Mkuu Pascal Mayalla tofauti ni muda na mahali zilipotolewa..lakini zote lengo ni moja..Kuna watu wanaichanganya kauli hii ya rais Magufuli na kauli hii ya mteule wake.
Hizi ni kauli mbili tofauti
P
Mayalla is very intelligent sema sasa"ukabila-usukuma " umemshinda, yaani kidogo tu aungane na "praise team" ya ibada ya kwanzaMayalla na ubaguzi wa kikanda,unamtetea magufuli kwa lipi?yeye ndiye aliyeruhusu hao wateule wake kuwa hivyo na hata wakitoa matamko ya kuhatarisha amani ulishaona anawakemea au kuwafanya lolote???sasa unawezaje kutofautisha hizo kauli mbili??kiujumla magufuli hana uchungu na tanzania na target yake kubwa ni kuifanya tanzania ichafuke na analitekeleza vzr kupitia kwa mshauri wake mkuu kagame.
Magufuli si msukuma mayalla simamia ukweli.
Kweli umesema kitu cha maana. Magufuri ndiye aliyeagiza kuwa polisi waue majambazi. Hata vile vifo vya watu kwenye viroba na watu waliouliwa MKIRU ni maagizo yake.Mkuu Pascal Mayalla tofauti ni muda na mahali zilipotolewa..lakini zote lengo ni moja..
2+2=4
3+1=4
Haha 😂 Mkuu ukweli huwa ni mchungu.
Pampeo ni nani hapa Tanganyika ?Kama kuna mwenye address ya Pampeo,
Naiomba.
P
YAMETIMIA maneno yako hapo juuKweli umesema kitu cha maana. Magufuri ndiye aliyeagiza kuwa polisi waue majambazi. Hata vile vifo vya watu kwenye viroba na watu waliouliwa MKIRU ni maagizo yake.
Hamna namna unaweza kumtenga JPM kutoka kwenye kauli na vitendo vya watu wake. Huyu RC Mbeya ni kichaa kabisa na JPM mwenyewe alisha kiri hadharani kuwa yeye mwenyewe ni kichaaa na ndiyo maana anachagua vichaa wenzie kama yule Luhaga Mpina waziri wa mifugo. Tuendelee kupiga goti kwa imani ya dini zetu ili Mungu atuepushe na utawala huu wa kifedhuli.
Ila naamini Mungu atatenda 2020, huyu mtu JPM hatufai.
Wanabodi,
Wewe kama mwana JF, unapata an added advantage to be the first to know, ambapo leo katika tukio la maboresho ya jeshi la polisi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ametoa kauli kwa kutumia fasihi, ambapo ameliamuru jeshi la polisi, kukabiliana na majambazi wenye silaha kwa "kuwanyang'anya silaha kwa haraka haraka" ambapo polisi wameruhusiwa kutumia mbinu za medani, (kivita) (MM) ambazo hutumiwa na majeshi wakati wa vita, ambapo kazi huwa ni moja tuu, kumteketeza adui!.
Amri hiyo kwa Jeshi la Polisi, inamaanisha, Polisi hawahitaji tena kuwakamata majambazi wanaotumia silaha, bali kukabiliana nao kwa kuwaua papo kwa papo, na polisi wataofanya mauaji hayo ya kuwauwa majambazi hayo papo kwa papo bila kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, hawatafikishwa tena mahakamani, kama zamani, bali sasa watapandishwa vyeo!.
Agizo hilo limepokelewa kwa shangwe na makofi kwa kila aliyekuwe pale ila makofi ya ajabu ni ya IGP Ernest Mangu, aliitikia kwa kichwa as if ni amri halali. Kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao. Kazi ya jeshi ndio kuua adui. Sasa CinC anapotoa amri ya jeshi kwa polisi halafu IGP anashangilia, hii inaonyesha IGP Mangu is wrong man at a wrong place!. Sisi wengine seriousness ya mtu unaiona usoni, it's very unfortunately sijawahi kuiona hiyo serious face ya kijeshi kwenye uso wa IGP Mangu, sasa kama CinC ni dikiteta halafu IGP ni soft, sijui kama ataweza ku cop nae!. Let's wait and see.
Rais huku akisema kwa msisitizo kwa kutumia fasihi ya "kuwanyanganya silaha kwa haraka haraka", kwa vile majambazi wanatumia silaha, zenye risasi kufanya ujambazi, na jeshi la polisi nalo wanazo silaha zenye risasi, haoni kwa nini majambazi hayo yasinyang'anywe silaha zao kwa haraka haraka!.
