kipipili
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 1,589
- 186
please kuwa mtoto wa mkulima siyo kuwa mkulima, hata Bill Gates anaweza kuwa mtoto wa mkulima. Mbona Mengi naye ni mtoto wa mkulimaFredy Azzah
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana walimkaribisha chuoni kwao Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa bango lililoandikwa "Mtoto wa Mkulima, Tunalala Nje", kilio kilichomsukumu mtendaji huyo mkuu wa serikali kuahidi kukichangia Sh10 milioni kila mwaka kwenye ujenzi wa malazi yao hadi ukomo wa uongozi wake.
Huyu kweli ni "Mtoto wa Mkulima"? Jameni, idadi ya wakulima nchini ni 80% ya wananchi wote, je watoto wa wakulima wenye uwezo wa kutoa mchango kama huu nchini ni wangapi? Nasemea "watoto wa wakulima" wanao tegemea kilimo kujikimu, siyo watoto wa mafisadi. Au ndo muendelezo wa usanii? Watoto wa mafisadi wametoa ngapi? Kumbe Bongo hatuhitaji misaada, kama mtoto wa mkulima anatoa zote hizo msaada wa nini? Vinginevyo naona kama ni muendelezo wa filamu ya KISANII TU!