Hii 10% inayotakiwa kukatwa kwenye miamala ya kutoa pesa kutumia simu, naomba nieleweshwe

Nibaada ya kukatwa pesa ya muamala ulio ufanya
Malipo hayo yatakatwa 10%
Kama kutuma 10000 ada ni sh 300
hiyo 300 itakatwa 10%
ambayo ni sawa na Tsh30
Asante mkuu nimekuelewa vizuri,maana nilitaka nianze kuwa natuma ela kupitia njia ya basi sasa.Ili kabiashara kangu kasije kufa nikahangaika kutembeza bahasha.
 
Hata kama ni makampuni yanakatwa, msisahau kuwa mfanyabiashara yeye faida yake iko palepale. Hii inamaana kwamba tegemeeni gharama zinazotozwa kwenye huduma hii kupanda ili mfanyabiashara aweze kulipa hiyo kodi na kubakiza faida yake ikiwa intact
Well said
 
Wakuu,

Hii imekaaje kuwa ukimtumia mtu pesa wakati anaitoa, serikali itakuwa inachukua kodi ya 10%?.

Nikimtumia mtu sh laki tano,serikali inakata kodi ya elfu hamsini, hivi kuna ukweli wowote hapo?

Wakuu nisaidieni.

Ni 10% ya gharama isije kuwa humo kwenye 88 tukapata taabu ya kuelezea. Siku ingine unasoma between lines lakini kuuliza kwako utaokoa 88 wenzako kibao Na tayari washaingia Chaka wanalalama Tu.
 
  • Thanks
Reactions: F9T
Wacheni kudanganya
Kodi hiyo ilikuwa ikikatwa siku nyingi tu
Ispokuwa haikuwa na maboresho
Na hiyo inahusika na kiwango unacho katwa na mtandao wako
Mfano unatuma tsh.50000
voda utakatwa 600
serikali itachukua 10% ya 600

Kodi ya zuio ipo hasa mawakala wa mpesa,tigo pesa na airtel money
Hawapokei malipo yao bila kukatwa 10%
Afadhali umetoa ufafanuzi, nilishaanza ogopa
 
Nadhani hiyo ni % ya unachokatwa, make hata vodacom nimeambiwa na wakala ambae namtumia kutuma pesa kuwa kuna baadhi ya miamala imepanda kiwango cha kutuma na kutoa pesa.
 
Yaani kama natuma ada ya Mwanangu ya milioni moja niweke Na laki moja ya kutolea.

Hii biashara sasa ni kama anasa.

Pamoja Na pesa kubwa inayozunguka kwenye mitandao lakini asilimia kubwa wanaofanya hivyo ni wakulima, wafabiashara wadogo, Na kiasi kidogo wafabiashara wa kati.

Wafabiashara wakubwa hawahangaiki na Mpesa au Tigo pesa.

Huduma za kipesa zimechangia sana maendeleo kwa Watanzania wa kawaida hasa wa vijijini.

Labda kama Serikali inampango wa kufuta hii biashara baada ya kuona wanachuana Na Mabenki nchini.

