Hii imekaaje wakuu mume na mke kusali dini tofauti wakati bado wako pamoja ndoani?

Wakatoliki wanakubali mseto wa imani mradi tu ndoa ifungwe kanisani kwao na watoto watakuwa wakatoliki wakipenda. Kuna mama mmoja hapa ni mkristo sijui wa wapi ila mume wake ni muislam, wamezaa kitoto naona kinavalishwa kiislam ila mama huvaa kiislam akitaka na wakati mwingine huvaa kawaida tu. Kuna mmoja tena mke ni msabato bwana ni mkatoliki ila kahamia usabatoni kwa mkewe. Mchanganyiko kama huo haupo kwa wapentekoste na hairuhusiwi.
 
Asante kwa ufafanuzi
 
Inaweza ikaonekana si vibaya kuoana dini/imani/dhehebu tofauti kwa dhana ya mapenzi hayana mipaka. Ishu itakuja wakati wa kufanya ibada kuna mmoja atakereka na ibada ya mwenzake. Fikiria unasali jumuiya nyumbani kwako halafu mwenzako ni muislam/dhehebu jingine ataishia kutoka hapo kama ataheshimu au kuponda na kudharau imani ya mwenzake. Inapendeza sana wanandoa wakiwa dini/dhehebu/imani moja
 
Mume na Mke kuwa dini tofauti ni changamoto kubwa. Ukweli ni kwamba hao wote hawaithamini dini. Ni watu holela. Siku mmojawapo atakapoanza kuthamini dini yake, ndoa itakuwa njia panda
 
Habari,

Moja kwa moja kwenye mada. Hii imekaaje wakuu mume na mke kusali dini tofauti wakati bado wako pamoja ndoani?.

Kwa maana kuna majirani zangu hapa mmoja mke anasali Katoliki yeye Mwislam na mwingine mke anaswali kwenye dini ya Uislam ume Anglican.

Je, haiwezi kuathiri ndoa?.

Uzi tayari
Kama wao wamekubaliana kukaa hivyo, wewe unataka kukaa katikati yao?
 
Habari,

Moja kwa moja kwenye mada. Hii imekaaje wakuu mume na mke kusali dini tofauti wakati bado wako pamoja ndoani?.

Kwa maana kuna majirani zangu hapa mmoja mke anasali Katoliki yeye Mwislam na mwingine mke anaswali kwenye dini ya Uislam ume Anglican.

Je, haiwezi kuathiri ndoa?.

Uzi tayari

Kwani kuna mkristo anasali ? Ni sala gani hiyo?
 
Habari,

Moja kwa moja kwenye mada. Hii imekaaje wakuu mume na mke kusali dini tofauti wakati bado wako pamoja ndoani?.

Kwa maana kuna majirani zangu hapa mmoja mke anasali Katoliki yeye Mwislam na mwingine mke anaswali kwenye dini ya Uislam ume Anglican.

Je, haiwezi kuathiri ndoa?.

Uzi tayari
Kama umri wake ni zaidi ya miaka 18 anaweza akachagua Imani anayoitaka Wala hakuna ajabu.
 
Kuna dhehebu moja wao hawakutaka mabinti na vijana wao waolewe/waoe nje na dhehebu lao. Kama kijana wa nje akitaka kuoa hapo itabidi awe muumini wao. Waliona madhehebu mengine hata kama wanafanana kiimani na wao kuwa ni wadhambi, hawajakamilika kiimani
 
Back
Top Bottom