haya mambo ya kushauri mtaalam mwelekezi wakati mmeajiri maenjinia wazuri tu tena wanaofaham mazingira halisi ya kitanzania ndio apo tunapoanzaga kuliwa....ushaur wa nini ina maana hamjui mnachokitaka?
Mkataba wa Euro 4,678,580 na USD 402,833 kwa ajili ya malipo ya ushauri (consultantation) ?
Je hio miradi inayoshauriwa na kusimamiwa na huyo consultant ina thamani gani?
Hadi muda huu, huyu mayor wa Kinondoni namuona kama jipu, tusubiri muda utatuambia, soon ataingizwa king, amepania sana.
Usi 'pige kelele' kwa maandishi makubwa kuna watu hawapendi kusikia wengine wana sifiwa kwa mazuri wanataka wasifiwe wao tu, wasije wakaanza fitina.viva UKAWA kwa mwanzo mzuri.
Kama jambo hulijui vizuri uulize au ukae kimya unaonekana kituko kwa sababu hujui kazi ya mtaalam muelekezihaya mambo ya kushauri mtaalam mwelekezi wakati mmeajiri maenjinia wazuri tu tena wanaofaham mazingira halisi ya kitanzania ndio apo tunapoanzaga kuliwa....ushaur wa nini ina maana hamjui mnachokitaka?
Huwezi kufanya Miradi mikubwa yoyote bila kuwa na mshauri mwelekezi,hata serikali kuu huwa wanatafuta mshauri mwelekezi wa Mradi husikahaya mambo ya kushauri mtaalam mwelekezi wakati mmeajiri maenjinia wazuri tu tena wanaofaham mazingira halisi ya kitanzania ndio apo tunapoanzaga kuliwa....ushaur wa nini ina maana hamjui mnachokitaka?
Kwahiyo huyu mtaalamu mwelekezi ndio atamaliza matatizo? au ndio kwanza anafanya upembuzi yakinifu? kwahiyo tunahitaji mgeni atufanyie upembuzi yakinifu hao maprofesa wa udsm na ardhi university hawajui kitu? hizo bil sita atakazolipwa hao wa chuo kikuu siwangefanya bure kwani wanalipwa mishahara na serikali.View attachment 340966 FOLENI, MAFURIKO KUWA HISTORIA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.
Hayo yamesemwa leo Jumatano tarehe 20 Aprili 2016 na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jackob wakati wa hafla ya kusaini Mkataba Na Kampuni ya MS/H.P GAUFF INGENIEURE GMBH&CO, KG -JBB ambayo ni mtaalam Mwelekezi (Consultant) atakayetoa Huduma za ushauri elekezi (Consultant services) katika, usimamizi wa ujenzi wa Miradi ya DMDP (Dar es salaam, Metropolitan, Development Project) itakayotekelezwa ndani ndani ya Manispaa ya Kinondoni wenye thamani ya URO 4.678580 Na USD 402833 utakaodumu hadi mwisho wa muda wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Mtaalam huyu mwelekezi atakuwa Na jukumu la kuhakikisha kazi zitakazofanyika zinakuwa katika mpangilio uliokubalika, (Designing) Na kwa kuzingatia ubora Na thamani ya miradi (Value for Money) ili wananchi wote wa Manispaa ya Kinondoni Na jiji la Dar es salaam, wanufaike Na miradi hiyo kama ilivyokusudiwa katika malengo yake.
