Hii bajeti ya kodi za Pombe toka nasoma hadi leo, hivi Gesi, madini yanafaida gani kwa Mtanzania?

Nchi haina vyanzo vya mapato vya kiume kiume namaanisha vyanzo vyenye mashiko na ndomana imebakia kutafta fedha kwa mwananchi wa kawaida kwa kumkamua had ndururu yake,..taasis za serikal zenye dhamana kwenye madin,utalii,anga,maji,hazifanyi kaz yake,so hakuna jipya,no export,nchi inapataje pesa,.kutwa ku discourage sekta binafsi,mara toen pesa weken nmb,mara panden ndege za serikal tuu etc,nchi haiwez pata pesa za maana kwa kumkamua maskin wa chin kabsa na mfanyakaz,.vipaumbele vyetu havina mashiko,ma flyover,mara madege meng meng,.hiv haya mabilion yangewekezwa kwenye kilimo,yaan kuwe na projects za mabilion yaan ma plantation ya kufa mtu,mashamba makubwa ya mazao ya biashara kila mkoa,watu waajiriwe huko wakae vijana huko maelf na maelf na wajengewe viwanda huko vya kuboresha mazao tuanze ku export hizo bidhaa nje tupate foreign currency,lakin wap,kutwa budget za kusadikika,mwaka jana trilion 28 sjui 29 huko,zilizokusanywa ni tril 18 tuu kumi zote hakuna,.af tutegemee mabadiliko?
Mkuu umeongea jambo la maana sana imefika wakati tupate vyanzo vipya vya mapato sio hayo hayo kila mwaka.... tukuze sekta zingine ili tupate mapato zaidi

Pia naona ni vzuri sasa tuwe na vipaumbele vichache vinavyotekelezeka kwenye bajeti ya maendeleo yaani kuliko kuigawa gawa hela kidog kidogo kwa miradi kibao ni heri kma taifa tuamue labda bajeti ya mwaka huu strictly tuwekeze kwenye kilimo...... au mwakani strictly kufufua viwanda !!! Pesa inayopatikana ikielekezwa kwenye mambo machache makubwa naona itasaidia sana kuharakisha miradi mikubwa ya kimaendeleo kukamilika na kuleta mabadiliko kwa wananchi wa kawaida

Ahsante
 
all mining contracts (MDAs) are subject to public disclosure; acha uongo. Ninakushauri uwe unasoma nyaraka za sera husika kabla ya kutoa matamshi yako kwenye public.
Kma ipo kwa public disclosure mbona ile mikataba 17 aliyosaini kikwete na china mpaka leo imebaki siri nzito??? Haya je ile mikataba ya TPDC iliyoombwa na PAC mbona mpaka leo kizungumkuti??? Hizo clause za uwazi zipo kwenye makaratasi tu ila kwenye uhalisia mambo yamefanywa siri sana
 
Hakuna kazi ngumu kama kuwaongoza watanzania, hata wao mpaka leo hawajui wanataka nini, wanalalamika motor vehicle itolewe maana hata gari haitembei deni na fain unaendelea, sasa imetilewa wameanza kupiga kelele kama kuku wameingiliwa na kicheche kwenye banda lao, akili mbovu kabisa.
 
Tuko kwenye pipeline ya kuleta viwanda. Kodi ni lazima itoke kwenye vyanzo asili vya kodi. Uwezo wa wachumi wetu ndipo umejikita huko
 
Gesi na madini wanagawana wao wanakula ten percent zao wanashidagani na wewe kapuku
 
Kutegemea pombe kwenye budget ni tatizo. Hata wanywaji wamechoka, japo baa kukaukiwa wateja kunahusishwa na wapiga dili. Inataka hela za pombe lakini inazuia pombe zisiuzwe, mpaka saa 10!. Walevi wapo wachache, wengi ni wanywaji wakiwa ama wanapumzika baada au kati ya kazi, au wakijadili mipango ya kazi. Bei zinashushwa na wazalishaji na bado bia hazinyweki, ngoja tuone zikipanda kwa ongezeko la kodi.
 
Hapo kwenye pombe kasoro kidogo kwan kipindi tulikuwa tunapiga maji toka asubuhi yani muda wowote we ukienda unapata Huduma na ilikuwa km unaweza kukesha ni wewe tu sasa Siku hizi kuanzia 10 join mpaka 5 usiku tu.Halo imekuwa ngumu so wanywaji nao wamepungua sn mauzo yameshuka sana ktk hilo soko so kuendelea kutegemea huko wakat mazingira sio rafiki ni hata sn.
Tuendelee kumuomba Mungu maana kuwa na bajet ni suala moja na kutekelezeka au la ni suala lingine.
 
