Hivi kuna pepo la viburi kwa watoto?

technology nayoinaharibu sana watoto, baadhi ya program za tvsio rafiki kwa watoto, mfano baadhi ya nyimbo, movie n.k. ni wajibu wa mzazi kua karibu na mtoto wake, umchagulia mtoto marafiki wazuri/wenye maadili, kumfundisha maadili ya kidini mapema.
asante umenifunua akili nikipata mtoto nataufuata mfumo huu
 
MASLAHI:
Walimu shuleni, masheikh madrasa, wachungaji kanisani wapo kimaslahi zaidi kuliko kujitolea kwa dhati km wazazi kufundisha maadili. Wazazi pia wapo biz na kutafuta pesa wiki nzima muda hakuna wakukaa na watoto wao

MAZINGIRA:
Majirani wanafurahia na kumuona mtoto wa mzazi mwingine akiharibika bila hata ya kuchukua hatua. Huku uswahilini kwetu pia nyumba za kupanga bei ghali watoto na wazazi wanalala chumba kimoja.

UTANDAWAZI:
Tumeacha mila na desturi zetu tulizorithishwa na wazee wetu na tunalea familia zetu kizungu..mtoto hata akikosea haguswi wala haambiwi kwa sababu atalia, wazazi au Tv wanapigana kiss, wanatukana matusi makubwa na kuvaa mavazi ya kisasa mbele ya watoto wao.
huo ni ugonjwa mkubwa sana tufanyaje sasa
 
a
dawa ni kumnyoosha mtoto tangu mdogo,kwa viboko au adhabu nyingine ambazo zitamuadhibu kweli na kutokana na kiwango cha kosa(adhabu iswe na madhara ya muda mrefu) tuwapende lakini tusiwadekeze bali tuwafundishe stadi mbalimbali za maisha tangu wakiwa wadogo.
nimekuelewa mzee mwenzangu nimekuelewa sana
 
Watoto hawana tatizo kabisa mkuu isipokuwa wanaenda sanjari na mabadiliko ya sayansi, teknolojia na mazingira kwa ujumla kwa spidi ya mwendokasi wakati wazazi mkitaka na kung'ang'ania kubaki na "umbumbumbu" wa enzi za mkoloni au mwinyi ambapo unakuta zee la miaka 16 linaogeshwa tofauti na watoto wa leo miaka 6 tu tayari alishajua kuficha "utamu" wake. Anaongea vitu vya kiutu uzima na anatenda kiutu uzima.
Cha msingi wazazi ndo tunatakiwa tubadilike ili kwendana na mazingira na hali ya watoto wa leo badala ya kubaki kuwalaumu na kudai ati sie wa enzi za mwinyi tulikuwa poa sana; poa sana wakati watoto wanaona tulikuwa wa hovyo kiasi cha kutishwa tu na kuamini, kwa mfano, "ukilia usiku mchawi anachukua sauti yako, mara ukikaa kwenye mafiga utakuwa mfupi kama mbilikimo n.k."
Hali ni tofauti kabisa kwa watoto wa leo hivyo wazazi tunatakiwa twendane nao kwa kasi ya Obama na tuwalee kama Obama yaani tuishi nao kama friends since their childhood na tuwaeleze ukweli juu ya athari ya chochote ambacho wewe kama mzazi unaona si kizuri mtoto kufanya.
NB. Viboko na vitisho kwa watoto wa leo havisaidii kuwajenga kimaadili bali mazungumzo ya ukweli na uwazi ndo yanawajenga na kuwafanya wajitambue zaidi.
 
Hakika na Mimi naishangaa mizazi ya sikuhizi limzazi unakuta lina mlea mtoto kama gari kwamba kama gari inavyo stahili kuwekwa petroli ndoliendi, na mizazi ya kisasa ndivyo inavyo walea watoto wao kwamba mtoto ili umtume inabidi kwanza umuhonge anachokitaka bila hivyo haendi. Yaani nikama ambavyo gari bila ya mafuta.

Nawazazi wana furahiya uzwazwa wawatoto wao nikatika wazazi wakileo ambapo limzazi linaweza kuishi na mtoto asiye na adabu hatakido na kuweza kuishi naye hata kwa miaka 20 bila yakuchepwa hata kwa kijiti cha chelewa.