Halmashauri ya Kinondoni ina miradi 11 inayogusa maeneo ya Ujenzi wa Barabara za Halmashauri kwa kiwango cha lami zinazolenga kupunguza msongamano (Local Roads) Uboreshaji wa Miundombinu katika maeneo yasiyopangwa (Infrastructural upgrading in unplanned Settlements) Ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua (Storm water drainage) Uimarishaji wa mifumo ya Mapato ya utawala Bora ya taasisi (Institutional Strengthen) Na Usimamizi wa taka ngumu (Solid waste Management)
Kwa mujibu wa upembuzi yakinifu uliofanywa Na wataalamu waelekezi (Consultants), Kati ya miradi yote 11 ya awamu ya kwanza na awamu ya pili, miradi 5 ya Barabara itakayotekelezwa katika awamu ya kwanza wakati wowote kuanzia sasa ambayo haihitaji ulipaji wa fidia katika utekelezaji na barabara 6 zitajengwa baada ya Manispaa kulipa fidia katika maeneo ya miradi, zote kwa ujumla zina urefu wa Kilometa 20.75 Na zitagharimu Tsh 26,552,114/= na fidia ya Tsh 6,672,251,760/=.
Mradi wa Uboreshaji wa maeneo yasiyopangwa utagusa kata 3 za Mburahati, Tandale Na Mwananyamala utakaohusisha uwekaji wa Huduma muhimu kwa kuboresha Miundombinu ya barabara, taa za barabarani, taka ngumu, njia za waenda kwa miguu Na maji safi utakaogharimu Tsh 1,264,576/= na fidia ya Tsh 180,413,275/=.
Aidha mradi wa Ujenzi wa mto Sinza (Mto Ng'ombe) wenye urefu wa Kilometa 7 kuanzia chuo cha maji Dar es salaam hadi mto Msimbazi kupitia kata 6 za Ubungo, Sinza, Mwananyamala, Ndugumbi, Magomeni na Hananasif umelenga kuuwezesha mto huo kupitisha maji kwa urahisi Na kuepusha mafuriko Na utagharimu Tsh 20,100,000/= Na utahitaji fidia ya Tsh 4,054,499,410/=.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob amewahakikishia wananchi wote wa Manispaa ya Kinondoni kuwa kwa kushirikiana Na Baraza lake la Madiwani na Serikali kuu na wadau wengine wakiwemo waheshimiwa wabunge, watafanya kila jitihada ya kutafuta fedha za kulipia fidia ili miradi hiyo ambayo inahitaji fidia ianze kutekelezwa na kukamilika kwa wakati ili kuwapunguzia wananchi kero ya msongamano uliopo ndani ya jiji la Dar es salaam.
wacha kuwasingizia wakwetu hiyo mitaro ilijengwa na konoike.Hizi zilizopo wamejenga hao wetu ikinyesha mvua dakika kumi tu balaa lake tunalijua,acha tujaribu mawazo mapya tutalinganisha baada ya miaka mitano,maana hao tuliwapa miaka hamsini walichofanya tumekiona.
Hebu tupe kwa kifupi hao ma engineer wazuri wamefanya nini hadi sasa? Nijuavyo mimi Kinondoni ndio barabara hutengenezwa na kudumu miezi mitatu sasa huo utaalam wa hao maengineer wameuweka makabatini au?haya mambo ya kushauri mtaalam mwelekezi wakati mmeajiri maenjinia wazuri tu tena wanaofaham mazingira halisi ya kitanzania ndio apo tunapoanzaga kuliwa....ushaur wa nini ina maana hamjui mnachokitaka?
Kweli mkuu hata mimi nimeshangaa sana mkuu!!!!Mkataba wa Euro 4,678,580 na USD 402,833 kwa ajili ya malipo ya ushauri (consultantation) ?
Je hio miradi inayoshauriwa na kusimamiwa na huyo consultant ina thamani gani?
Hadi muda huu, huyu mayor wa Kinondoni namuona kama jipu, tusubiri muda utatuambia, soon ataingizwa king, amepania sana.
Hata ya huku Tandale mkuu?ha ha ha hawacha kuwasingizia wakwetu hiyo mitaro ilijengwa na konoike.
Hivi kwa akili zako fupi unadhani hao consultants wametafutwa na wamenegotiate kwa mwezi mmoja na kustrike a deal?? Hii ni kitu ilikuwapo toka mwaka jana, kizuri ni kwamba wasimamizi watakuwa ukawa maana wanataka kuimpress. Ila ni mipango ya sisiemu.viva UKAWA kwa mwanzo mzuri.