Habari za jioni wa na jf
binafsi Naona hii dhana ya majipu sasa imeanza kuvamiwa na wahuni kiasi inakosa maana na kuanza kutumika vibaya na watu wenye chuki binafsi, zinazotokana na wao kukosa umahiri kiutendaji na hivyo kutumia silaha ya kutumbua majipu kama ngao ya kukatisha tamaa watu wanaojituma na wenye umahiri wa kazi.
tukirejea uzi uliowekwa hapa jamvini na mtu aliyejitambulisha kama nyundo ya chuma (mpelelzi binafsi ) uliobebwa na kichwa cha habari "Waziri na katibu wizara ya afya mna maslahi gani na ntlp ?".
kwanza hii akaunti ndio kwanza ina siku mbili na post moja,na katika mazingira ya kawaida utaona wazi ni akaunti ambayo mtu kafungua kwa madhumuni tu yakuchafua hali ya hewa na kutoa upotoshaji,kwa kujivika vilemba vya upelelezi binafsi ama whistle brower.
Binafsi huyu mama aliyedaiwa kuwa jipu ninaufahamu utendaji wake. Ni mchapa kazi mahiri na asiyependa wazembe, hivyo sishangai kuona vita na majungu yakipigwa dhidi yake. ni ukweli usiopingika bi beatrice Ameibadilisha sana hiyo program unayoisema kuwa imepoteza muelekeo na kufanya jamii ya tanzania kwa kiasi kikubwa kuwa na uelewa wa gonjwa la kifua kikuu.
Hata hao wafadhili unaowasema wanalifahamu hilo na wanasadiki kuwa utendaji wake umetukuka. na Hayo madai ya wafadhili kupunguza fedha hayana mashiko na yanadhihirisha ni jinsi gani ulivyo na upeo mdogo maana wafadhili wamepunguza pesa kila mahali ndani ya Tanzania mpaka serikali kuu. kwafupi Hayo madai hayaleti maana yoyote kwa mtu mwenye akili zake timamu
sana sana nikitizama naona ndugu nyundo ya chuma umechungulia vibaya dhana utumbuaji jibu na ukadhani mh rais wetu JPM ni wale wanaoishi kwa kusikiliza maneno ya watu pasipo kufanya tafiti zake kama dr.
mi naomba na huku jf tuanze kutumbua majipu kama wewe,ambao mnakurupuka toka huko mlikotumwa na kuanzisha vi thread visivyo na kichwa wala miguu mkidhani kupitia humo humo walipopita mashujaa wachache na wakweli nanyi mtafanikiwa na chuki binafsi
ili jamii ielewe vyema kuwa 'dhana ya majipu si kwaajili ya upotoshaji na kueneza chuki binafsi bali ni kuimiza uwajibikaji na uzalendo'