kadovela
JF-Expert Member
- Jan 31, 2016
- 471
- 679
MIMI MKINGA NIKIFA DAR KUPITIA UMOJA WA WAKINGA WAISHIO DAR NINAUHAKIKA WA KWENDA KUZIKWA BULONGWA KANDO NA ALIPOZIKWA BABA BILA WASIWASI. NI RAHISI MWILI WANGU KUSINDIKIZWA HADI MAKETE NA WAKINGA WENZANGU. ITAHITAJI KUPIGA SANA MAGOTI NA KUBEMBELEZA ILI MTU AMBAYE HATA MAKETE HAKUJUI KUKUBALI KUSINDIKIZA MAREHEMU. DAR NI KUBWA MTU KUJUA MAREHEMU WANATOKA SEHEMU MOJA NI RAHISI KUPITIA HIVI VIKUNDI MAANA WANA UTARATIBU WA VIKAO, MAWASILIANO NA MICHANGO MFANO NAKUFA SAA 1 ASUBUHI KUFIKA SAA 7 MCHANA NIPO KWENYE JENEZA ZURI, NIMEPAKIZWA KWENYE COSTA NAELEKEA MAKETE SASA BILA HIVI VIKUNDI MAMBO YA KUPITISHA BAKULI HADI IFIKE MILLION 2 ZA MIPANGO YA KUSAFIRISHA MAREHEMU MBONA NITAKUWA NIMEANZA KUOZA KABISA. KUTENGANA KIKABILA TANZANIA NI NGUMU KUJA TOKEA MAANA TUMEINGILIANA SANA KUPITIA NDOA NA MAHUSIANO MENGINEO MENGI. VIKUNDI HIVI VIENDELEA VINA FAIDA SANA. MTU AKISIKIA MZARAMO MWENZAKE ANATATIZO ATAMSAIDIA HATA KAMA HAMFAHAMU ILA BILA KUTAJA ASILI ZETU NI NGUMU MTU KUKUSAIDIA KAMA SI WAKARIBU YAKO.