Mtoto wa Shule
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 14,207
- 11,308
Twambie kwanza, mradi wa umeme wa Mwl. Nyerere utakamilika lini. Hatutaki maswala ya gesi kwani Rais Magufuli aliishatwambia kuwa huko tushapigwa.Contents za Mh. Waziri Makamba
1. Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia nchini ulianza mwanzoni mwa miaka ya 1950. Mafanikio makubwa yalipatikana yakiwemo ugunduzi wa gesi asilia katika kisiwa cha Songo Songo mwaka 1974 na Mnazi Bay mwaka 1982. Aidha, Katika miaka ya 2010 na 2012 utafiti uliendelea katika maeneo ya kina kirefu cha Bahari ya Hindi. Hadi kufikia mwezi Mei 2022, jumla ya Futi za Ujazo Trilioni (TCF) 57.54 za gesi asilia ziligunduliwa katika maeneo ya nchi kavu na kina kirefu cha bahari. Kati ya kiasi hicho Futi za Ujazo Trilioni 47.13 zimegundulika katika Vitalu vilivyopo katika kina kirefu cha bahari ya Hindi, na Futi za Ujazo Trilioni 10.41 zimegundulika kutoka maeneo ya nchi kavu.
2. kutokana na ugunduzi huo wa kiasi kingi cha gesi asilia, Serikali ilifanya maamuzi ya uanzishwaji wa Mradi wa Kusindika na Kuchakata Gesi Asilia (Liquefied Natural Gas -LNG) kama njia bora ya kuendeleza rasilimali hiyo kwa ajili ya kuuzwa katika masoko ya Kimataifa na sehemu nyingine ya gesi hiyo kutengwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi
3. Serikali kupitia TPDC itashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huu. Ushiriki, katika ubia na ushirika wa uendeshaji wa mradi, utasaidia kujenga uwezo wa Shirika hili ili miaka ijayo liweze kufanya shughuli hizi lenyewe na kwa tija na ufanisi kwa manufaa makubwa zaidi kwa taifa. Safari ya kuisuka upya TPDC kama Shirika mahiri na la kimkakati imeanza kwa wewe kutupatia Mwenyekiti wa Bodi mzito na sisi tumeunda Bodi mpya yenye kutoa mwelekeo wa dira mpya tunayoitaka kwa TPDC.
4. Manufaa yatakayopatikana katika utekelezaji wa mradi huu ni pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi; kujenga uzoefu wa TPDC kupitia ushiriki wake; kuongeza mapato ya Serikali yatakayotokana na mauzo ya gesi; upatikanaji wa gesi asilia iliyochakatwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi; ushiriki wa watanzania katika uuzaji wa bidhaa na utoaji huduma; na fursa nyingi za ajira kwa watanzania hususan katika kipindi cha ujenzi na hata katika kipindi cha uendeshaji wa mradi.
5. pia tumefanya uamuzi wa kuanzisha Eneo Maalum la Kiuchumi (Special Economic Zone) kwenye eneo la mradi ambapo kutakuwa na vivutio mbalimbali, ikiwemo bei nafuu ya umeme, ili kuvutia viwanda na shughuli za kiuchumi katika mikoa ya Kusini.