Hivi baada ya kulipia usajili wa gari unapokua umelinunua si ndio basi ama huwa zina mwendelezo kwa kipindi fulani
 
Kma ipo kwa public disclosure mbona ile mikataba 17 aliyosaini kikwete na china mpaka leo imebaki siri nzito??? Haya je ile mikataba ya TPDC iliyoombwa na PAC mbona mpaka leo kizungumkuti??? Hizo clause za uwazi zipo kwenye makaratasi tu ila kwenye uhalisia mambo yamefanywa siri sana
Ninadhani wewe unaongea hearsay na kisha kuathiriwa na generalisation. PAC iliomba lini mikataba hiyo na ilikuwaje ikashindwa kutumia mamlaka yaliyowekwa ndani ya sheria hiyo? Ua unataka kuwa PAC haijui kuwa kuna sharia hiyo? This is totally fallacious. Mikataba ya gesi inaitwa PSAs na hadi sasa kuna mikataba 26 tu ya kutafuta, kuendeleza na kisha kutakuwa na mikataba ya kuchimba na kuuza gesi asilia. Na kwa mujibu wa sheria, mikataba hii husainiwa na waziri wa nishati na madini, sasa kama Kikwete alisaini mikataba hiyo unayosema mbona hakuna kampuni hata moja miongoni mwa makampuni wawekezaji kwenye kwenye gesi asilia? Ninakushauri uachane na hearsay, bali utafute kujisomea na kujua ukweli.
 
Ninadhani wewe unaongea hearsay na kisha kuathiriwa na generalisation. PAC iliomba lini mikataba hiyo na ilikuwaje ikashindwa kutumia mamlaka yaliyowekwa ndani ya sheria hiyo? Ua unataka kuwa PAC haijui kuwa kuna sharia hiyo? This is totally fallacious. Mikataba ya gesi inaitwa PSAs na hadi sasa kuna mikataba 26 tu ya kutafuta, kuendeleza na kisha kutakuwa na mikataba ya kuchimba na kuuza gesi asilia. Na kwa mujibu wa sheria, mikataba hii husainiwa na waziri wa nishati na madini, sasa kama Kikwete alisaini mikataba hiyo unayosema mbona hakuna kampuni hata moja miongoni mwa makampuni wawekezaji kwenye kwenye gesi asilia? Ninakushauri uachane na hearsay, bali utafute kujisomea na kujua ukweli.
Mkuu ilishawahi kuomba hyo mikataba enzi hizo ikitwa POAC kma unatakaa taafifa zaidi soma hapa

The Chief: Gas City: Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (Poac) yataka mikataba ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam

Mkuu hawakusema kwenye sekta ya gesi pekee ila kikwete alisaini mikataba 17 ambayo ni siri mimi na wwe hatujui kwani uongo sasa ulitegemea uone wapi siri za mkataba hyo??

Xi Jinping kusaini mkataba ujenzi wa Bandari Bagamoyo

Mkuu walipoidai spika aliishia kuivunja kamati hyo na mpaka leo hakuna aliyewahi kujua kilichomo kwenye mikataba hyo waliyoomba hao POAC hasa ule wa bomba la gesi na bandari!!!!


PAC wanajua kuwa kuna sheria hizo lakini kumbuka tanzania ni signatory wa OGI ambao unatala uwazi kwenye mikataba na kwamba iwe wazi kwa public kila makubaliano ya serikali yanapofanyika!!! Ssa kma hatutaki uwazi tulisaini nni hyo OGI

Mkuu issue hapa ni kwamba mikataba iwekwe wazi mambo yote yajulikane ila hya ya kujifungua chumbani na kusani mikataba ya kuuza nchi tutaishia kulia lia tu kila cku afu tukihoji unasema eti HEARSAY!
 
Watu hawajui kuwa akija mwekezaji akatafuta madini kwa gharama zake,akaanza uwekezaji,akaleta mitambo,akaajili watu,
akaanzauzalishaji akilipa kodi ya ardhi,akilipa kodi mbalimbali za local government,

hiyo dhahabu inayopatikana sio yetu tena,hapo chetu ni malipo ya mrahaba na corporate tax labda kama tuko nae ubia ndo tunaweza gawana mapato nusu kwa nusu
 
Tunamalizia kuchekecha mchanga kontena la 207 hali ni nzuri mana maji ni mengi hapa bandarini kule acacia maji ya shida sana ndio mana tunaibiwa;sisi chama chakavu ni shida na huwezi amini mpka sasa tumepata dhahabu 15 tons bado copper,silver etc,.....kidumu chama chakavu kichaka cha wezi na mafisadi
 
Back
Top Bottom