Kimsingi tatizo ni

1wazazi
2wazazi
3wazazi
4jamii
5utandawazi
 
kweli mkuu kuna mdogo wangu yupo form two ni mbishi kila kitu anajua, kaz hataki kufanya yy akiamka ni misele.
Wapo wengine huku mtaan kwetu kamar imelala kichwan karudia form 2 tena shule za private mpaka mzaz wake kaamua ampeleke veta.
Watoto wa siku hiz pasua kichwa tena vibint ndio vimezalishwa mpaka kero kabint ka 1997 leo ukikutana nako barabaran kanakuambia "MAMBO" huwa nakasirika sana.
Vinaanza ngono vikiwa ktk umri mdogo.
Hiki ni kizaz cha dot com
 
Jana katika matembezi yangu ya mtaani nilishuhudia mtoto mmoja wa kiume kati ya miaka 13 akiwa anampiga mtoto mwenzie. Watu wazima walimsihi aache kumpiga lakini jamani mtoto yule aliwasonya wakamfukuza wampige wala hakukimbia akapigwa mabao lakini ameshika kiuno tu anawaangalia tu kwa dharau nilikuwa pembeni nikasema ngoja niondoke tu maana naweza kumrarua mwishowe dogo aliwasonya wale wazazi akaondoka
 
Watoto hawana tatizo kabisa mkuu isipokuwa wanaenda sanjari na mabadiliko ya sayansi, teknolojia na mazingira kwa ujumla kwa spidi ya mwendokasi wakati wazazi mkitaka na kung'ang'ania kubaki na "umbumbumbu" wa enzi za mkoloni au mwinyi ambapo unakuta zee la miaka 16 linaogeshwa tofauti na watoto wa leo miaka 6 tu tayari alishajua kuficha "utamu" wake. Anaongea vitu vya kiutu uzima na anatenda kiutu uzima.
Cha msingi wazazi ndo tunatakiwa tubadilike ili kwendana na mazingira na hali ya watoto wa leo badala ya kubaki kuwalaumu na kudai ati sie wa enzi za mwinyi tulikuwa poa sana; poa sana wakati watoto wanaona tulikuwa wa hovyo kiasi cha kutishwa tu na kuamini, kwa mfano, "ukilia usiku mchawi anachukua sauti yako, mara ukikaa kwenye mafiga utakuwa mfupi kama mbilikimo n.k."
Hali ni tofauti kabisa kwa watoto wa leo hivyo wazazi tunatakiwa twendane nao kwa kasi ya Obama na tuwalee kama Obama yaani tuishi nao kama friends since their childhood na tuwaeleze ukweli juu ya athari ya chochote ambacho wewe kama mzazi unaona si kizuri mtoto kufanya.
NB. Viboko na vitisho kwa watoto wa leo havisaidii kuwajenga kimaadili bali mazungumzo ya ukweli na uwazi ndo yanawajenga na kuwafanya wajitambue zaidi.
Viboko ni kwa watoto kati ya mwaka 1-8, baada ya hapo unamjengea nidhamu ya uoga-mbaya sana hiyo.
 
asante kwa mchango wako...ni funzo kubwa sana kwa sisi tusiokuwa na watoto
 
Hakika na Mimi naishangaa mizazi ya sikuhizi limzazi unakuta lina mlea mtoto kama gari kwamba kama gari inavyo stahili kuwekwa petroli ndoliendi, na mizazi ya kisasa ndivyo inavyo walea watoto wao kwamba mtoto ili umtume inabidi kwanza umuhonge anachokitaka bila hivyo haendi. Yaani nikama ambavyo gari bila ya mafuta.

Nawazazi wana furahiya uzwazwa wawatoto wao nikatika wazazi wakileo ambapo limzazi linaweza kuishi na mtoto asiye na adabu hatakido na kuweza kuishi naye hata kwa miaka 20 bila yakuchepwa hata kwa kijiti cha chelewa.

