Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 14,386
- 53,866
Kujiuzulu kwa Ndugai kumeambatana na hisia tofauti za wananchi. Lipo kundi la wananchi libalooamini kuwa kilichomfanya Samia akasirike, kuwa mbogo na kukunjua makucha dhidi ya Ndugai kinyume cha haiba yake ya upole ambayo wananchi wameizoea ni. kutokana na Ndugai kuonyesha mshangao bungeni wa kwa nini takriban shilingi bilioni 230 ambayoni sawa na 17% ya mkopo wote kupelekwa Zanzibar yenye watu wasiofika milioni 2,halafu eti kilichobaki ndo kigawiwe kwa watu milioni moja 58 waliobaki.
Wachambuzi wa Mambo wanasema hilo suala lilimkera Bi Mkubwa na kwa hiyo akawa anatafuta timing tu ya kumla Ndugai kichwa. Watu wanaozungumzia sakata la Ndugai wanasema licha ya mambo mengi mabaya ambayo Ndugai amewahi kutenda, lakini hili suala la kuzungumzia mikopo siyo suala kubwa kivile la kusabanisha rais awe mbogo. Watu wanasema Rais ana Jambo lake, Nalo ni Zanzibar!. Wananchi wanasema ukiigusa Zanzibar, Samia hatokuacha!
Wanaopinga Mihela mingi kwenda Zanzibar wanasema kuwa Zanzibar yenyewe kwa yenyewe hata kama ndiyo iliyokopa kupitia jina la Tanzania, haina uwezo wa kulipa mabilioni yote kwa hiyo at the end of the day Kwenye ulipaji licha ya kuwa ni kweli tutalipa kama nchi, lakini zigo zito litabebwa na watanganyika.
watu wanahoji kuwa, Zanzibar ambayo bajeti yake haijawahi kufika Trillion mbili, yenye kudaiwa deni la Umeme miaka nenda rudi, itapata wapi pesa za kulipa shilingi bilioni 230 kama hilo deni siyo zigo litakalobebwa na watanganyika?
Wapo wanaotetea mabilioni mengi ya idadi hiyo kwenda Zanzibar kwa hoja kuwa Zanzibar ni nchi, hata hivyo watu hao wanajibiwa kuwa Zanzibar kuwa nchi hskumfanyi Mzanzibar astahili zaidi kuliko mtanzania mwingine yeyote.
Wananchi hasa mitandaoni, wamekuwa wakijadili aina ya muungano wetu na kupendekeza ufanyiwe marekebisho. Watu wanahoji, Kwa nini Mranganyika hana power juu ya mambo ya ndani ya Zanzibar yasiyo ya muungano, lakini Mzanzibar anaweza kuwa Mtawala ambaye ana amri juu ya mambo ya Tanganyika yasiyo ya Muungano?
Kujiuzulu kwa Ndugai na namna alivyojiuzulu kumeibua hisia kali na mijadala mikali mitandaoni. Ngoja tuone hili sakata litaelekea wapi!