BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 497
- 1,200
Hii kauli ya Freeman Mbowe kuhusu kushangaa kuwa IGP Simon Sirro mpaka leo yupo ofisini na anashangaa mpaka leo bado yupo ofisini unadhani ni sahihi muda huu mkuu huyo wa Jeshi la Polisi anatakiwa akuwa ameshajiuzulu?
Mbowe ameelezea mambo kadhaa Machi 18, 2022, jinsi ambavyo Jeshi la Polisi linavyowatesa wananchi na ambavyo halitendi haki kwa asilimia kubwa.
Mimi naona Mbowe ana pointi, hivi inakuwaje mpaka sasa hivi Sirro bado yupo kwenye nafasi hiyo wakati hata chama tawala chenyewe kilishaonyesha hakina imani naye!
Mfululizo wa matukio ya askari polisi kuua raia wasiokuwa na hatia nayo ni sehemu ya kuonyesha jinsi gani ambavyo jeshi hilo limeoza, huo ndiyo ukweli, hata kitendo cha Rais Samia kuagiza uchunguzu juu ya mauaji ya mfanyabishara wa Mtwara ni wazi kuwa Sirro anatakiwa awe na uso wa aibu.
Nimeona mitandaoni Kigoma na kule Shinyanga kote kuna mauaji ya raia kwa kupigwa risasi na askari katika mazingira ambayo yanaonekana ni ya kizembe.
Achana na hiyo, fuatilia kwenye magazeti ya Mwananchi hivi karibuni, matukio ya askari kuua raia kizembe au kwa sababu binafsi ni kawaida kutokea.
Hivi Sirro hayo yote hauyaoni? Rais amesema, chama chake kimesema, wewe bado upo tu? Basi hata kama wewe huwezi kuwajibika, mbona hauonyeshi bidi yoyote ya kutaka kufanya mabadiliko kwenye jeshi lako hilo! Inasikitisha sana.