Kimsingi tatizo ni

1wazazi
2wazazi
3wazazi
4jamii
5utandawazi
wazazi kumbe nao ni chanzo enh...ila ni kweli mzee mwenzangu mizazi ya siku hizi sijui milofa...maana mh
 
Jana katika matembezi yangu ya mtaani nilishuhudia mtoto mmoja wa kiume kati ya miaka 13 akiwa anampiga mtoto mwenzie. Watu wazima walimsihi aache kumpiga lakini jamani mtoto yule aliwasonya wakamfukuza wampige wala hakukimbia akapigwa mabao lakini ameshika kiuno tu anawaangalia tu kwa dharau nilikuwa pembeni nikasema ngoja niondoke tu maana naweza kumrarua mwishowe dogo aliwasonya wale wazazi akaondoka
tuombee hiki kizazi kinapoelekea sipo kabisa
 
tatizo la wewe na watu wengi Africa na hata nchi za magaribi mnaangalia ujeuri wa mtoto kama vile ni jinsi mtoto alivyo tu na haijasababishwa na kitu. Lakini unakuta dunia ya leo hii watu, haswa watanzania wanapata hela alafu wakiwa na watoto wanataka wawape kila kitu. Wanaweka TV ili mtoto aangalie siku nzima, hawana jitihada za wao wenyewe kuwafundisha watoto wao kusoma, hawajengi uvumilivu kwa watoto na kila mtoto anapo taka kitu anapewa hapo kwa hapo. Wazazi hawawi makini na vitu kama condom au, vitu watoto wanavyoviona au kusikia kutoka kwa wao wenyewe wazazi, marafiki zao, au hata extended family. Vibaya zaidi waAfrica wanafikiri hekima ni kumpiga mtoto, na hawana jitihada ya kujenga mahusiano ya kiphilosophia na mtoto wao.

I. Usiwape watoto kila wanachotaka bali uwape unachotakiwa kuwapa kama mzazi. Hivi ni chakula, nguo, elimu, na sehemu ya kuishi. Kitu chochote kingine cha ziada ukitumie kama dhamana ya kuwafanya wakusikilize. Starehe na burudhani zinakuja wakiwa na adabu. Hii inamaanisha hata vitu vidogo kama soda, na pipi au burudani nyingine, unawanyima kama wakifanya kosa au unawanyima mpaka wakifanya vizuri either darasani au nyumbani.

II. Usiweke Tv Nyumbani kwako mpaka mtoto afike miaka 18. TV imeitwa idiot box na wataalamu na ni kwasababu nzuri. Watoto hawajengi uwezo wa kusoma vizuri au kufikiri vizuri darasani kama wanaangalia TV sana.

III. Uwe makini kuwafundisha watoto wako wenyewe jinsi ya kusoma, kuandika, na kucheza michezo ya nje na kutokukaa ndani siku nzima. Usifikiri ukiwapeleka shule watoto watajua kusoma. walimu hawawajali watoto wako kama wewe. hakikisha kila mwezi mtoto anasoma kitabu kimoja au zaidi.

IV. Uwasikilize na uwe makini kuwajibu na heshima wakikuongelesha kama wewe ungependa kujibiwa na heshima. Heshima ni barara ya njia mbili na hauwezi ukategemea kupata heshima kama wewe mwenyewe unawafanya watoto wako kama wanyama.

Jaribu haya kwa umakini, nikimaanisha wengine watafikiria kuwanyima watoto TV lakini wao wataangalia. Mtoto akiona hivyo ataona hamna haki nyumbani na atajenga chuki. Nilazima uiondoe nyumbani mpaka mtoto akifika miaka 18. Na internet uweke K9 Web Protection ublock website zote ambazo haziusu shule au elimu au kusoma. NA NI MUHIMU MTOTO ASOME KITABU KIMOJA KILA MWEZI, CHA LUGA ZOTE MBILI KINGEREZA NA KISWAHILI.
 
Hao wazazi wa kulea watoto kwa adabu wako wapi? Unawezaje kulea mtoto awe na adabu wakati wewe huna adabu, heshima, hekima wala busara.

Tusiwalaumu watoto wetu, wazazi wamekosa maadili, usidhani wataweza kuwapa watoto wao maadili mema.

Imagine mtu anarudi home after work, hana time na watoto, hawaogeshi na kuwaangalia miili yao, hawasikilizi, hawafundishi hata table manners, yeye na simu, simu na yeye.

Mwingine anarudi kalewa, mwingine anatoka kulalwa/kulala nje huko anarudi na majanaba na laana home. Hajawahi hata kukaripia na kufundisha kwa upole, achilia mbali kumshikia fimbo na kumuadhibu mtoto.

Kizazi kinaharibiwa na wazazi kwa asilimia kubwa sana.
 
Back
Top Bottom