Hivi kulazimisha Ubatizo kwa Rc Makonda ili awe Bashite kuna tija kwa Watanzania ?.

Anayetuhumiwa anatakiwa yeye mwenyewe kukataa kuwa haitwi Daudi Albert Bashite. Tena akatae hadharani kama alivyowataja kwa Ujasiri watuhumiwa wauza/wala Unga kwenye vyombo vya habari.
 
Tija kubwa sana..yani uwizi wa cheti unasema sio tija? Ndio mana kuna sheria ya kuwadhibiti...Ethiopia isuburi kwanza tumalize hili la bashite
 
Anaezuia mchanga alikua mmoja wapo wa waliopitisha sheria ya kubebwa mchanga ulaya..halafu tujadili swala la mchanga kuzuiwa..huu ni unafiki wa kiwango gani?
 
Kama unaona hakuna ulazima

Je, kuna ulazima wa kumfunga Daktari aliyefoji vyeti akasomea udaktari na akatibu watu kwa miaka kadhaa au kumnyima mafao mtu aliyeitumikia nchi mda wote wa kazi?

Ukinijibu hayo tunaweza endelea.
 
Nawewe vyeti vyako vimehakikiwa au nawe ni fafafafafa kwahiyo unatetea fafafafaa
 
Mi naamini Bashite anajua Ben Sanaane alikoshia this holds a bond between
 
Tija ya vyeti vya Bashite, ni kutuaminisha na kutuhakikishia watanzania kuwa nchi yetu haiongozwi Kwa double standards. Hilo ni muhimu Kama serikali yetu inakusudia kutenda haki sawa kwa wote ila Kama ni serikali ya wachache basi vyeti hivyo si muhimu.
 
Wew
Wako baadhi ya watu ambao bila aibu wanahangaika na kumlazimisha Mkuu wa Mkoa wa Dsm aitwe Daud Albert Bashite, badala ya Paul Makonda. Sijui wanapata wapi mamlaka na sheria ipi inawaruhusu kufanya hayo, na najiuliza kuna tija gani kwa Watz kuhangaika na vyeti vya Rc Makonda? Wapo pia wenye mawazo finye wanalazimisha hoja kuwa, kwa vile tu JPM alianzisha uhakiki wa vyeti feki hivyo lazima na Rc Makonda ahakikiwe. Lakini hawajiulizi? Mwanzilishi wa Uhakiki ni JPM na siyo Gwajima au mtu mwingine yeyote, sasa iweje leo watu wasiokuwa na mamlaka ya uhakiki walazimishe kumhakiki Rc Makonda? Je JPM hakujua kuwa Rc Makonda hana vyeti? Hadi asubili Watu wapembeni kama Gwajima wapayuke ? Na wengine watumie tu-Mb twao kupost mitandaoni? Kwanini Watanzania tusijishughulishe na mambo yenye tija kama "Ugeni kutoka Ethiopia ambao unaleta tija na ajira nyingi kwa Watanzania? Ujio wa mwekezaji Dangote, Uthubutu wa kudhibiti usafirishaji wa mchanga wa madini usiokuwa na tija kwa nchi, JPM kudhibiti uhuni wa kuendeleza mikutano isiyokuwa na kikomo nchi nzima ? .Haya ni baadhi tu ya mambo ambao Wtz wapendao kupost mitandaoni wanatakiwa kufanya, badala ya kupost mistari miwili, Bashite, au Vyeti, tabia ambayo ni ya Kishetani. Tuweni Wazalendo hata kama kwa bahati mbaya tuliyekuwa tunampenda kura zilipungua. Tuwe kama Tundu Lisu ambaye kwa sasa ameamua kumkubali JPM kuwa ni Rais mahili na anafaa kuiongoza Tz, ndiyo maana amesema anaomba kukutana naye, na hakuthubutu kusema anataka kukutana na Rais Uchwara kama alivyokuwa akidai hapo awali. Big up Lisu kwa kutambua kosa lako na kukubali kuwa JPM ni Rais sahihi kwa Watz.
Wewe mwenyewe ume - post upuuzi mtandaoni na kwa maana hiyo na wewe ni mmbea wenye elements za ushetani ndani yake !!

All in all, hoja hapa siyo kubatizwa jina bali yeye kujibatiza jina jingine, imekujakujaje, Baasi. Aeleze tu tutamwelewa....

Aidha, sisi wengine tuliyesoma naye kuanzia Primary school level hadi ngazi ya O'level ktk miaka hiyo, we know him as Daudi Albert Bashite....

Shida inayokuja na ambayo ndiyo msingi wa mjadala huu kumhusu jamaa yako, ni ghafla kwa sura ileile tunayoifahamu lakini inaitwa jina lingine la Paul Christian Makonda tena akiwa mtu mwenye nafasi kubwa na nyeti ktk serikali....udadisi huu unaanzia hapa....

Ni yeye anayepaswa kuueleza umma ni lini na kwa nini alibatizwa jina jingine badala la lile la asili ambalo jamii na dunia nzima inamfahamu.....

Kumbuka kuwa si kosa kwa mtu kubadili kwa kubatizwa jina jingine, lakini mgogoro mkubwa zaidi wa huyu jamaa yako ni kubadili majina yote matatu, la kwanza, katikati pamoja na la ukoo wake.....

Hili kwangu mimi sijawahi kuona ubatizo wa namna hii popote pale.... kwamba ukane jina lako, la baba yako na la ukoo wako ?? Aisee, never ever !!

Mwisho kabisa, the point here is not about envy & jelousy but It's about intergrity and credibility of our leaders !!
 
Back
Top Bottom