Nawaza tu, ni kundi lipi litakaloendelea kumshangilia Mtukufu Rais.?
Haya ni mawazo yako ama utafiti! Unajua kiasi kinachotembea kwa siku kwenye huduma za kifedha za mitandao ya simu? Hivi haujui kuwa ni changamoto kwa mabenki! Umesema wakulima! By the way unahisi mkulima na mtu wa kawaida sana! Au huamini kwamba kuna baadhi ya wakulima wenye hela! Usiwe na mawazo ya aina hiyo! Rafiki yangu aliyeacha chuo kwa kukosa ada sasa ni Mkulima, amejenga,ameoa na ana hekari zaidi ya 50! Hebu tafuta wafanyakazi wenye mafanikio kama hayo! Wenzako wanalima matikiti huku Tabora na wanaleta Semi toka Dar kufuata na kuuza huko kwenu kwa wafanyakazi! Point yangu usidharau kada fulani ya watu. By the way huyo tajiri unayemsema hizo hela huwa anazipokea kwa lundo kwa kupitia fuso au! Ofcoz jibu ni kidogo kidogo na njia ya kupokea pesa moja wapo kati ya nyingi ila yenye uharaka na inayotumiwa sana ni mitandao ya simu. Nenda hapo kariakoo kafanye research ujue per day kiasi gani hutengenezwa! Haya umeshawahi kutuma pesa rafiki? Kuna makato ya aina mbili, mosi we unayetuma unakatwa kiasi lakini hiwa kidogo pia yule anayepokea ndio hukatwa zaidi. Sasa kile ambacho unakatwa mtumaji kilikuwa hakitozwi kodi. Just think kuna watu wangapi wanatuma fedha per day? Hiyo ni biashara ndogo! Unajua kwamba Tanzania ni namba mbili kwa matumizi makubwa ya simu Africa? Sitetei hoja ya bajeti ila nilitaka utoe ideology ulioanza nayo tulitazame jambo hili kwa upana wake. Asante
 
Wacheni kudanganya
Kodi hiyo ilikuwa ikikatwa siku nyingi tu
Ispokuwa haikuwa na maboresho
Na hiyo inahusika na kiwango unacho katwa na mtandao wako
Mfano unatuma tsh.50000
voda utakatwa 600
serikali itachukua 10% ya 600

Kodi ya zuio ipo hasa mawakala wa mpesa,tigo pesa na airtel money
Hawapokei malipo yao bila kukatwa 10%

Likely ndiyo hivyo

Lakini kama wamepandishiwa kodi maana yake kampuni za simu nazo zitahamishia huo mzigo kwa mlaji tu

Kwa hiyo, whether we like or not unafuu wa maisha ya maskini haupo na pengine ndiyo maangamizi zaidi!!
 
Haya ni mawazo yako ama utafiti! Unajua kiasi kinachotembea kwa siku kwenye huduma za kifedha za mitandao ya simu? Hivi haujui kuwa ni changamoto kwa mabenki! Umesema wakulima! By the way unahisi mkulima na mtu wa kawaida sana! Au huamini kwamba kuna baadhi ya wakulima wenye hela! Usiwe na mawazo ya aina hiyo! Rafiki yangu aliyeacha chuo kwa kukosa ada sasa ni Mkulima, amejenga,ameoa na ana hekari zaidi ya 50! Hebu tafuta wafanyakazi wenye mafanikio kama hayo! Wenzako wanalima matikiti huku Tabora na wanaleta Semi toka Dar kufuata na kuuza huko kwenu kwa wafanyakazi! Point yangu usidharau kada fulani ya watu. By the way huyo tajiri unayemsema hizo hela huwa anazipokea kwa lundo kwa kupitia fuso au! Ofcoz jibu ni kidogo kidogo na njia ya kupokea pesa moja wapo kati ya nyingi ila yenye uharaka na inayotumiwa sana ni mitandao ya simu. Nenda hapo kariakoo kafanye research ujue per day kiasi gani hutengenezwa! Haya umeshawahi kutuma pesa rafiki? Kuna makato ya aina mbili, mosi we unayetuma unakatwa kiasi lakini hiwa kidogo pia yule anayepokea ndio hukatwa zaidi. Sasa kile ambacho unakatwa mtumaji kilikuwa hakitozwi kodi. Just think kuna watu wangapi wanatuma fedha per day? Hiyo ni biashara ndogo! Unajua kwamba Tanzania ni namba mbili kwa matumizi makubwa ya simu Africa? Sitetei hoja ya bajeti ila nilitaka utoe ideology ulioanza nayo tulitazame jambo hili kwa upana wake. Asante

Mkuu hapo ndio umetoa jibu, hizo zingene story tu asante.!
 
Back
Top Bottom