Hivi CHADEMA mtawaambia nini wananchi wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2020?

Yaani CCM unauliza CHADEMA watawaambia nini Wananchi? Hebu jioneeni huruma basi? Hayo uliyoyataja kuna hata moja lililokamilika, Yaani kwa jinsi Kikwete alivyopokelewa leo bungeni Sizonje kapata ujumbe kua ameshakataliwa.mjidanganye arudi tena kugombea, nawahakikishieni CCM mtaimba wimbo mwingine.
 
WaTz wana macho si kuku wa kizungu Lizaboni !!
1. Watoto wetu hawana mikopo ya kujiendeleza ki elimu.
2. Vijana hawana ajira kuanzia waliohitimu 2015 mpaka sasa.
3. Utumbuaji wa vyeti feki wenye double standard.
4. Serikali isiyowajali wakati wa shida zao eg Mafuriko na matetemeko.
5. Uteuzi uliojaa ukabila eg Mawaziri na ma RCs
6. Kuearudisha WaTz kwenye ujima (bunge gizani, siasa za mtu mmoja , visasi ndani na nje ya chama) etc

Mambo ni mengi na WaTz wanajuta kulazimishwa kulimia meno
Hakuna chanjo mahospitalini na mazao kupanda bei mara mbili zaidi. Huyu Lizaboni ametumwa na mabosi wake aje kuwachota maneno kwa bahati mbaya hata wakijua kero za wananchi hawawezi kuzifanyia kazi. Ccm ijiandae kung'oka kwa lazima.
 
Hakuna hata moja hapo litakalofanya Mgufuli asichaguliwe 2020. Huwezi kuwaamimisha watanzania ujinga huo, yaani kwa sababbu Makonda hajatumbuliwa basi iwe sababu ya kutomchagua rais anayepiga vita rushwa, ufisadi, uzembe kazini, Madawa ya kulevya n.k. Walionyimwa mikopo ndiyo wale walikuwa wanaziba nafasi za maskini. Jipangeni hivyo visababu vya kulazimisha habitawafikisha popote
 
Ugumu tu wa maisha wenyewe hivi sasa ni wazi kua CCM waliwalaghai wanamchi, Yaani CCM inachukiwa kama Kunguru watu hawana hamu nao kabisa.
 
Hakuna hata moja hapo litakalofanya Mgufuli asichaguliwe 2020. Huwezi kuwaamimisha watanzania ujinga huo, yaani kwa sababbu Makonda hajatumbuliwa basi iwe sababu ya kutomchagua rais anayepiga vita rushwa, ufisadi, uzembe kazini, Madawa ya kulevya n.k. Walionyimwa mikopo ndiyo wale walikuwa wanaziba nafasi za maskini. Jipangeni hivyo visababu vya kulazimisha habitawafikisha popote
Usiwadharau wananchi kiasi hicho, subirini 2020! Mlipiga pushups, magoti mlipiga kuomba kura, Kwa sasa inabidi mtandikwe viboko muache ulaghai wenu.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

CCM tuna mambo mengi ya kuwaambia wananchi. Si kuwaambia tu bali wanaona kwa macho yao. Hakuna blaa blaa bali bampa to bampa.

1. Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka umeanza kazi na wana Darisalama wananufaika. Huo ni mtaji wetu

2. Shirika la Ndege ATCL limeanza kusimama kwa miguu yake na limeweza kutengeneza faida ya bilioni 7

3. Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa hadi 2020 ujenzi utakuwa umekamilika hadi Morogoro. Na kabla ya kuanza kampeni, treni zitakuwa zimeanza ambapo umbali wa Dar Morogoro ni saa 1:30

4. Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Tanga utakuwa umekamilika. Tanzania tutakuwa Exporter wa mafuta kwenda nchi jirani.

5. Usambazaji wa umeme vijijini unapamba kasi kwa sasa. Hadi 2020, Asilimia kubwa ya vijiji vyetu vitakuwa na umeme wa uhakika na wa bai nafuu

6. Mradi wa kusambaza maji vijijini unaendelea kwa kasi. Hali hii imepunguza magonjwa ya kuambukiza kama kipindipindu. Kwa utawala wa Magufuli, Kipindupindu hakikubaliki

7. Milioni 50 kwa kila kijiji si ndoto tena. Mchakato wa kugawa fedha hizo unaendelea. Na wananchi wanaendelea kuhamasishwa kujiunga kwenye vikundi.

8. Hadi 2020, mikoa yote Tanzania itakuwa imeunganishwa kwa barabara za lami.

9. Hadi 2020, wananchi wengi watakuwa wameajiriwa kwenye sekta ya viwanda iliyoanza kupaa kwa kasi

10. Ifikapo 2020, ubabe wa Rais Magufuli utakuwa umezika kabisa tatizo la ufisadi, uzembe na uhujumu uchumi nchini.

11. Mwaka 2020 tutashuhudia Tanzania ikiongoza nchi zote za Afrika Mashariki katika kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

12. Uchaguzi Mkuu wa 2020 utafanyika kipindi ambacho Sekta ya Afrika itakuwa imeimarika na vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 5 vitakuwa vimepungua.

13. Hadi 2020, mazao ya biashara ya pamba, korosho, ufita, tumbaku, kahawa na alizeti yatakuwa na thamani kubwa kutokana na ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao hayo kujengwa kwa wingi hapa nchini.

Kwa kweli mambo ni mengi sana na nikiamua kuyaorodhesha yote, nitatumia zaidi ya siku mbili kuyamaliza.

Sasa tuje upande wa pili wa shilingi, vyama vya upinzani. Kick zao zote wanazotumia kuishambulia Serikali ni za msimu. Ni kama nyanya vile ambayo huwezi kuiweka ghalani.

1. Ile kick ya UKUTA imeishia wapi?

2. Kick ya Bunge Live imeota mbawa na sasa hakuna anayeiongelea tena. Watanzania wameanza kuuona ukweli.

3. Vipi kuhusu bei ya sukari? Hoja hiyo bado ina value kwa wapinzani? Nani anaiongelea?

4. Mapambano dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda yamenaki kwa Mange Kimambi tu.

5. Hivi wapinzani mnaungwa mkono na wananchi juu ya hoja yenu kuwa Rais Magufuli ni Dikteta uchwara?

Aiseeeee! Nawahurumia sana machadema. Nina hakika mzee wao Lowasa ambaye ndiye mgombea Urais wao 2020 si tu atashindwa kuongea bali atashindwa hata kuruka na chopa.

Lazima tuheshimiane.
Mwambie ukweli Kipara ngoto atakuwa kiongozi wa awamu moja tu
 
Magufuli kafanya mengi sana ndani ya mwaka mmoja tu mpaka 2020 wapinzani watakimbia majukwaa ya siasa
 
Yani bado mnatoa ahadi tu?!...Mi nilijua keshafanya kumbe ndio kwanza atafanya...mnatia kinyaa bora mnyamaze tu.
 
Hakuna chanjo mahospitalini na mazao kupanda bei mara mbili zaidi. Huyu Lizaboni ametumwa na mabosi wake aje kuwachota maneno kwa bahati mbaya hata wakijua kero za wananchi hawawezi kuzifanyia kazi. Ccm ijiandae kung'oka kwa lazima.
Mahospitalini hazihitajiki dawa za chanjo tu na dawa hizo za chanjo siyo kwamba hazipo muda wote bali inatokea tu kwa kipindi fulani tena kutokana na stock kuisha kabla ya iliyoagizwa kufika. Sababu za mazao kupanda bei haisababishwi na rais bali mabadiliko ikiwemo ukame n.k hayo ni mambo ya mpito tu. Jipangeni hoja zenu ni dhaifu sana
 
Wewe ndiye bwege kabisa! Kwani kuna Serikali isiyotumia pesa za Umma kujenga Miradi ya Maendeleo? Au nikuulize ni Serikali ipi imebuni Mradi wa DART? CHADEMA? CUF? NCCR etc? Acha ulofa wewe CCM imefanya mambo mengi mazuri pamoja na mapungufu kadhaa! Muulize baba yako atakuambia wewe Binti!
Mkuu hizo akili za CHAMDOMO, wanafikiri wakiingia madarakani wataendesha nchi kwa pesa za Mihadarati na BILCANUS.
 
Back
Top Bottom