Hii ni Tenda ya ajabu kabisa: Tenda kama hizi ni kifo cha sekta binafsi,nani aliziruhusu?

Local contractors inabidi wajirekebishe wenyewe kwanza, gharama zao zilikuwa haziakisi uhalisia, utakuta karibia 20% ya gharama inaishia kwenye rushwa, ubora wa kazi zao una walakini pia. Kuanza kutumika kwa taasis za ki serikali kwenye ujenzi kutaongeza ubunifu na ushindani. Wakandarasi waanze kuungana na kukataa kutoa rushwa, ndio njia pekee ya kuweza kushindana na taasis za kiserikali.
 
Hawawezi kwenda nje maana wengi wao sio competent.
Watanzania tulishazoea kua wababaishaji ni vigumu kufanya kazi na watu wa nje ambao wengi wao sio wababaishaji.
Angalia miradi mingi inayochukuliwa na wahandisi wetu kutoka private sectors na wengine kutoka serikalini mingi inakua miradi ya hovyo(haina ubora unaoendana na thamani).

Kama uliwahi kufika au kusoma UDSM kuna venues zinaitwa Nyerere Theatre zilijengwa mda mrefu sana na watu wa nje sasa angalia zile Yombo 4 na 5 za juzi zilizojengwa na watanzania wenzetu zimepasuka nyufa nyingi na zimezeeka kuzidi Nyerere Theatre zilizojengwa miaka mingi iliyopita.

Kwanini waende nje? Hao wa nje wao hawana wakandarasi wao? Hebu jaribu hata kupeleka kandarasi ya ku'supply' vitumbua Kenya uone cha moto!
 
Nadhani muhusika hakuwa na haja ya kutangaza tenda ya ushindani kama tayari alishatambua watu wa kumfanyia kazi,angeenda moja kwa moja kwa SUMA JKT,Tanzania Building Agency au VETA akawapa makaratasi ya tenda kisha akachagua wa kumfanyia kazi.

Mbali na kiingereza cha hovyo,huu ni ubaguzi dhidi ya makampuni ya binafsi,ubaguzi wowote ni wa kupingwa na kila mtu

View attachment 501183
Tatizo lako ni lugha tu hiyo ni restricted tenda kwa vendors ambao wanatoa national services kama Suma JKT, TBA nk. Na inaruhusiwa na sheria zetu
Kama imekukwaza muombe Mbunge wako ashauri sheria ibadirishwe siyo kutoa povu
 
Kwanini waende nje? Hao wa nje wao hawana wakandarasi wao? Hebu jaribu hata kupeleka kandarasi ya ku'supply' vitumbua Kenya uone cha moto!
Una ushahidi usio tiliwa shaka wa haya uliyoyaandika?
=====
Kenya wako tayari kushirikiana na wakandarasi wetu. ndiyo maana wakaamua kufanya kongamano kubwa mwezi June mwaka huu litakaojumuisha wakandarasi wetu watakaopenda kushirikiana nao
Fuatilia link hii hapa chini

East African Roads & Corridor Conference
 
Wengi humu watupu kwenye procurement ivo wanalalama restrictions tender ni method of procurement bnj

Utaratibu wa aina hii mtakuja kuuona madhara yake, hasa wale ambao ni wagumu sana kuelewa. Haya mashirika na makampuni ya serikali si walipa kodi wakubwa katika nchi hii. Kila siku tunaosikia wanaodaiwa kodi kubwa katika nchi hii ni akina Dewji, Manji, TCC, TBL n.k. Sijawahi kusikia Suma JKT au TBA wanalipa kodi kiasi gani kwa serikali... Baadaye akili itakuja kuturudia tu. Uzuri mmeshasema wenyewe mapena... Tutaisoma namba.
 
Mbona tayari waraka ulishatoka since mwaka jana. Hakuna kusafiri kwa airline yoyote isipokuwa bombadier kwa safari official ndani ya TZ

Na sisi watu binafsi tumeshapokea waraka unaosema hakuna kusafiri kwa bombardier, ni fastjet pekee. Ngoja tuone nani atakuwa anaruka na abiria wasiozidi 10.
 
Nadhani muhusika hakuwa na haja ya kutangaza tenda ya ushindani kama tayari alishatambua watu wa kumfanyia kazi,angeenda moja kwa moja kwa SUMA JKT,Tanzania Building Agency au VETA akawapa makaratasi ya tenda kisha akachagua wa kumfanyia kazi.

Mbali na kiingereza cha hovyo,huu ni ubaguzi dhidi ya makampuni ya binafsi,ubaguzi wowote ni wa kupingwa na kila mtu

View attachment 501183

Sekta binafsi walizidi kwa 10%
 
Una ushahidi usio tiliwa shaka wa haya uliyoyaandika?
=====
Kenya wako tayari kushirikiana na wakandarasi wetu. ndiyo maana wakaamua kufanya kongamano kubwa mwezi June mwaka huu litakaojumuisha wakandarasi wetu watakaopenda kushirikiana nao
Fuatilia link hii hapa chini

East African Roads & Corridor Conference

WANACHOTAKA WAKENYA NI SOKO LETU NA SI VINGINEVYO. HIZO ZOTE NI BIDII ZA KUWALAZA WAJINGA!
 
