Lowassa .
Hapo kulikuwa kunanitatiza sana, hatimaye sasa nimepata jibu mujarabu kutoka kwa Lowassa kwa sababu nilikuwa najiuliza huyu jamaa (TB Joshua) alialikwa/alikuja kufanya nini hapa TZ kipindi kile?

Kwenye kuapishwa kwa Mlipuko hakuwepo ila namuona yuko na Lowasa muda wote huku serikali ikijigamba TB Joshua kaja kwenye kumuapisha Mlipuko.
Nikijiuliza sana
 
Huu ni mwezi mtukufu kutukana siyo issue mkuu!!......Am happy b'cause i well know that hate will never overthrow love!.....Hate will never win!......Solution badili tu hiyo avatar ya kike unayotumia!
Mbona bi mkubwa hajaniambia kuwa huu kwenu ni mwezi mtukufu,na amasema tuwahi kwenye kitimoto,ili aje awapikie kifungua kinywa cha jioni
 
So wachungaji wamezidiana power au wanaabudu mungu tofauti?
Mkuu nadhani unajua vyema kuwa kwenye usulushi tunaangalia pia "how influential msuluhishi atakua" ndo kusema wote wana nguvu na pia ni watumishi ila TB J ni more influential...pia ukaribu wa TBJ na pande zote unaweza changia yeye kuwa assigned mediation role.

Naamini wanamwabudu Mungu mmoja ila wao wanajua zaidi undani wa hili la kuabudu.
 
Usipoishughulisha akili yako hauwezi kuelewa jambo lolote,Baada ya uchaguzi mkuu kukamilika TB Joshua alikuja nchini kwa mwaliko wa serikali ya ccm,alipokelewa na maafisa wa serikali,akakutanishwa na mukulu na moja ya mazungumzo yao aliombwa anshawishi Mh.Lowassa ayakubali matokeo "fake" .

Ukiutazama uongozi huu kwa jicho la tatu,utaiona hofu ya serikali juu ya kile walichokifanya katika uchaguzi uliopita.Iangalie nguvu inayotumika kuuzima upinzani,kumbuka uvamizi wa vyombo vya usalama katika vituo vya kupokelea matokeo vya ukawa,kisha jiulize: ilikuwaje maafisa wa usalama wavamie na kuteka vifaa vyote vilivyokuwa vinatumika kupokea matokeo ya ukawa huku wakiviacha vituo kama hivyo vilivyokuwa vinasimamiwa na January na walimuacha January akiibuka kila baada ya muda akijitangazia ushindi bila ridhaa ya necccm?

Ni mwendawazimu pekee awezaye kuyaamini matokeo yaliyotangazwa, ukiwa na akili ndogo walau kama ya killlaza J,kamwe hutoweza kulishwa matango pori na kuyaamini matokeo fake.

Hili liko wazi,hata hao waliopewa ushindi wanatambua fika,lakini kutokana na ulevi wa madarakani na hofu yao juu ya madhira waliyolisababishia Taifa,waliamua kubaki madarakani kwa hila kama walivyompora Mh.Seif kule Zanzibar.

Leo hii tunashuhudia nguvu kubwa inayotumiwa na serikali na vyombo vyake kuuzima upinzani,hawafanyi hivyo kwa bahati mbaya,wanafanya hivyo kwa sababu walio katika mamlaka wanaifahamu nguvu halisi ya upinzani.Wanafahamu upinzani ulipata nini katika uchaguzi mkuu ndiyo maana wanahangaika usiku na mchana kuzima sauti za wapinzani.

Ni jambo la muda tu,lakini kwa mwenye akili hawezi kupoteza muda wake kujiuliza maswali ya matokeo ya uchaguzi uliopita.Mshindi na mshindwa wanajulikana na ndiyo maana leo hii tunashuhudia nguvu kubwa ikitumika kuulinda utawala uliokataliwa na wananchi.
Mungu akujalie maisha marefu
 
Swali ni Kwanini TB joshua hakuhudhuria kuapishwa kwa JPM na wakati ndio alikuwa mwenyeji wake na JPM alienda kumpokea ?


Nini kilitokea Jamaa kuishia hoterini na kugeuza ?,mtoa Mada hujamalizia alichoongea Edward Lowassa .
Alijua Lowassa hata muelewa kwani alikwisha piga mpunga mrefu sana, akaamua kumpotezea magufuli ili Lowassa abaki na amani kwamba atakua rais wa awamu ya tano kumbe kanyaboya!
 
Hivi unajua mahakama ya kimataifa ya ICC inashughulika na makosa gani?...

Maana tokea uchaguzi wa mwaka jana uishe watu mnataja tu ICC mara ICJ utafkiri inashughulika na matokeo ya uchaguzi
 
Ndiye Rais halali wa Watanzania waliopiga kura kwa zaidi ya 60% na wengi ambao hawakupiga kura. Liko wazi na hakuna cha TB Joshua hapa. Lowassa alishinda kwa kishindo. Tena kama kusingekuwa na kuchakachua angeshinda kwa 74-80%. Ni demokrasia nimesema na sitaki tujibizane na anti-Lowassa hapa.
 
Hivi unajua mahakama ya kimataifa ya ICC inashughulika na makosa gani?...