Namna pekee ya kunyang'anya silaha jambazi mwenye silaha, ni kwa kumalizana nao, papo kwa papo kabla silaha hiyo haijatumika.
Sina shaka kabisa na nia njema ya dhati ya rais wetu Magufuli kwa jeshi letu la polisi na Watanzania kwa ujumla kufuatia kukithiri kwa vitendo vya ujambazi wa kutumia silaha, hivyo rais ametoa amri, hiyo, kufuatia nchi na wananchi kuchoshwa na vitendo vya ujambazi kuongezeka, vituo vya polisi kuvamiwa na polisi wetu kuuwawa.
Lakini pamoja na nia njema rais wetu, katika utekelezaji wa amri hiyo, ni kuwatangazia vita majambazi wanaotumia silaha kuwa ni "ama zao ama zetu". wakijua kuwa wakikamatwa tuu watauwawa right away, then, amri hii badala ya kupunguza ujambazi wa kutumia silaha, ndio kwanza inaweza kuchochea impunity kwa majambazi wanaotumia silaha, kuzitumia silaha hizo kwa kuwawahi polisi na chochote kilichopo mbele yao, na wakati huo huo kuligeuza jeshi letu la polisi kugeuka Gestapo!.
Lengo la Majambazi Wanaotumia Silaha.
Lengo la ujambazi wowote ni kuiba mali. Majambazi wanatumia silaha, lengo lao sio kuua bali kutumia silaha hizo kutishia na kukiwepo resistance ndipo hutumia kuua ili kulazimisha, kujihami au kupoteza ushahidi.
Sio majambazi wote wanaotumia silaha, huzitumia silaha hizo kufanyia mauaji!, sio silaha zote zinazobebwa zinakuwa loaded!, wengine huzitumia kutishia tuu, lakini hawana nia ya kufanya mauaji, na kuna wengine hubeba silaha ambazo hazina risasi, na wengine hutumia toy pistor
true!,na majambazi wengine, hubeba silaha, na ziko loaded, lakini hawafanyi mauaji baada ya kupata walichotaka!.
Tumeshuhudia majambazi yakiingia bank kuamrisha wote laleni chini. Wanapora kisha wanakwenda zao bila kufanya mauaji yoyote!. Tumeshuhudia mabasi yanatekwa, abiria wanashushwa wanasachiwa wanaporwa wanachiwa uhai wao.
Lakini kufuatia amri hii sasa, hao majambazi wenye huruma na maisha ya watu, hawatakuwa na huruma tena, na kama polisi ndio kwanza wamekuwa licenced to kill kwa mtindo wa MM, then every encounter kati ya majambazi na polisi na majambazi, tutegemee nothing, no justice but just blood bath!.
Tangazo hili litawaponza polisi wetu kugeuzwa an easy target ya majambazi wanaotumia silaha kwa kuwatarget kwanza polisi wa doria na kuwauwa wote kisha ndipo wafanye ujambazi wao na sijui kama hata wale wanaotumia silaha kwa lengo la kutishia, wataendelea kutishia au sasa watazitumia ipasavyo?!.
Tanzania ni nchi ya kidemokasia inayofuata katiba yenye kuzingatia misingi ya haki na utawala wa sheria!, amri kuu ya kwanza ya haki, ni "no one is condemned unheard", yaani hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Amri hii ya rais, imewapa mamlaka polisi, sio tena kuchunguza, kukamata na kuwapeleka majambazi wanaotumia silaha, mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, bali sasa polisi hawana tena haja ya kukamata na kufanya uchunguzi, bali kukitokea tuu tukio la uhalifu wa kutumia silaha, polisi wamepewa mamlaka kuwa ni wachunguzi, prosecutors, mahakimu tena kwa kutoa "capital punishment", na hakuna tena haja ya kumsubiri rais kuzisaini hizo hati za capital punishment, bali, wao wenyewe kutumia MM, kuitekeleza adhabu ya kifo, na baada ya hapo kusubiria kupandishwa vyeo!.
Just imagine mashindano ya kupanda vyeo miongoni mwa polisi wetu!.
Kama wanasheria wetu, hawatashitushwa na amri hii ya rais, nitaamini sasa Watanzania wameanza kumwelewa rais wetu, na ukiisha elewa, huna haja ya kuhoji!.
