Hivi kusaidia wazazi wa aina hii ni lazima?

Kusaidia ni jambo linalotoka moyoni, ni upendo wa ndani kabisa usio na mwisho, usioangalia mabaya, usio na kigezo chochote.

Si kila mtu anakuwa na huo Upendo.

Acha kusaidia kwa kuwa Umechagua kutokufanya hivyo, usitafute sababu huku JF ya kusaidia au kutokusaidia. Upendo huo ungekuwa nao Ungeshamsaidia kitambo.
Naunga mkono %💯.
Kama huna moyo wa kusaidia unaishia kutafuta visingizio ili uhalalishe ulichoamua
 
Hata pesa zangu sio zake hivyo nimeamua kutomsaidia
Pamoja na kwamba umeshafanya maamuzi ya kutomsaidia, nikutahadharishe kuwa huwezi kushindana na mzazi na ukashinda.

Kwanza, unakubali kuwa alichokifanya baba yako siyo kizuri na kilikuumiza sana na unao uchungu hadi leo. Lakini mshindi wa hili sio yule anayelipa kisasi, NI YULE ANAYEWEZA KUUSHINDA UCHUNGU, kusamehe na kumlipa mema aliyekukosa.

Pili, thamani ya mzazi (hata kama ni muovu) unaweza usiijue akiwa hai; lakini akitangulia mbele ya haki utaanza kutamani kwanini asingekuwepo?

Tatu, hata ufanikiwe namna gani usipokuwa na baraka ya mzazi kuna viwango vya mafanikio hutavuka. Baraka huwa zinaombwa, kwako hii ni fursa ya kumtendea baba yako wema ili uvuke viwango vingine vya mafanikio.

PIGA MOYO KONDE, YALIYOPITA SI NDWELE - TUGANGE YAJAYO; SHINDA UBAYA KWA WEMA. MSAMEHE BABA YAKO, MSAIDIE KWA KADRI YA UWEZO WAKO -- UTAKUJA KUNISHUKURU SIKU MOJA.
 
Mzazi ni Mzazi tu gentleman, hauwezi kumuokota jalalani au uende ukamnunue sokoni.

hakuna haja wala sababu hata moja kuchota laana na mikosi kutoka kwa mzazi wako.

huwezi kujua,
huenda hata kuzaliwa kwako mzazi moja wapo alisema, hii mimba tuichomoe tu halafu huyo Mzee unaemzodoa leo akasema, nitawajibika usiitoe, na ndipo ukazaliwa wewe japo una mfanyia kiburi hatari huyo Mzee, but still anakupenda na huyo ndiyo Baba yako mzazi, umuheshimu na kumsitiri ikiwa unayo nafasi kufanya hivyo,

hujafa hujaumbika,

sawa gentleman 🐒
Point ya maana mno asipokuelew basi akajiandikishe mirembe
 
Mkuu hela alikua anatoa akipokea mshahara ndani ya wiki pesa yake ya mshahara imeisha na si Kwa matumizi ya nyumbani ni Kwa kuhonga wanawake zake halafu tunaanza kulala njaa mzee kama huyu unamchukuliaje
 

Attachments

  • 20241122_230824.jpg
    20241122_230824.jpg
    35.4 KB · Views: 3
Pamoja na madhaifu ya mzazi wako msaidie tu. Chukulia kama funzo la kujifunza mwenyewe.

Mzee wangu hakutaka msikiliza mama wajenge hata Mimi nilipokuwa darasa la 3 niliwahi mshauri ajenge lakini hakunisikiliza.

Sijali madhaifu yake aliyofanya enzi za ujana wake. Nimechukua jukumu la kupambana kuwajengea wazazi nyumba. Walipo sasa siyo sehemu nzuri kwao. Mungu akijalia nyumba ikiisha watakaa wazazi , wadogo zangu hata ndugu wakipenda kuwatembelea wazazi wangu.

Kwa kuwasaidia wazazi kuna raha flani hivi naipata japo hali ngumu lakini napambana hivyo hivyo nyumba iishe.
 
Lakini yeye alishindwa kutulea vizuri watoto wake na uwezo alikua nao
Shukuru kwa chochote alichokupa mzee, ujue kuna watu pia wanadhani unaweza kuwapa pesa kiasi fulani ilhali wewe huo uwezo huna.

Kwahiyo inaweza kua kweli alikua vizuri au ni fikra zako tu ila uwezo hakua nao.
We mpe shukrani kwa kukuleta duniani, maana laiti kama angelikua hawapendi kiasi hicho wala asingetaka hata muishi kwake.
 
Back
Top Bottom