Maana tokea uchaguzi wa mwaka jana uishe watu mnataja tu ICC mara ICJ utafkiri inashughulika na matokeo ya uchaguzi
Si ndo mbowe aliyese atapeleka kesi ICJ
 
Ulitaka Lowassa ahamasishe watu kudai ushindi wake ili watu wamwage damu ufurahie..?? Tuna katiba mbovu ambayo hairuhusu mtu kuhoji au kupeleka mashtaka juu ya matokeo ya urais mahakamani!! Je endapo malalamiko yangeenda ICC, huko wana mamlaka ya kutengua matokeo ya urais baada ya kurangazwa na NEC?? T.B Joshua alitumia nafasi yake kama kiongozi wa kiroho na rafiki wa Lowassa kumshauri kama ambavyo angeweza kufanya kiongozi mwingine wa kiroho katika kuzuia jambo ambalo lingeweza kusababisha athari zinazoweza kuzuilika!!!
Haha ICC haina mamlaka yoyote juu ya uchaguzi wa nchi yetu na huyo lowassa angeshawishi watu wamwage damu basi ndio angekuwa wa kwanza kushtakiwa ICC...

ICC ina mamlaka katika haya makosa tuu

1. Makosa yanayohusiana na uhalifu dhidi ya Binadamu

2. Makosa dhidi ya uhalifu wa Kivita

3. Uvamizi......(agression)

4. Mauaji ya kimbari... (Genocide)..

je, kuna hata kosa moja hapo juu lilitokea kwenye uchaguzi mwaka jana?...

Kama hamna basi msihusishe uchaguzi wa mwaka jana na ICC kwa namna yeyote ile
 
Kama ........ni chaguo na kipenzi cha watanzania, kwanini sasa inatumika nguvu kubwa mno kuthibiti demokrasia? Hofu ya nini?
Big up mkuu. Anajua hakubaliki. Kuna kundi kubwa kwa sasa ingeitishwa uchaguzi wasingempigia kura na wanasena wazi mtaani. Achilia mbali walio ndani ya ccm na wale ambao walikuwa pro Lowassa au Ukawa wanaondoshwa madarakani kwa staili ya Majibu.
 
Amani ya bwana iwe nanyi wapendwa,
bila kupoteza muda,naomba nielekee moja kwa moja kwenye maada,binafisi nimekuwa nikishangaa juu ya matamshi ya ndugu E.N.Lowassa kuendelea kupotosha umma kuwa alipokwa ushindi wake wake huku akijifungamanisha na muhubiri wa kinaijeria ndugu T.B.Joshua kuwa hata yeye anajua kuwa UKAWA na viringe vyao walipokwa ushindi,naona huku ni kufirisika na kuishiwa kisiasa kwa ndugu lowassa na genge lake,hapa napata tabu kujua,je huyu T.B.Joshua ni nani mpaka lowassa amtumie kuthibitisha kuwa yeye ndo anajua kuwa alipokwa ushindi wake,je mahakama za kimataifa kama ICC inataarifa juu ya jambo hili kuwa huyu bwana aliporwa ushindi wake,binafisi naona CHADEMA&UKAWA Wanapaswa kumwandalia wahariri huyu bwana kabla hajaongea mbele za watu Ili kuepuka aibu kama izi, na akumbuke kuwa huu ni muda wa kujenda taifa na sio kufanya sanaa za maonesho majukwaani.
Yupo anayehitaji wahariri kwa kuwa matamshi yake huathiri wananchi wote wa nchi hi, si huyu ambaye ikitokea hivyo athari itakuwa tu kwa wanachama wa chama hicho na wafuasi wake...
 
Viva my President Viva forever in Majority of Tanzanians hearts.
 
Ukitaka kujua umuhm wa watu mbali mbali dunian angalia sehem zisizo na aman uone wapatanishi ni watu gan ndio utajua Tb joshua ni nan katka kauli ya Lowasa!

Nikukumbushe nafas ya wahubir dunian ni ilivyokubwa.
Hujiuliz kwa nn jumuia ya kimataifa kwann imempa Askofu Desmond Tutu amepewa tuzo ya nobel?
Yeye ni nan hapa dunian??

Kwa sisi wakristo tunaheshim maneno ya Bwana yesu , heri wapatanishi maana hao watauona ufalme wa Mungu. Joshua alifanya kaz hiyo.

La mwisho kama hujui nafas ya viongoz wa din dunian kuna uwezekano usijue nafas ya Mungu hapa dunian.

Binafs sio muumin wa Tb joshua ila yeye amechukua nafas ya askofu wangu ambavyo ningemsikiliza akinikanya juu ya athar ya jambo fulan ninalokusudia kulifanya. Kadharka kwa muislam nina iman huwasikiliza zaid viongoz wao wa din kuliko mtu yeyote dunian.

Lowassa yule ndie anaye mkubali heshm maamuz yake.
Na nyie msiwe mnakubali kila kitu asee. Yani muda woootee mliokuwa mnalazimishwa kuzungusha mikono na kujitoa akili halafu akatokea mtu mmoja toka Nigeria akawaambia achaneni na ushindi mlioupata na nyie mkakubali!? Fikirieni kiundani bas!!
 
Back
Top Bottom