Historia Fupi ya Siku ya Wapendanao (Valentine's Day)

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
319
666
Hii ni siku inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Februari 14. Imetokana na Mtakatifu, Askofu wa Kanisa Katoliki wa miaka ya 496 baada ya Kristo aliyeitwa Valentino.​


Siku hii watu wengi huiadhimisha kwa kupeana zawadi mbalimbali kama kadi, maua na nyingine nyingi zenye ishara ya upendo.

Fahamu tu siku hii ni maalum kwa kumkumbuka Padri Valentino aliyeuawa na Utawala wa Kirumi kwasababu ya kutetea waumini waweze kufunga ndoa.

Sasa ilikuwaje hadi siku hii iwe siku maarufu duniani na siku pendwa kwa watu wengi hususan walio katika mahusiano ya kimapenzi?

Sikiliza hii! Katika miaka hiyo kulikuwa na vita kama ilivyokuwa desturi ya falme nyingine ili ziweze kujiongeza na kujiimarisha kiutawala.

Mfalme Cladius II naye alikuwa mtawala aliyependa sana kupigana vita na majirani zake katika kile kinachoitwa kukuza eneo analolitawala.

Inaelezwa katika vyanzo mbalimbali kuwa, katika utafiti mdogo alioufanya Cladius, aligundua kuwa wanajeshi wasiooa, ndio walikuwa imara kuliko waliooa.

Ndipo Cladius akaweka marufuku na kuwataka vijana wasifunge ndoa badala yake, wajiunge Jeshini.

Baada ya muda kupita, Mfalme Cladius II akapata taarifa kuhusu mambo ya siri ya kufungisha Ndoa anayoyafanya Padri Valentino.

Akaagiza akamatwe na kumtaka Valentino aachane na kile anachokifanya. Valentino hakukubaliana na matakwa ya Mfalme na kubaki katika msimamo wake.

Habari zinasema baada ya msimamo huo, Mfalme aliagiza Valentino akamatwe na ahukumiwe adhabu ya kifo.

Inasemekana kwamba muda mchache kabla hajanyongwa, Valentino aliomba kalamu na karatasi na kuandika ujumbe uliohitimishwa kwa maneno: “From Your Valentine” akimaanisha (Kutoka kwa Valentino wako). Maneno haya yamekuwa yakitumika sana katika siku hii.

Valentine akanyongwa Februari 14 mwaka 269 AD.

Nikuache na hili Mdau wa JamiiForums! Siku hii imelenga kuhamasisha watu kupendana.

Hii ni kusema kuwa, unaweza kuonesha upendo kwa mtu yeyote, si lazima awe mwenza wako.

 
Back
Top Bottom