Hivi kujenga mbona kama hakuna maana? - unajenga bangaloo lakini unazikwa kwenye kichumba cha mita 1*2.5

Eti wakuu?

Maana naona kila mtu yupo mbio kupanga matofali.

Au sisi wengine ndo kuna vitu hatuvioni?
Usiishie hapo tu kwenye kupanga matofali.
1. Unakuwa na nguo nyingi lakini unazikwa kwa Sanda tu ambayo hujawahi ivaa hata siku moja wakati wa uhai wako
2. Unakuwa na magari lakini unazikwa kwenye jeneza la mbao ambalo halitumii mafuta hata kidogo
3. etc
 
Eti wakuu?

Maana naona kila mtu yupo mbio kupanga matofali.

Au sisi wengine ndo kuna vitu hatuvioni?
Hvi siku hizi hawafundishi tena kwa kutumia vitabu vya Shaaban Robert? Kwa sababu mawazo finyu kama yako yalikuwepo miaka 100 iliyopita na yalishapatiwa majibu. Anyways, huku ni kuonyesha bado kuna binadamu wengine wana akili za kinyama, zinazowaza ''mimi'' na ''leo''. Zile akili za kusema tujenge barabara za nini wakati unyayo wa mtu hauzidi futi moja. Kwa kifupi tafuta kitabu kinachoitwa Kusadikika usome.
 
Unajenga kwa ajili ya watoto na kuepusha fedheha ukiwa na umri wa uraia pacha (duniani na peponi).

Ukifikiria kama unavyofikiria huwezi kujenga.
Maisha unayoinjoi kwenye nyumba yako ni mafupi kuliko unaowaachia na wana uhuru nayo kuliko wewe.
 
Usiishie hapo tu kwenye kupanga matofali.
1. Unakuwa na nguo nyingi lakini unazikwa kwa Sanda tu ambayo hujawahi ivaa hata siku moja wakati wa uhai wako
2. Unakuwa na magari lakini unazikwa kwenye jeneza la mbao ambalo halitumii mafuta hata kidogo
3. etc
Sehemu zote zenye umaskini uliokithiri watu hujiliwaza kwa maneno kama haya.
 
Back
Top Bottom