Angalizo: Sitetei vitendo vyovyote vya uhalifu wa aina yoyote, bali natetea utoaji wa haki!, hata jambazi anayetumia silaha, anastahili kutendewa haki!. Natolea mfano wa nchi mbili za Marekani na Uingereza. Miaka ya nyuma nchi zote hizi zilikumbwa na vitendo vingi vya mauaji kwa kutumia silaha, na zote ukipatikana na hatia ya 1st degree murder, unahukumiwa adhabu ya kifo. Uingereza ikafuta adhabu ya kifo!, vitendo vya mauaji, vikapungua kwa kiasi kikubwa!. Marekani ikaendelea na adhabu ya kifo, vitendo vya mauaji bado vimeongezeka!.
Amri ya kuwaua majambazi papo kwa papo, sio lazima itapunguza ujambazi, inaweza kuwa haitapunguza ujambazi, bali itawafanya hao majambazi ndio kugeua wauwaji wakuu, kwa hoja za "ama zao, ama zetu" na kwenye tukio lolote la ujambazi wa kutumia silaha, polisi wakitokea, sasa sio tena kutuliza amani bali kufanya a blood bath!, hivyo polisi sasa pia wanaweza kuwa ni an easy target ya majambazi!.
Kwetu sisi waandishi, ikitokea polisi wakakutana na gun mike, au boom mike, au hata kamera wakaiona ni kama sihaha!, kama ilivyotokea kwa Daudi Mwangosi!, askari mhusika, atapandishwa cheo!. Kama wale vijana wa Zombe, sasa watazawadiwa vyeo!.
Huko nyuma niliwahi kushauri, kama katiba ni kikwazo, rais Magufuli, aiweke pembeni kidogo hii katiba na badala yake atawale kwa kutumia 'presidential decrees' tuu!. Hivyo kwa amri hii ya polisi kuua majambazi papo kwa papo, kama mahakama ni kikwazo, pia anaweza kuiweka mahakama, pembeni kidogo, kwa kuwapatia polisi uwezo wa kimahakama kwa kutoa hukumu za kifo cha papo kwa papo kwa majambazi wanaotumia silaha, tena hatua itaokoa sana fedha nyingi, maana majaji wa mahakama zetu, wanahudumiwa kwa gharama kubwa sana!.
Wasiwasi wangu kwa amri kama hizi, sio ili kuokoa maisha ya majambazi wanaotumia silaha, au kuwaacha tuu majambazi wanaotumia silaha kuua, lakini pale polisi wetu watakapo wahiwa na kuuliwa kabla, tuta
piga tuu kelele, no!, wasiwasi wangu ni utekelezaji wa amri za aina hii, zisije kuwa kwa majambazi ni mwanzo tuu, baadae amri kama hizi za 'kinyemela' zikaelekezwa kwa makundi mengine, yanayoonekana ni kero!.
Mwaka 1976, kulifanyika mauaji ya wazee waliokuwa wakituhumiwa kuwa ni wachawi. Serikali kupitia waziri wa Mambo ya Ndani kipindi hicho, Ali Hassan Mwinyi, kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mwanza, chini ya RC Peter Kisumo, RSO, RPC, DSO, na OCD wakadhamiria kwa kauli moja kukomesha vitendo hivyo kwa hizo hizo MM alizoamrisha Magufuli zitumike!.
Katika Mahojiano, yaliyoendeshwa eneo la Kigoto, watuhumiwa wawili, Masanja Makula Mazengenuka, na Isaack Mwanamkoboko, walipoteza maisha!.
Mwalimu Nyerere alikasika sana, Waziri Mwinyi, IGP, Pundugu, Director wa TISS Mzena, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Kisumo, RSO, RPC, DSO na OCD wote wakastaafishwa kwa manufaa, na wengine kupandishwa kizimbani, ambapo wote walifungwa, isipokuwa mshtakiwa mmoja tuu ambaye ni Mzee wangu, tena aliokoka kwa vile tuu alikuwa anatetewa na wakili Murtaza Lakha!.
Utendaji wa Jeshi la Polisi unaongozwa na kitu kinachoitwa General Police Orders (GPO or GOP) ambacho tumekirithi kutoka kwa Waingereza kama tulivyorithi sheria zetu mbalimbali, ambazo zina maelekezo yote ni kwenye mazingira gani polisi anaruhusiwa kutumia silaha kuwadhibiti wahalifu na kuna polisi maalum wa kazi hiyo wanaoitwa snipers au wadunguaji, ambao wana shabaha na uwezo wa kulenga maeneo rasmi ya kulenga ili kumdestabilize mhalifu kwa lengo la kumkamata lakini sio kwa lengo la kumua!. Agizo la jana la Rais Magufuli, ni kuwaelekeza polisi kuua tena kwa haraka bila kuchelewa, na sasa kwa kila mauaji ya polisi, polisi hao badala ya kupandishwa kizimbani, sasa watapandishwa vyeo!.