Wanafanya haya kumfurahisha Mkuu. Hii tayari ni pre-qualification na bora tu wangewapelekea hizo bidding docs hao SUMA, VETA, JKT na TBA. Kwa trend hii, very soon kila Afisa wa Serikali atapigwa marufuku kupanda ndege nyingine yoyote tofauti na our dear bombers
Wapigwe marufuku mara ngapi mkuu. Hilo mbona tayari limeishaanza kutekelezwa!
 
Local contractors inabidi wajirekebishe wenyewe kwanza, gharama zao zilikuwa haziakisi uhalisia, utakuta karibia 20% ya gharama inaishia kwenye rushwa, ubora wa kazi zao una walakini pia. Kuanza kutumika kwa taasis za ki serikali kwenye ujenzi kutaongeza ubunifu na ushindani. Wakandarasi waanze kuungana na kukataa kutoa rushwa, ndio njia pekee ya kuweza kushindana na taasis za kiserikali.
Mkuu rushwa INADAIWA na watoa kazi.
Mambo yakiendelea hivi wakandarasi mwzgeni ugali maana mboga ndo inamwagwa, mambo yawe hadharani.
 
Makandarasi mlizidi wizi. kujenga chini ya viwango ndo zilmekuwa zenu. Leo mnashangaa wodi. Yale madarasa? magorofa yanayoanguka? Jirekebisheni muone kama hamtarudiwa. Eti mna bodi! Isiyo na macho kuona mlivyo jenga public buildings zinazopasuka kabla ya matumizi. Ile miradi ya maji? Barabara mbovu? Dawa ni nyie KUJIREKEBISHA na siyo kulalama. Miradi mnapewa miaka na miaka haiiishi na mmepokea malipo kw a 200% na zaidi.

Ndicho nilikuwa nakifikiria juu yao. Waliweka mazoea kupiga pesa tu na wanaowapa tenda, bila kujijenga na kufikiria mbeleni now wanaisoma namba kwa kujitakia wenyewe.
 
Mkuu rushwa INADAIWA na watoa kazi.
Mambo yakiendelea hivi wakandarasi mwzgeni ugali maana mboga ndo inamwagwa, mambo yawe hadharani.
Huo ndio ukweli kama wakandarasi wataendelea kutoa rushwa ili kupata kazi, quotation zao zitakuwa juu sana zaidi ya taasis za serikali, wao ndio wana jukumu la kuanza kuwachoma wanaotaka rushwa vinginevyo ndio hivi wanapotezwa polepole.
 
Tulishajaribu huko nyuma kutumia mbinu za fundi mwashi 'kuwateua' wachunga mbuzi, wawindaji na wapagazi kusimamia na kuleta mapindizi ya viwanda tukashindwa. Njia ya kuwafanya wenye interest na mambo husika ndio waingie huko na kufanya hizo kazi ilionekana ndio sahihi maana inaondoa lawama hata kwa vizazi vijavyo.
Hakuna uhakika hii michakato inatupelekwa kutuzika wapi maana kufa tutakufa lakini bora tungelipewa japo uhuru wa tuzikwe wapi.
Hebu msome Mkuu M7 anasemaje kuhusu sekta binafsi na maendeleo ya nchi:

https://web.facebook.com/PresidentYoweriKagutaMuseveni/
Addressed all government accounting officers who are attending a conference in Kampala today.
I urge government officials to support and facilitate the growth of the private sector because it is what will create jobs.
We made the decision as way back as 1987 to support private-sector led growth when some people still thought that they would create jobs through parastatals.
Like in China, some government enterprises will work and we shall keep them, but the main approach will be through the private sector.
Radio stations should support this. They are duty bound to teach about the future of the country.
Let them spend three hours abusing Museveni and five or six educating masses on the future of the country.
We should all know that wealth is created through commercial agriculture, industry, services and ICT.
CAOs should work with local leaders to attract investors to your areas, get land ready and call Hon Anite (Investments Minister), so that your areas attract investments.
M7.jpg

iparamasa
 
Ni kweli nimepotea kule kwa muda!
======
Sijui, mkuu hiki ni kijembe nini; kama hoja zangu zina mapungufu hapa, tafadhali nionyeshe mapungufu hayo ili nirekebike. Maana hili nalo ni tija kwangu katika kutumia JF.
Hapana mkuu Sana, mm ni kijana napenda Sana mnavyoelezea mambo basi tuu hawa mamod wamenifungia kuchangia kwenye ule Uzi niwapige maswali wazee wangu.
 
Huo ndio ukweli kama wakandarasi wataendelea kutoa rushwa ili kupata kazi, quotation zao zitakuwa juu sana zaidi ya taasis za serikali, wao ndio wana jukumu la kuanza kuwachoma wanaotaka rushwa vinginevyo ndio hivi wanapotezwa polepole.
Mkuu elewa nilichoposti.
RUSHWA INADAIWA na watoa kazi.
Na ni miradi midogo hadi mikubwa kabisa.
 
Wanafanya haya kumfurahisha Mkuu. Hii tayari ni pre-qualification na bora tu wangewapelekea hizo bidding docs hao SUMA, VETA, JKT na TBA. Kwa trend hii, very soon kila Afisa wa Serikali atapigwa marufuku kupanda ndege nyingine yoyote tofauti na our dear bombers

Wahindi na makampuni binafsi ambayo si yakitanzania yalikuwa yanatumalizia hela...bora hela sasa zirudi katika serikali ya tanzania...AM SOOOOOO HAPPY
SOON NEEMA ITAONEKANA TANZANIA
 
Back
Top Bottom