100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 4,766
- 16,151
Ni takribani siku kadhaa sasa tangu internet nchini imekuwa na changamoto.
Hadi sasa tunachofahamishwa ni kwamba kuna nyaya huko baharini zimeleta hitilafu, hilo ndilo kila mmoja nchini utasikia akisema, sasa najiuliza na huu mtandao ulivyo chini ina maana kuna nyaya zilibaki ndizo zinaleta mtandao huu hafifu? Au tumekodi satellite kama backup kwa muda.
Hao wataalamu wa IT huko TCRA na mamlaka husika hawana uwezo kufanya press conference na vyombo vya habari kuelezea wananchi kwa kina au kutoa elimu mwanzo mwisho kuhusu jambo lililotokea na mfumo mzima wa huo mkonga unavyofanya kazi, je umeleta hasara ipi? Je kuna ulazima wa kuwa na back up kwa wakati ujao? Ilishawahi kutokea mara ngapi? Mitandao ya simu itafidia gharama za watumiaji walioathirika na hili tatizo? Kuna mengi ya kuelezea tena kwa maelezo ya kitaalamu ili wananchi waelewe. Au na hao IT na wao ni weupe vichwani kutoa maelezo, au pengine wateja au wananchi hawapaswi kuwa na uelewa wa kinachoendelea? Kingine serikali iangalie mawaziri wenye uelewa mkubwa kuhusiana na wizara husika.
Hili suala limeathiri shughuli za wengi, kuna vijana wana hizi online TVs, kuna vijana wana trade stocks n.k kwa kifupi internet imesaidia wananchi wengi kujiajiri kuna watu internet ndio maisha yao, lakini kwa jinsi mamlaka zinavyochukulia hili suala ni kama jambo la kawaida tu. Suala la mtandao ni issue serious. Kushirikiana na wananchi kunaweza pelekea utatuzi wa tatizo hili kwa siku zijazo.
Ukimuuliza mtu mbona mtandao upo chini utasikia kuna nyaya huko baharini zina hitilafu. Hizo nyaya zenyewe hajui hata zinafanana vipi. Ukimuuliza hitilafu imesababishwa na nini hapo jibu hana.
Wanasiasa na mamlaka husika nyie mmeajiriwa na wananchi lazima kuhakikisha wananchi wanapata updates kwa kila kinachoendelea kwa maelezo ya kitaalamu yasiyoleta shaka, vijana sasa wamesoma wana uelewa mkubwa kuhusu ulimwengu huu wa kidijitali.
Katika kituko cha karne ni pale kuna shida ya internet halafu mamlaka husika zinakwenda kutoa taarifa mtandaoni kupitia mitandao ya kijamii, sasa hao wananchi wanapata vipi taarifa?
Hii nchi tuna safari ndefu.