Japo lengo la agizo hilo la rais, amelitoa kwa dhamira njema,(in good faith), lakini utekelezaji wake, unaweza kuligeuza jeshi letu la polisi kugeuka Gestapo!, na polisi wetu wakafanywa ni asusa ya majambazi wanaotumia silaha kwa kuwa wahi kabla hawajawahiwa!.
Kama sheria, taratibu na kanuni zipo, kwanini zisifuatwe?. Kama zimepitwa na wakati na imethibitishwa hazisaidii, tuzibadili rasmi.
Nalishauri Jeshi la polisi litoe takwimu za matukio yote ya ujambazi wa kutumia nguvu kumetokea vifo vingapi vya askari na raia kabla ya amri hii na takwimu za baada ya amri hii.
Hata Adofu alipoanza, alianza hivi hivi kwa kuwa a populist leader, anayeshangiliwa sana na umati wa watu!, ni baadae sana, ndipo watu wakaja kugundua, walimshangilia kila alichofanya akafikia kuwa unstoppable, by the time wanashtuka, it was too little too late, wakaishia kujuta!, kwa upande wetu, chonde chonde twendeni taratibu jamani, tufungue macho kuhusu hizi amri za mdomo ambazo hazijaandikwa popote, tushtuke mapema before it is too late, tusije kujuta!.
Jumamosi Njema.
Paskali
Rejea.
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa .
Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa ..
Wanabodi,
Wewe kama mwana JF, unapata an added advantage to be the first to know, ambapo leo katika tukio la maboresho ya jeshi la polisi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ametoa kauli kwa kutumia fasihi, ambapo ameliamuru jeshi la polisi, kukabiliana na majambazi wenye silaha kwa "kuwanyang'anya silaha kwa haraka haraka" ambapo polisi wameruhusiwa kutumia mbinu za medani, (kivita) (MM) ambazo hutumiwa na majeshi wakati wa vita, ambapo kazi huwa ni moja tuu, kumteketeza adui!.
Amri hiyo kwa Jeshi la Polisi, inamaanisha, Polisi hawahitaji tena kuwakamata majambazi wanaotumia silaha, bali kukabiliana nao kwa kuwaua papo kwa papo, na polisi wataofanya mauaji hayo ya kuwauwa majambazi hayo papo kwa papo bila kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, hawatafikishwa tena mahakamani, kama zamani, bali sasa watapandishwa vyeo!.
Tanzania ni nchi ya kidemokasia inayofuata katiba yenye kuzingatia misingi ya haki na utawala wa sheria!, amri kuu ya kwanza ya haki, ni "no one is condemned unheard", yaani hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Amri hii ya rais, imewapa mamlaka polisi, sio tena kuchunguza, kukamata na kuwapeleka majambazi wanaotumia silaha, mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, bali sasa polisi hawana tena haja ya kukamata na kufanya uchunguzi, bali kukitokea tuu tukio la uhalifu wa kutumia silaha, polisi wamepewa mamlaka kuwa ni wachunguzi, prosecutors, mahakimu tena kwa kutoa "capital punishment", na hakuna tena haja ya kumsubiri rais kuzisaini hizo hati za capital punishment, bali, wao wenyewe kutumia MM, kuitekeleza adhabu ya kifo, na baada ya hapo kusubiria kupandishwa vyeo!.
Jumamosi Njema.
Paskali
Rejea.
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa .
Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa ..
Polisi waliruhusiwa kuua!, sasa wanasubiri kupandishwa vyeo.Taarifa kutoka kwenye kikao cha familia ya Marehemu Mwise Simon na Mgare Mokiri , ambao ni miongoni mwa wale waliouawa na Jeshi la Polisi kwa madai ya Ujambazi , imefikia Uamuzi wa kutoshiriki wala kuhusika na Mazishi ya ndugu zao hao waliouawa mithili ya Wanyama wakorofi wa mwituni .
Familia hiyo inataka uchunguzi huru ambao utathibitisha Ujambazi wao na pia wanataka kujua Sababu hasa za kuuawa kwao , maana kuwa jambazi bado siyo tiketi ya mtu kuuawa , maana katika Magereza za Tanzania wamo wafungwa waliotokana na Makosa ya Ujambazi , kwanini hawa pamoja na kukamatwa lakini bado wakauawa ?
Binafsi : Naunga mkono Msimamo wa Familia hiyo .