Hii katuni ya Kipanya hatari, sio kwa mbeleko hii

Uzuri wa katuni hii ni kuwa hakuna mwenye nguvu,babu amechoka mpaka ana mkongojo mkononi na aliyebebwa ni mtoto na silaha iko nyuma huku wanavuka maji.
Yaaani wew ndio una IQ kubwa kuliko wote waliochangia hapa
 
Siku ile pale stetihausi walivyoitwa waandishi habari, nakumbuka kama vile aliongelea suala la Kipanya kumchora kichwa kikiwa kimechongoka!!!!!
 
..Magufuli na Makonda wanamvutia kasi Masoud Kipanya, ipo siku ataingia kwenye mtego wao na hapo atakiona cha moto.

Nadhani hapa itakuwa Bor huko South Sudan na huyo jemedari wa Vita atakuwa Le general Salva Kiir Mayardit akivuka mto na mwanae. Magu na mwanane wasijishuku hapa..
 
FB_IMG_1489698109295.jpg

Na hii je?
 
Uzuri wa katuni hii ni kuwa hakuna mwenye nguvu,babu amechoka mpaka ana mkongojo mkononi na aliyebebwa ni mtoto na silaha iko nyuma huku wanavuka maji.
Duuh basi mimi nilitafsiri mkongojo kama fimbo ya kupimia KINA CHA MAJI
 
Mto ni nchi

huyo mtoto aliyebebwa ni Daud
na hyo mbereko maana ake ni ushirika

Huyo mbebaji ni mkulu

hyo fimbo ni kiashiria cha kutokua na uwezo wa kutembea mpaka utumie mguu wa tatu

hyo silaha ni nyenzo inayotumika kunyanamazisha Viumbe wenye vidomodomo kwenye huo mto japo wana haki ya kusema kisheria!

hilo jua ni nyakati.

wapo katikati ya mto wanavuka na jua linazama .je watafika salama kabla jua kuzama?
 
Kisasi kizuri ni mafanikio. Mh Magufuli kaza buti Mh Makonda kaza buti. Mafanikio yenu si ya kutafutwa kwa tochi kila mwenye milango ya fahamu hata mmoja atafahamu mafanikio yenu. Kuimarika shirika la ndege, mateja kupungua na wauzaji kukamatwa, foleni Dar kwisha na tija kuongezeka, reli ya kiwango, viwanda vya sukari ya kukidhi mahitaji yetu,watumishi wenye kuwajibika na kuto huduma bora kwa wananchi, serikali kuhamia Dodoma na kusogeza huduma za kiutawala kwa wananchi. Hivi ndivyo vitakuwa vigezo vya kuipima kama serikali inaweza kuwaletea watu wake maendeleo.
 
Umesahau mafanikio ya kutisha watu, udikteta, kuvamia studio za watu, kusingizia watu tuhuma za uongo Gwajima mbowe manji
 
Uzuri wa katuni hii ni kuwa hakuna mwenye nguvu,babu amechoka mpaka ana mkongojo mkononi na aliyebebwa ni mtoto na silaha iko nyuma huku wanavuka maji.
Haiko tu nyuma ila ishafyatua risasi zote zimeisha
 
Back
Top Bottom