Historia ya Rais John Pombe Magufuli

Bilionea kid

JF-Expert Member
Oct 19, 2018
581
519
John Pombe Joseph Magufuli (amezaliwa 29 Oktoba, 1959) ni rais wa tano wa Tanzania. Anatokea katika chama cha CCM.

John Pombe Magufuli
John Pombe Magufuli
John Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania
Tarehe ya kuzaliwa
29 Oktoba 1959
Chama
CCM
Dini
Katoliki
Elimu yake
Mwanakemia
Digrii anazoshika
Shahada ya Uzamivu
Alikuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki katika bunge la kitaifa huko nchini Tanzania na tangu mwaka 2010 waziri wa ujenzi.[1]

Tarehe 12 Julai 2015 alichaguliwa kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi na mgombea mwenza ni Samia Suluhu Hassani.

Tarehe 29 Oktoba 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ulimtangaza kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46% pamoja na makamu wa rais Samia Suluhu Hassani.

Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama rais wa tano wa Tanzania, ingawa upinzani haujakubali matokeo hayo.

Tarehe 10 Desemba 2015 alitangaza baraza la mawaziri likiwa na watu 34 tu katika nafasi ya waziri au naibu waziri, ndiyo baraza lenye mawaziri wachache ukilinganisha na uongozi uliopita.

Elimu

Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia miaka 1991 – 1994 alisomea Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza na miaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati. Kabla ya hapo Magufuli alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati, hiyo ilikuwa miaka 1981 – 1982.

Upande wa sekondari, Magufuli alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa huko Iringa kipindi cha miaka 1979 – 1981. Kabla ya hapo miaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza na miaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera. Hapo kati alikwenda Jeshi la Kujenga Taifa huko Arusha kwa mujibu wa sheria.

Ameandika vitabu na majarida mbalimbali.

Uzoefu wa kazi

Magufuli alipomaliza elimu yake ya ualimu katika chuo cha ualimu cha Mkwawa, kule Iringa, Tanzania mwaka 1982 akaanza kutumia taaluma yake ya Kemia na Hisabati kwa kufundisha shule ya Sekondari Sengerema hadi mwaka 1983.

Baada ya hapo akafanya kazi kama Mkemia katika Chama cha Ushirika cha Nyanza huko Mwanza hadi mwaka 1995 kisha akaanza safari yake ya siasa kwa kugombea ubunge mwaka 1995 huko Biharamulo Mashariki, kazi ambayo anaifanya hadi tarehe 1 Agosti 2015.

Akiwa Mbunge wa Biharamulo Masahriki huko Chato amekuwa Naibu Waziri na Waziri katika Wizara mbalimbali. Tangu mwaka 2000 hadi 2005 alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi. Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki. Mwisho 2010 – 2015: Waziri wa Ujenzi.

Uchaguzi wa urais wa mwaka 2015 Edit

Tarehe 22 Julai Magufuli alichaguliwa kukiwakilisha Chama cha mapinduzi kama mgombea urais kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka, 2015, alipongezwa na naibu katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Asha-Rose Migiro na balozi wa Marekani kwa umoja wa Afrika Amina Salum Ali kwa kwenda kukiwakilisha chama.

Japokuwa alikutana na changamoto kubwa ya mgombea mwenzake wa chama cha upinzani Edward Lowassa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, tume ya taifa ya uchaguzi ilimtangaza Magufuli ndiye mshindi kwa asilimia hamsini na nane. Mgombea mwenza, Samia Suluhu, pia alitangazwa kuwa makamu wa rais. Kuapishwa kwa Magufuli kulifanyika tarehe 5 Novemba 2015.

Ndani ya mwezi mmoja tangu alipoingia madarakani ameanza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha ndani ya serikali kwa kufuta baadhi ya sherehe zisizo na ulazima pamoja na kupambana kwa dhati na wakwepakodi.

Hivyo amefanikiwa kujenga imani ya wananchi wengi wa Tanzania ambao kwa kiasi kikubwa walionyesha kuchoshwa na uongozi wa chama chake.

Wananchi wa Tanzania, nchi jirani na baadhi ya mataifa makubwa wamepongeza utendaji wake, ingawa wengine wanajiuliza kama kasi hiyo itaendelea.
 
naomba kujua vitabu na majarida aliyoandika au ni siri 😁😁😁😁
 
Hujatuambia kuwa jpm alizaliwa wapi na wazazi wake walitokea nchi gani, shughuli walizojihusisha nazo, alafu ndo ulete huo uongo wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom